Mbunge amlipua mfanyabiashara kuwa ni 'jasusi'

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Mbunge amlipua mfanyabiashara kuwa ni jasusi
Monday, 18 June 2012 21:02

Neville Meena, Dodoma
Mwananchi


MBUNGE wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed jana aliilipua Kampuni ya Madini ya Minerals Extractions Technologies Ltd kutokana na mmiliki wake kufanya biashara za madini kwa njia za utapeli na ujasusi.

Minerals Extractions Technologies Ltd ni kampuni ambayo inafanya kazi ya kusafisha mchanga wa dhahabu katika baadhi ya migodi iliyopo Kanda ya ziwa na iliwahi kulalamikiwa kwa kukataa kushirikiana na mpango wa kufuatilia mapato yanayolipwa kwa Serikali na kampuni za madini, gesi na mafuta (TEIT) unaoongozwa na Jaji Msitaafu, Mark Bomani.

Kutokana na hali hiyo, Mohamed alitoa mapendekezo ya kuundwa kwa kamati ya wabunge sita kutoka Kamati tatu za Bunge ili kuchunguza kampuni hiyo na mmiliki wake ambaye (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye alisema kuwa anatamba kwamba Tanzania hakuna mtu anayeweza kumgusa.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Serikali ya 2012/2013, Mohamed alisema mwekezaji huyo anamiliki hati tano za kusafiria, tatu kutoka nchini kwake Belgium na mbili za Burundi na kwamba bado anaishi nchini licha ya kufukuzwa nchini na Serikali.

Mbunge huyo alisema katika hali ya kushangaza, taarifa za mwekezaji huyo ziliripotiwa polisi ili akamatwe katika hoteli ya Holiday Inn ya jijini Dar es Salaam, lakini kwa kuthibitisha kwamba amekuwa akiishi nchini kijasusi, taarifa hizo zilimfikia kabla ya kutekelezwa kwa mpango huo, hivyo aliwakwepa polisi kwa kukodi vyumba viwili katika hoteli hiyo na baadaye kuwatoroka.

"Huyu mtu aliwahi kumtukana Kamishna wa Nishati na Madini ambaye ni mbunge mwenzetu (Dk Dalaly Kafumu). Tumeshirikiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani (Pereira Ame Silima) na polisi walikwenda kumkamata lakini…ndo maana nasema ni jasusi, alikuwa amekodi vyumba viwili katika hoteli ya Holiday Inn kwa hiyo hakukamatwa," alisema mbunge huyo.

Alisema mwekezaji huyo amekuwa akiliibia taifa mamilioni ya fedha kutokana na kufanya udanganyifu katika kiasi cha dhahabu ambacho amekuwa akikisafirisha kwenda nje ya nchi kila wiki na kwamba baadhi ya vyombo vya dola vinafahamu suala hilo lakini vimeshindwa kuchukua hatua.

"Huyu bwana amekuwa akisafirisha kila wiki kilo 15 za dhahabu kwenda nje ya nchi, lakini anafanya udanganyifu mkubwa hivyo kuliibia taifa mamilioni ya pesa, lazima Bunge hili lichukue hatua kwa kulifanyia kazi suala hili," alisema Mohamed.

Alipendekeza timu ya wabunge itakayoundwa ijumuishe wajumbe wawili kutoka kamati za Bunge za Mambo ya Nje na Ulinzi na Usalama, Nishati na Madini na Kamati ya Fedha na Uchumi.

Mbunge huyo aliahidi kuwasilisha kwa Spika nyaraka kadhaa kuhusu kampuni hiyo na madudu inayofanya nchini, huku mmiliki wake akitamba kwamba anawamiliki Watanzania wote.

Habari ambazo gazeti hili lilizipata zimeeleza kuwa mbunge huyo alikuwa amewasilisha nyaraka mbalimbali katika ofisi ya Spika ambazo zilikuwa zikionyesha taarifa mbalimbali za mwekezaji huyo.

Miongoni mwa taarifa hizo ambazo Mwananchi imeziona ni namba za hati za kusafiria za raia huyo wa Ubelgiji ambazo ni EG 125092, EH 096587 na EI 590081 za Ubelgiji wakati hati zake za kusafiria kutoka nchini Burundi ni EE 132212 na EF 558746.

Nyaraka hizo pia zinaonyesha kuwa mwekezaji huyo anaishi nchini kwa hati ya daraja la kwanza (Class A) ambayo aliipata Novemba 2011 lakini ukweli ni kwamba yupo nchini tangu 2005, japokuwa hakuna taarifa zozote kwamba tangu wakati huo alikuwa akiishi nchini kama nani na kwa shughuli ipi.

Baadaye Mohamed aliliambia Mwananchi kuwa kuna udanganyifu mkubwa katika taarifa za uhamiaji kuhusu mwekezaji huyo na kwamba ujeuri alionao hata kwa viongozi wa Serikali, unatia shaka kwamba huenda analindwa na mfumo ambao unahitaji nguvu za Bunge kuuvunja.


 
Hiyo ndio Tanzania shamba la bibi mtu anakuja kuchuma anaingia na kutoka anavyotaka

Hivi nchi yetu hiko salama kweli? Huyu jamaa nani kampa taharifa kwamba anakuja kukamatwa kwa hiyo kupata muda wa kuwatoroka POLISI!

Watu wenye fedha wanachezea usalama wetu sana kwa kushirikiana na watu wenye dhamana ya kulinda usalama wetu wa ndani; nafikili hii ingekuwa ni wakeup call kwa JK ili aweze kuwashughulikia ma afisa ambao sio waminifu - sina shaka wanajulikana.

Tatizo hili la kutojali amri zinazotolewa na Viongozi wa juu limekwisha kuwa sugu nchini, mtu uwezi kuamini kwamba wakati mwingine some Principal/Permanent Secretaries wanadhalau amri ya Waziri, anakaa bila kutekeleza alicho ambiwa na boss wake hasa hasa jambo lenyewe likiwa linahusu maslahi yake binafsi kuliko TAIFA - hawachukuliwi hatua yoyote kwa kuwa Waziri na PS wote wanateuliwa na RAIS, nafikili hili linapashwa kuangaliwa upya ili uteuzi wa ma-PS utokane na Waziri Mkuu.
 
Embu mwekeni wazi kwa jina lake tumjue, ikiwezakana na picha kabisa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii ndo Tanzania, hawa UWT wakipewa za chapati tu, wanaufyata, wakisubiri uchaguzi mwingine wachakachue matokeo.
Haiwezekani mtu awakwepe kipuuzi hivyo.
 
na hao viongozi wa CCM wanajuwa ndo maana wanawalinda kwa hali na mali
 
Sina imani tena na tume yoyote ya wabunge, uzoefu unaonyesha wamekuwa wakipozwa halafu nao wanatuuza tu. Rejea mfano wa Mh. Badwell aliyetaka kupozwa kwa hesabu tu za Halmashauri, sembuse mshiko wa dhahabu!
 
Sniper na Wana JF,
Naongezea kidogo au kusahihisha, labda Director na Mmiliki ni watu wawili tofauti,
Maana taarifa inasema ni mmiliki hapa inasema Director.
Wenye Majina yake watujuze
Nawakilisha

Sniper na Wana JF,
Uki-google utapata yafuatayo:

Contact Person:Mr. Marc Roelandts (Director)
Company :Mineral Extraction Technologies Ltd
Address:plot 34 Nyakato Industrial Area, Mwanza, Tanzania
Telephone:255-786-516475


Mtaniwia radhi kama nimekosea

My Take: Wachache sana wenye Uchungu wa Nchi yetu, am Speechless.
Nawakilisha
 
I'm waiting a detailed report from FMES and Enigma. Huu uchafu, naamini viinzi vilishatembelea siku nyingi, bado kupukuta mikono na miguu.
 
nauma sana,inatisha hivi hawa mbwa mwitu kwa nini wasipigwe chini kweli watz tunamilikiwa na mtu mmoja,haya ndiyo aliyoyakataa yule mzanaki(nyerere)
 
Ba Hamadi kumbe yupo jamani anawakilisha kanda ya Ziwa huko bara na sio Wawi Znz?

Ukipanda upepo , utavuna Dhoba. Pole sana Ba Hamad
 
roho yangu inaniambiya huyu atakuwa ni Mbiya Mkubwa wa Raisi wetu wa Tanzania ,Raisi Jakaya Kikwete,akilindwa na Inspector General wa police , nd Saidi Mwema na chief of defence General Mwamunyange,najiuliza nchi hii ambayo iliwahi kupigana vita zaidi ya kumi kwa wakati mmoja wakati wa ukombozi wa nchi zilizoko kusini mwa Afrika ambazo ni Angola,Zimbabwe,south Africa,Namibia,Msumbiji, Wakati huo huo pia tukipambana na mamuruki wa afrika kusini ambao walikuwa Malawi,zaire, huku tukisaidia nchi zilizokuwa kwenye utawala mbovu za burundi,ruanda na Uganda na hakuna mbwa yeyote aliyevamia nchi hii,hakuna mbwa yeyote alikuja kuvuna madini yetu,hakuna mbwa yeyote alidhalilisha viongozi na nchi yetu
haiwezi kuingia kwenye akili yangu , Usalama wa taifa ,jeshi la polisi na Jeshi la wananchi,lingeweza kupata kigugumizi kwa jasusi linalotamba hapa nchini bila kuwa na msaada wa viongozi niliowataja hapa juu,wakumbuke kwamba historia ianawasuta viongozi hao nchi yetu ilikuwa kinara katika nyanja zote za kiulinzi na sauti ya maamuzi
 
usiangalie nani kasema ndio upanue mdomo, ni mTZ mwenzetu katupatia habari tum support tujue ukweli kwa maslahi ya nchi yetu

Huyo jamaa juzi alikuwa kwenye vyomba vya habari Mwanza, kagoma kulipa mkataba wa nyumba kafungiwa nje, sasa leo Hamad anakurupuka kuwa eti hajui alipo.
 
I'm waiting a detailed report from FMES and Enigma. Huu uchafu, naamini viinzi vilishatembelea siku nyingi, bado kupukuta mikono na miguu.
 
Back
Top Bottom