Mbunge amlipua mfanyabiashara kuwa ni 'jasusi'

I'm waiting a detailed report from FMES and Enigma. Huu uchafu, naamini viinzi vilishatembelea siku nyingi, bado kupukuta mikono na miguu.

Huyu tangia amerudi bongo amekatwa kilimilimi, haongei siku hizi, nafkiri UWT na CCM wamempiga mkwara ha! ha! ha! Le Mutuz
 
Mbowe-na-Hamad-Rashid.jpg

Monday, 18 June 2012 21:02


Mbunge wa Wawi (CUF),Hamad Rashid Mohamed


Neville Meena, Dodoma



MBUNGE wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed jana aliilipua Kampuni ya Madini ya Minerals Extractions Technologies Ltd kutokana na mmiliki wake kufanya biashara za madini kwa njia za utapeli na ujasusi.

Minerals Extractions Technologies Ltd ni kampuni ambayo inafanya kazi ya kusafisha mchanga wa dhahabu katika baadhi ya migodi iliyopo Kanda ya ziwa na iliwahi kulalamikiwa kwa kukataa kushirikiana na mpango wa kufuatilia mapato yanayolipwa kwa Serikali na kampuni za madini, gesi na mafuta (TEIT) unaoongozwa na Jaji Msitaafu, Mark Bomani.

Kutokana na hali hiyo, Mohamed alitoa mapendekezo ya kuundwa kwa kamati ya wabunge sita kutoka Kamati tatu za Bunge ili kuchunguza kampuni hiyo na mmiliki wake ambaye (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye alisema kuwa anatamba kwamba Tanzania hakuna mtu anayeweza kumgusa.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Serikali ya 2012/2013, Mohamed alisema mwekezaji huyo anamiliki hati tano za kusafiria, tatu kutoka nchini kwake Belgium na mbili za Burundi na kwamba bado anaishi nchini licha ya kufukuzwa nchini na Serikali.

Mbunge huyo alisema katika hali ya kushangaza, taarifa za mwekezaji huyo ziliripotiwa polisi ili akamatwe katika hoteli ya Holiday Inn ya jijini Dar es Salaam, lakini kwa kuthibitisha kwamba amekuwa akiishi nchini kijasusi, taarifa hizo zilimfikia kabla ya kutekelezwa kwa mpango huo, hivyo aliwakwepa polisi kwa kukodi vyumba viwili katika hoteli hiyo na baadaye kuwatoroka.

“Huyu mtu aliwahi kumtukana Kamishna wa Nishati na Madini ambaye ni mbunge mwenzetu (Dk Dalaly Kafumu). Tumeshirikiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani (Pereira Ame Silima) na polisi walikwenda kumkamata lakini…ndo maana nasema ni jasusi, alikuwa amekodi vyumba viwili katika hoteli ya Holiday Inn kwa hiyo hakukamatwa,” alisema mbunge huyo.

Alisema mwekezaji huyo amekuwa akiliibia taifa mamilioni ya fedha kutokana na kufanya udanganyifu katika kiasi cha dhahabu ambacho amekuwa akikisafirisha kwenda nje ya nchi kila wiki na kwamba baadhi ya vyombo vya dola vinafahamu suala hilo lakini vimeshindwa kuchukua hatua.

“Huyu bwana amekuwa akisafirisha kila wiki kilo 15 za dhahabu kwenda nje ya nchi, lakini anafanya udanganyifu mkubwa hivyo kuliibia taifa mamilioni ya pesa, lazima Bunge hili lichukue hatua kwa kulifanyia kazi suala hili,” alisema Mohamed.

Alipendekeza timu ya wabunge itakayoundwa ijumuishe wajumbe wawili kutoka kamati za Bunge za Mambo ya Nje na Ulinzi na Usalama, Nishati na Madini na Kamati ya Fedha na Uchumi.

Mbunge huyo aliahidi kuwasilisha kwa Spika nyaraka kadhaa kuhusu kampuni hiyo na madudu inayofanya nchini, huku mmiliki wake akitamba kwamba anawamiliki Watanzania wote.

Habari ambazo gazeti hili lilizipata zimeeleza kuwa mbunge huyo alikuwa amewasilisha nyaraka mbalimbali katika ofisi ya Spika ambazo zilikuwa zikionyesha taarifa mbalimbali za mwekezaji huyo.

Miongoni mwa taarifa hizo ambazo Mwananchi imeziona ni namba za hati za kusafiria za raia huyo wa Ubelgiji ambazo ni EG 125092, EH 096587 na EI 590081 za Ubelgiji wakati hati zake za kusafiria kutoka nchini Burundi ni EE 132212 na EF 558746.

Nyaraka hizo pia zinaonyesha kuwa mwekezaji huyo anaishi nchini kwa hati ya daraja la kwanza (Class A) ambayo aliipata Novemba 2011 lakini ukweli ni kwamba yupo nchini tangu 2005, japokuwa hakuna taarifa zozote kwamba tangu wakati huo alikuwa akiishi nchini kama nani na kwa shughuli ipi.

Baadaye Mohamed aliliambia Mwananchi kuwa kuna udanganyifu mkubwa katika taarifa za uhamiaji kuhusu mwekezaji huyo na kwamba ujeuri alionao hata kwa viongozi wa Serikali, unatia shaka kwamba huenda analindwa na mfumo ambao unahitaji nguvu za Bunge kuuvunja.
 
hii mijitu imejaa sana pale Holiday inn mijambazi tu..inakwambia..we will pay transport and accomodation for you to dubai then we pay for your gold there..nenda uone..utajuta kuzaliwa....utaikuta imekaa pale restaurant kibao..kumbe mitapeli tu...inatumia mpaka magari ya security companies
 
Nakumbuka kipindi cha nyerere alisema alishawahi kumfukuza jamaa ambaye alisema ameiweka mfukoni serikali yake,lakini huyo mbeligiji anadunda hapa ingawa amesema watanzania wote(serikali ya kikwete plus wananchi wote) lakin jk yupo kimya tu kweli mnyika aliona mbali tumefikishwa hapa na udhaifu wa kikwete
 
wanaona mikataba yetu ilivyo loose na wanajiaminisha kuwa
hawatafanywa lolote
hivi ni ukihiyo wetu au magumash yanazidi?

hapo kwetu kenya mbona wao wakali sana...
sijasikia upmbav kama huu pande hizo laaah
Wanachojali ni maslahi yao binafsi na si yale ya nchi.
 
Japo nakubaliana na jambo hili kuwekwa hadharani, kwamba linaenda kusemewa bungeni ni dalili kubwa kwamba mfumo wa serikali (institutional set up) hauna utendaji (dysfuntional). Hili ni suala ambalo lilipaswa kushughulikiwa kikamilifu na Mambo ya Ndani bila hata ya kufikishwa bungeni. Itafikia mahali bunge litakuwa kama ndio polisi wa kushughulikia mafisadi, kuwajibisha mawaziri na viongozi wabovu, na kushughulikia watu kama huyu mwekezaji. Hii ni dalili ya a very dysfuntional government, kaput kabisa.
 
Kama nimegoogle vizuri taarifa zasema gold yetu ni carat ya 22 (second best) hivyo 15Kg ni $716,683.65
na hata kama quality yetu ni carat ya 10 (the lowest), 15Kg ni $325,907.40

Wadau inabidi nasie tuingie huko maana ni bora tuwe na wenzetu wanaoingiza hizi hela kwenye mzunguko
 
A member of parliamentary committee for Finance and Economy Hamad Rashid Mohamed yesterday accused a foreign investor Marc Rene Roelandts of possessing six traveling documents and abusing Tanzanians. He said Roelandts holds three Belgian passports with registration numbers EG 125092, EH 096287 and EI 590081 and two Burundi ones with number EE 132212 and EF 558746.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
Wakina Mnyika wakisema JK na serikali yake ni dhaifu,kuna mibwege inang'aka na kutokwa povu bila sababu,
haya sasa mgeni anaiba anatukana na anaichimba mikwara serikali,
Enzi za Nyerere huyo angeisha kimbia mwenyewe siku nyingi,
Lakini kwa kuwa aliyepo magogoni kazi yake ni kuhukumu wazawa na kuwakumbatia wezi acha waendelee kutamba tu.
 
Hii ndo maana yake. Pipi zetu atunyang'anya na konzi kutupiga, mbaya zaidi ni kwamaba atupigia kwetu
 
Back
Top Bottom