Mbunge akitekeleza majukumu ya jimbo anatoa msaada? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge akitekeleza majukumu ya jimbo anatoa msaada?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mbopo, Jun 6, 2011.

 1. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Juzi juzi nilisoma habari katika moja ya magazeti ya kila siku, likiripoti kwamba Mbunge wa Mvomero Mheshimiwa Amos Makalla ametoa msaada wa mipira 23 pamoja na seti za sare za michezo kwa vikundi vya vijana ambao ni wapiga kura wa jimboni kwake. Hili neno msaada lilinipa maswali kidogo hasa nikizingatia kwamba moja ya majukumu ya mbunge ni kutekeleza ahadi za chama chake kama zilivyoainishwa katika ilani yao ya uchaguzi, lakini vile vile kutekeleza ahadi zake mwenyewe. Mbunge pia ana wajibu wa kuhakikisha ustawi wa wananchi wa jimbo lake kwa kipindi chote cha ubunge wake. Sasa iweje kutekeleza majukumu haya kuwe ni msaada wakati aliomba kuchaguliwa na kuwaongoza wananchi wake ili atoe huduma hizo?

  Hii ikanikumbusha hoja ambayo aliitoa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Africa Mashariki wa Uganda (wakati huo) Eliya Kategeya ambaye alisema kwamba wapiga kura wa Afrika wanahitaji kupewa elimu ya uraia ili wajue haki na wajibu wao na akatoa mfano wa wapiga kura wa huko Uganda ambavyo wanaandaa nyimbo na sherehe za kumpongeza na kumshukuru mbunge au waziri aliyefanikisha ujenzi wa barabara, bila kujua kwamba ujenzi huo umefanikishwa kwa kodi zao hao wananchi na kwamba sasa wanalipwa kutokana na kodi zao hizo. Kwa hakika elimu ya uraia inahitajika pia hata kwa waandishi wanaoripoti matukio ya namna hii.
   
 2. n

  ndutu Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbopo, natamani ungeona jinsi wabunge wetu wanavyojipiga kifua na kutoa jeuri kwamba yeye anafanya hivyo kwa mapenzi mema kwa wananchi wao wakati ukifika wakati wa kura za maoni au uchaguzi wanapiga magoti wakiomba waongezewe muda kwa sababu kuna mipango waliyopanga na inahitaji muda kuitekeleza. Bure kabisa!
   
 3. m

  mudavadi Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hao wabunge wenyewe wanastahili kupewa elimu ili kujua kwamba hawafanyi favour yoyote kwa kufanya hayo wanayofanya. Na ndiyo maana wakishindwa kutekeleza tunawalaumu na kuwapiga chini.
   
 4. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hapa tatizo kubwa ni kwa wananchi kudhani kuwa mbunge ni mfadhili wa kuwasaidia au kuwatatulia matatizo yao. Hii inasababishwa na fulana, khanga na kofia tunazogawiwa kila wakati wa kampeni za uchaguzi.
  Mbunge akishachaguliwa anakuwa kimbilio la wananchi kutaka wasaidiwe kusomeshewa watoto wao, na matatizo kadha wa kadha. Ndiyo maana wabunge wetu siku hizi wakishindwa kwenye uchaguzi basi hung'oa vitasa kwenye ofisi, au hudai madawati waliyochonga walipokuwa madarakani.
   
 5. m

  mudavadi Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You are very right mkuu. Tena wanavyokasirika utadhani ubunge ni mali yao binafsi na wengi wao huishia kuondoka kwa kisukari au presha baada ya hapo.
   
 6. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hahahaaa! Thank you very much
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Elimu ya uraia yahitajika sana ili wananchi waelewe wajibu wa viongozi wanaowachagua...wananchi wamejenga hulka ya kuchagua watu wenye uwezo wa fedha kuwa viongozi wao na wanaishia kuwababaikia badala ya kuwatumikisha kulingana na nafasi walizochaguliwa.
   
 8. b

  banyimwa Senior Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa Dar mbunge wetu alitoa ahadi ya mambo ambayo angeyatekeleza katika siku 100 za kwanza za ubunge wake. Walipomfuata siku 200 baadaye na kumuuliza kulikoni akawajia juu na kuwambia kwamba hata mimba ikitunga huchukua miezi tisa ndiyo mtoto anazaliwa. Akawataka waache kumkera maana hata suti 4 hajanunua toka achaguliwe.
   
 9. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hao wana Mvomero wamepewa mipira na jezi ili wachezecheze na kusahau shida zao na ikifika 2015 wawe wapole na watoe tena kura zao. Hii ndo bongo bana, tumia ujinga na umaskini wa wananchi wako uwatawale milele. Well done Brother Amos Makala, Big up sana.
   
 10. b

  banyimwa Senior Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Very true. Kama huna hela wewe huna sifa ya kuwa kiongozi bora na vile visenti vya wakati wa uchaguzi ndiyo huwa kitanzi cha wapiga kura na jamaa wanakuwa wajeuri kila wakifuatwa.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lakini moyoni mwao hawana hata chembe ya huruma wanapoona watu waliowafikisha hapo walipo wakokosa mahitaji ya msingi kama maji na huduma za matibabu wakati wao wanaishi maisha ya kifahari ambayo yametokana na wananchi hao? Sasa huo mpira wakiumia wanatibiwaje? Wamuogope Mungu!
   
 12. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  hali hii inawapa kiburi sana 'viongozi' wa aina hii na ndio chanzo cha kutokupiga hatua kimaendelo.
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu huwa kinaniudhi kama magazeti ya bongo ambavyo huwa yanaripoti kuhusu hii the so called misaada ya wabunge, na most likely ni kwa baraka zao: Mfano

  1. Makala amimina misaada Mvomero

  2. Zungu amwaga misaada Ilala

  3. Serukamba aitikisa Kigoma kwa misaada..........etc etc etc.

  Kazi ya mbunge facilitation, na tunahitaji wabunge wanaothink big!!!!!!! Hzi biashara za visima, sijui amemwaga misaada eti kwa kusaidia SACCOS sh. laki mbili, au kutembelea yatima anybody able can do it! Tunahitaji wabunge watakaofacilitate mbinu mpya za kilimo, upatikanaji wa mabwawa makubwa ya umwagiliaji, Ubununifu kwa ajira za vijana na si hawa wa kumimina na kumwaga misaada.
   
 14. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Msaada wa mipira! duh ndio maana kwetu vunjo upumbavu wa misaaada kama hiyo hatuitaki kamwe a wabunge wetu wanajua hilo.
   
 15. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu utahangaika sana kupata wabunge wenye ubunifu huo na ukibahatika basi hata asilimia 0.5 ya wabunge wote haifiki. Lakini kama ulivyosema, ukiwa na waandishi ambao wanapakatwa na wabunge matokeo yake ni haya na siku ukiona mwandishi anamkosoa mbunge basi ujue wamekorofishana kwa mambo binafsi na hasa mshiko. Aibu kubwa sana na ni changamoto kwa wamiliki wa vyombo vya habari!
   
 16. w

  watenda Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu haya ndiyo yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi hii. Wapiga kura wanaswagwa kama mifugo na wenyewe ukiwasikia wanavyojipiga kifua na kutamka "jimboni kwangu" mara mia mia utadhani ni watu wa maana sana. Hata hizo constituency development funds sijui zinafanya kazi gani!
   
 17. w

  watenda Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Au ndo maana wachagga mpira siyo zao nini?
   
 18. w

  watenda Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nataka niipige moto kadi yangu ya kupigia kura.
   
 19. T

  Tiote Senior Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uzuri ni kwamba hata miaka mitano nayo inakimbia kama feni. Tutawaona safari hii wanakuja na staili ipi. Lakini kwa kweli inakera kuona watu wanalamba miguu watu walioomba kufanya kazi ya kuleta maendeleo.
   
 20. T

  Tiote Senior Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hasira hasara mkuu.
   
Loading...