Mbunge atimuliwa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge atimuliwa bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]MBUNGE wa Kasulu Mjini mkoani Kigoma, Moses Machali (NCCR- Mageuzi) leo jioni amejikuta akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Spika wa Bunge Anne Makinda wakati mjadala wa kupitisha Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano 2011/2016 yakiendelea kutokana na kuvaa mavazi kinyume na Kanuni za Bunge hilo.

  Machali alitakiwa akabadili nguo hizo ambazo ni shati la Kaunda suti ya bluu na suruali nyeusi baada ya Mbunge wa Karagwe, Godbless Blandes (CCM) kuomba mwongozo wa Spika kwa kutumia kanuni ya 146 kifungu kidogo cha kwanza na cha tatu kinachozungumzia mavazi anayotakiwa kuvaa Mbunge ndani ya eneo la bungeni.

  “Kwa mujibu wa kifungu hiki Mheshimiwa Spika, Mbunge anatakiwa awe nadhifu, nimeamua kusimama kwa sababu nimeguswa na mavazi ya Mheshimiwa Machali ambaye amevaa shati moja na suruali nyingine, naomba mwongozo wako Mheshimiwa Spika,” alisema Blandes.

  Akijibu mwongozo huo Makinda, alimtaka Machali atafute namna ya kutoka nje ili akajirekebishe, ambapo Mbunge huyo alitoka huku akicheka na kushangiliwa na wabunge wa chama chake.

  Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la mwaka 2007, kifungu cha tatu kinachoainisha mavazi ya Mbunge mwanamume, kinamtaka avae suti ya Kiafrika na shati la mikono mirefu au mifupi lenye ukosi wa mviringo au shingo ya kawaida na fulana ndani au bila fulana lakini vyote suruali na shati vikiwa vya rangi moja isiyo na nakshi pamoja au bila kibarakashia.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  acha wafukuzane tu....hamna maslahi ya taifa hapo
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndio wabunge wengine wanaweza zaidi, kuangali nani kavaa nini... sikuwahi kudhani kuvaa rangi tofauti ni kosa na kutawanya vikuku si kosa!!!

  Karagwe kweli wamechagua this time
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hv siziga yule jamaa anayejiita paka mweusi siku hz yupo wapi?maana sioni kabisa comments zake hapa JF
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuwa nadhifu ni vipi kwani. Basi bunge liwashoneshee uniform.

  Itapendeza wakiwekewa sheria wavae suti nguo zilishoneshwa Tanzania. Itakuwa ni sheria nzuri sana. Huwezikusema suti ya Italy ninadifu kuliko lubega ya mmasai. ndo ukoloni wenyewe huo. Vivile igependeza h japo bunge liweke siku moja katika wiki ya wabunge wavae kitamaduni.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kama kavunja kweli basi sheria imefuata mkondo.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM wana vioja wala si hoja . Sasa kuvaa vile kulifanya Bunge liache kazi au ?
   
 8. d

  doctore. Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama ni sheria basi haina budi ifuatwe hadi hapo watakapoamua kubadili
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Pamoja na uwepo wa sheria, busara inabidi itumike. Kama mavazi ya mbunge hayaendi kinyume na utamaduni, mila na desturi zetu, hakuna sababu ya kumtoa. Na wabunge wa ccm sasa wafanye kilichowapeleka bungeni. Mambo ya upinzani hadi kwenye mavazi ni upuuzi na kupoteza muda wa kujadili mambo ya msingi. Sidhan kama wanakaragwe wamemtuma hayo mbunge wao!?
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wabongo bana, nguo zenyewe tumeanza kuvaa in the 1940's lakini mbwembwe nyingiiiiii!
   
 11. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mama wa Karagwe si ndio yule aliyechakachua matokeo ya uchaguz tena kwa kusaidiwa na polisi kwa kupiga mabomu ya machoz! Lol kumbe mdaku hv kuna haja gani kukagua mavaz ya wenzie?!
   
 12. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  alitamani pamba nini? Akaona akiendelea kukaa nazo angepoteza concentration, akaona bora tu amtoe
   
 13. v

  vivimama Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wizi mtupu
  mbona wanadada wa mmjengoni wanavaa vikuku au ndo iyo sheria haijatungwa bado!!!

  wanaochunguza vitu ivyo hata point zao za wasiwasi maana hawana hata muda kutafakari mustakabali wa wananchi walowaweka madarakani.
  mapenzi yangu
   
Loading...