Mbunge Catherine Magige yuko maji ya shingo uchaguzi UWT Arusha

Mbunge Catherine Magige yuko maji ya shingo uchaguzi UWT Arusha

buswelu moja

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
226
Reaction score
183
MBUNGE CATHERINE MAGIGE YUKO MAJI YASHINGO UCHAGUZI UWT ARUSHA.

Wadau wa JF,

Wakati uchaguzi wa UWT wilayani Arusha ukitaraji kufanyika kesho hali imeelezwa kuwa mbaya sana kwambunge wa viti maalumu mkoani Arusha,Bi Catherine Magige.

Hali hiyo imemlazimu achanganyikiwe na kuanza kugawa fedha kwa wajumbe kutoka wilaya za mkoa wa Arusha kama njuguna taarifa za ndani zinadai tayari milioni 20 tangu jana imekuwa ikisambazwa na wapambe wake kwa wajumbe hao.

Lakini kituo ni kwamba le Magige amelazimika kumwangukia mkuu wa mkoa wa Arusha,Daud Felix Ntimbenda amwokolee jahazi linalotaraji kuzama kesho.

Inadaiwa kuwa Magige anamtumia mkuu wa mkoa huyo kuwatisha baadhi ya wagombea na wajumbe akiwemo hasimu wake Violet Mfuko ambaye anampa joto Magige kwenye uchaguzi wa kesho na inasemekana kama haki ikitendea basi ataibuka kidedea.

Magige,anapita mitaani akitamba kwamba ana mahusiano ya kimwili na RC huyo hivyo amemwahidi kumbeba katikauchaguzi wa kesho hizi taarifa zimesambaa kwa kasi hapa Arusha.

Tukio jingine ni kwamba mwenyekiti wa UVCCM,Robinson Meitinyiku wa hapa mkoani Arusha pamoja na yule wa UWT,Flora Zelothe wanatengenezewa zengwe na Magige kwakuwa wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kumwangusha katika uchaguzi wakesho.

Taarifa zinadai kuwa leo Robinsonalish atakiwa kwa RC ARUSHA kwamba yeye ndiye anayesambaza picha ya Catherine akiwa na Bernad Membe ambaye alihaidi kumsaidia katika uchaguzi wa kesho huku Zelothe akifuatwa ofisini na maofisa wa Takukuru kwa madai kuwa anagawa rushwa kama mojawapo ya vitisho na kuna taarifa kwamba maofisa hao wamemnyang'anya simu zake zote za mkononi.

Kituko kingine kuna mtumishimmojawapo wa idara ya uhamiaji mkoani Arusha aliyetambulika kwa jina moja la Ally amesimamishwa kazi kwa amri ya mkuuwa mkoa wa Arusha kwa madai kuwa yeye ndiye anasambaza ujumbe wa kumchafuaMagige na kesho ameitwa kwenye kikao cha maadili hapo ofisini kwao.

Kuna mengi tutasikia uchaguzi wasafari hii lakini kinachoonekana Catherine ataangukia pua kwa kuwa tangu apeweubunge alikimbia Arusha na sasa amerudi tena kuomba ridhaa wajumbe wamesema NO.

Inasemekana mchuano wa kesho ni kati ya Catherine na Viola kwani Zelothe ambaye ni mkiti wa UWT anamuunga mkono Viola.

Kesho ni kesho tutawapasaha mengiwadau wa jukwaa hili lakini taaarifa za kuelekea uchaguzi zinakuja kila hatuakuanzaia sasa hivyo mkae mkao wa kula.

CHANZO: MDAU WA ARUSHA

Pichani chini ni Violet Mfuko (aliyevaa miwani),Flora Zelothe (aliyeshikilia kipaza sauti) na Catherine Magige akiwa bungeni kwenye vikao vilivyopita vya Bunge la Jamhuri.

Attachments

  • sam_2660[1].jpg
    sam_2660[1].jpg
    40.3 KB · Views: 1,431
  • bunge[1].jpg
    bunge[1].jpg
    18 KB · Views: 1,377
  • b23[1].jpg
    b23[1].jpg
    39.9 KB · Views: 1,340
Mbona sijawahi kumsikia akisema lolote huko mjengoni? Jamani si mmpe nafasi hata hg wangu mbona angewatetea ma hg wengine?? Hii kodi yangu, mmejua namna ya kuitafuna. Bila jashoooo kazi kuuza uzuri wenyu tu Dodoma. Hamkosekani kuitikia ndiyooooo
 
Wabunge wa viti maalum hawana kazi yoyote ni wasting of money tu. Hakuna mbunge wa viti maalum wa kunidanganya eti atafanya hivi au vile.

Mbunge wa viti maalum anayejitambuwa ni yule atakayesimama kitaifa zaidi kama Easter Bulaya hapo ndipo unapoweza kutengeneza political mailage.
 
Takukuru arusha mko wapi?Alex magige mdogo wa damu wa Catherine magige mbunge wa vitu maalumu mkoani arusha kupitia uvccm anagawa rushwa kama njugu akiwa kwenye gari Noah nyeusi mitaa ya kaloleni muda huu
 
waambie wazichukue halafu wamtie adabu kwenye sanduku la kura, na hao wanaopewa pigeni mawe mkiulizwa waambien polisi tumepinga rushwa wala hamtafungwa
 
Takukuru arusha naomba kuuliza Alex magige mdogo wa damu wa Catherine magige ambaye Ni mbunge wa viti maalumu mkoani arusha kupitia uvccm anagawa rushwa kama njugu,Yuko na gari Noah nyeusi mitaa ya kaloleni muda huu ,fedha inagawiwa kama njugu kwa maelekezo ya Catherine hii inatisha Kuna mil 20 kwenye gari Hilo sasa hivi Wako tenki la maji wanakimbia maeneo ya mkusanyiko kwa kuwa Leo Catherine simu zake zote zimeshikiliwa na takukuru.
 
Uwiii......wapo wapi niwawahi..........
naishi karibu na tanki la maji........very close mkuu.........nielekeze.......
 
Uwiii......wapo wapi niwawahi..........
naishi karibu na tanki la maji........very close mkuu.........nielekeze.......

Ni wakati wa mavuno yatakayogeuka mavune baada ya uchaguzi
 
Magige cathe anagombea kwa tiketi ya chama gani ??
Hicho chama ndio kilaumiwe sio huyo mtoa rushwa. Ile rushwa nyingine ya chini kwa chini nayo anatoa ?
 
Mi nilidhani huyo Catherine ni mmoja wa wanabend wa Jide........kumbe ni mbunge tena Arusha.......?.......
well..........hayo ya CCM kwa makamanda haituhusu sana........watajijua wenyewe.......
 
Catherine Magige.......ni beautiful hajawahi kuchangia bungeni hata siku moja.....Hansard zipo kuthibitisha......au yupo bungeni kwa kazi maalum.Akipitishwa tutalazimika kuamini vinginevyo
 
Huyu Catherine alikuwa mwanafunzi wangu Enzi hizo pale Arusha Meru secondary, Pia ni mtoto wa Mwalimu Valentine Magige.

Kumbe wewe ni KIZEEE, ndo maana akili yako ilishajichokea. Kuanzia leo sitakaa nishangae tena hoja zako za kizeee....
 
Takukuru arusha naomba kuuliza Alex magige mdogo wa damu wa Catherine magige ambaye Ni mbunge wa viti maalumu mkoani arusha kupitia uvccm anagawa rushwa kama njugu,Yuko na gari Noah nyeusi mitaa ya kaloleni muda huu ,fedha inagawiwa kama njugu kwa maelekezo ya Catherine hii inatisha Kuna mil 20 kwenye gari Hilo sasa hivi Wako tenki la maji wanakimbia maeneo ya mkusanyiko kwa kuwa Leo Catherine simu zake zote zimeshikiliwa na takukuru.

We unatangaza kuna mil 20 utafanya wale jamaa wa boda boda wamfate na SMG zao
 
mwenye picha ya huyo mrembo Catherine atuwekeee plz maana ka hata alikuwa hachangii hata kwa sura hatumjui
 
Takukuru arusha naomba kuuliza Alex magige mdogo wa damu wa Catherine magige ambaye Ni mbunge wa viti maalumu mkoani arusha kupitia uvccm anagawa rushwa kama njugu,Yuko na gari Noah nyeusi mitaa ya kaloleni muda huu ,fedha inagawiwa kama njugu kwa maelekezo ya Catherine hii inatisha Kuna mil 20 kwenye gari Hilo sasa hivi Wako tenki la maji wanakimbia maeneo ya mkusanyiko kwa kuwa Leo Catherine simu zake zote zimeshikiliwa na takukuru.
Majanga! hii nchi khaa! mie naomba iuzwe kila mtu apewe chake alale mbele wai!
 
buswelu moja

Wenzake waliojitambua wanaingia majimboni,yeye kama ni kidume si asimame hapo na mh Lema?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom