Mbunge: Adui mkubwa wa serikali sio CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge: Adui mkubwa wa serikali sio CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 26, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mbunge wa Mtera(CCM) Livingston Lusinde amesema bungeni kuwa, adui mkuwa wa serikali sio Chadema bali ni utendaji mbovu wa serikali yenyewe na kuendeleza visingizio visivyokuwa na msingi wowote, amesema mvua isiponyesha serikali inatangaza janga ikinyesha inatangaza janga bila kuwa na mipango yeyote endelevu.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,435
  Trophy Points: 280
  hahah!! @new york city.. bado una plan za hili jimbo?
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duuu st ivuga hii ni meseji kwa nani maana..
   
 4. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Sasa katika nchi ambayo asilimia 90% ya viongozi ni makada, wewe unategemea nini?

  Kiongozi wa nchi anatembelea nchi iliyoendelea badala ya kuleta technologia ya kujenga nchi yeye analeta matembezi ya mshikamano.

  Wewe unategemea nini hapo?

  Kiongozi ana kwenda tibiwa Uingereza, akirudi nchini badala ya kuagiza mitambo ya kisasa madaktari wetu waizoee na kubana mapesa ya kutibu viongozi nchi za nje, yeye anasema Ni vizuri kiongozi wa chama akaangaliwe afya mara moja kila mwaka ulaya! Watendaji wetu wanatakiwa wawe na akiri za mafundi chereheni. Wao mafundi ikitokea fasheni ya nguo tuu ulaya, utakuta wao wameisha ifanyia mazoezi na wanaweza kukutengenezea ukivaa unaonekana kama vile umenunua ulaya.

  Vyuo vya CCM kivukoni na Hombolo vimetoa watu wa kupiga polojo saaanah mitaani kuliko kujenga nchi. Nani kama marehemu Dereck Bryson?
   
 5. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa Serikali yetu ya chama chetu tawala haina jipya. Ni jambo la ajabu kabisa kwa kiongozi mwenye maona na shupavu wa uongozi kutoa sababu za eti mvua hazikunyesha.

  Kwa maoni yangu tumechoka na hii serikali isiyo na huruma na watu wake na sasa tunasubiria tamko tu sisi tuingie mtaani. Tupo tayari ni tamko ndo linasubiliwa maana tumeonewa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha na sasa imetosha tunaomba kiongozi tu wa kutuongoza tulete mabadiliko ya kweli .....
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,158
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Amesema kweli, Mvua ikinyesha balaa. Hebu fikiria maji yanvyojaa huko Posta, watu wanalia na mali kuharibika. Isiponyesha balaa tena.. kama ilivyo sasa umeme hakuna. Hivi ninyi CCM mnataka Mungu awape nini?

  Ningekuwa na uwezo ningaliwafunza hawa viongozi wenu kwa viboko...inama, pitisha mikono nyuma ya miguu, shika masikio. Mboko mbili mbili kisha unawaambia kesho nataka umeme hapa.

  Tunasumbuliwa na akili mgando tu hapa
   
 7. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lazima tuwang'oe madarakani hawa kwa gharama yoyote ile
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Kibaya zaidi ni pale mvua zinaacha kunyesha kwa miezi miwili tu ama mitatu linatangazwaa janga. Sasa tujiulize siku ikiacha kunyesha kwa miezi 6 ama
  Mwaka itakuwa je? Hii serikali ni wasanii sijapata kuona chini ya mbingu. Mara utasikia tatizo la sasa ni mtikisiko wa uchumi uliotokea huko magharibi, mara ni kupanda kwa mafuta uarabuni, mara ni wafazili wetu wako vitani afghanistan n, kadha wa kadha.
  CHAKUJIULIZA NI KWA NINI VIONGOZI WETU WAMEKUWA WAKISINGIZIA MATATIZO YOTE YA NDANI NA NJE KUTUHUSU? Sisiem imekuwepo madarakani kwa miongo zaidi ya mitatu haina mipango endelevu? Kweli hawa watu akili zao zinafanana, cha msingi ni sisi watanzania kuwapa talaka haraka iwezekanavyo.
  .
   
 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wakati wa vyuo vya CCM kulikuwa na viongozi, sio sasa. Mafanikio unayoyaona Tanzania sasa yanatokana na mawazo na msimamo thabi wa hayati mwl Nyerere, fikilia siku moja kama angenza Kiwete, akaja Mkapa, Mwinyo, Tanzania ingekuwa wapi?

   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Anna Abdallah: Hii ndiyo Serikali ya CCM ninayoifahamu?
  *Anne Kilango: Waziri Mkuu, nasema siungi mkono hoja
  *Lusinde: Mchawi wa CCM siyo CHADEMA, ni Serikali
  *Ally Keissy: Hii ni Serikali gani hii isiyowajali wananchi?

  Na Maregesi Paul, Dodoma
  [​IMG]


  HALI ya hewa juzi na jana ilichafuka bungeni baada ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa kauli zinazoonyesha jinsi wasivyoridhishwa na utendaji wa Serikali inayoongozwa na chama chao.

  Walitoa kauli hizo walipokuwa wakichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 iliyowasilishwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe.

  Dalili ya wabunge hao "kuchafua hali ya hewa" zilianzishwa na mwanasiasa mkongwe nchini ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), ambaye alisema haamini kama ukiukwaji wa taratibu za kazi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali unafanywa na watu wanaotekeleza ilani ya CCM.

  "Mimi sina kawaida ya kutounga mkono bajeti, lakini katika bajeti hii naomba iwe ni mara yangu ya kwanza kutoiunga mkono mpaka nipate majibu ya hoja zangu.

  "Mei mwaka huu Kamati ya POAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma) ilikutana na kuiita Bodi ya Korosho na kuwahoji kuhusu zao la korosho, walishindwa kujieleza. Kamati ikaagiza CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) akague hesabu zao.

  "Pamoja na hayo, mimi nawashangaa sana, zao la korosho limesahaulika, Mtwara hakuna dawa za korosho watu hawamwagilii dawa, hakuna sulpher, hakuna pembejeo halafu Serikali mnasema mnafanya kazi.

  "Nyie Serikali mnachukua pesa za korosho, mnakusanya watu wachache na kujifanya hao ndiyo wadau wa korosho na kupanga mipango ya korosho wakati sisi wajumbe wa RCC (Baraza la Ushauri la Mkoa) hatuna taarifa, sitaki, naomba wewe waziri utueleze vinginevyo hapa hapatoshi.

  "Hata bodi ya wakurugenzi haipo, mwenyekiti hakuna, hivi waziri nikuulize, huu ndiyo utawala bora huu, hivi hii ndiyo CCM yangu ninayoifahamu kweli?

  "Mimi namwamini sana Waziri Mkuu, najua nyinyi mnafanya mambo mengine bila Serikali kujua, lakini nakuomba waziri unipe majibu ya kutosha kwa nini mnatelekeza zao la korosho? Hivi haya mnayoyafanya hata katika pamba, kahawa, tumbaku na mazao mengine mnafanya hivyo?

  "Nakwambia kwa mara ya kwanza sitaunga mkono hoja, sitaunga mkono kwa masikitiko makubwa, tena nasikitika kweli kweli kuipinga Serikali yangu," alisema Anna.


  Anna Kilango – Malecela aichambua Serikali

  Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango – Malecela, yeye alitumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuichambua Serikali akinukuu toleo la mwaka 1977 sehemu ya pili ibara ya 8 (c) na 9 (i) ambayo inaeleza jinsi Serikali itakavyotumia rasilimali za nchi kuwaondolea umasikini Watanzania.

  "Bei ya mazao ili imnufaishe mkulima lazima izidi gharama za uzalishaji, inapotokea gharama zinakuwa juu kuliko bei ya kuuzia, hapo mkulima anakuwa hafaidiki kwa namna yoyote.

  "Katika mazungumzo yangu haya nitaitumia Katiba ya nchi yetu toleo la 1977, sehemu ya pili, ibara ya 8 (c) na 9 (i) ili wenyewe muone jinsi Serikali isivyowajali wakulima.

  "Katika eneo hilo la Katiba, Serikali itatakiwa kuwaodolea Watanzania umasikini, sasa kwa mtindo huu kweli mnawaondolea umasikini? Hamuwezi kuzuia chakula kisiuzwe popote wakati nyinyi hamna uwezo wa kukinunua, hii haiwezekani.

  "Katika gazeti moja linalotoka kila siku Waziri umenukuliwa ukisema nchi jirani zenye njaa zinatakiwa kuwasiliana na Serikali yetu ili ziuziwe chakula badala ya kupitia moja kwa moja kwa wakulima.

  "Sasa Mheshimiwa Waziri, nakuuliza ni lini Serikali imeanza biashara ya kuuza chakula nje? Mnawakaribisha watu wa nje waje kununua chakula, hicho chakula mmekilima nyinyi? Nasema hili nalikataa, kwa nini mnauza chakula nje halafu wananchi mnawazuia?

  "Waziri Mkuu nasema hapana, waacheni wakulima nao wanunue ma-VX, nitakuwa mtu wa ajabu kama nitasema naunga mkono jambo ambalo silipendi, siungi mkono hoja," alisema Kilango.

  Mbunge huyo alizungumzia pia Kiwanda cha Tangawizi kilichoko Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro na kuishutumu Serikali kwa kushindwa kuweka miundombinu ya maji na barabara kiwandani hapo ili wananchi weweze kunufaika na kiwanda hicho pindi kitakapoanza.

  "Mheshimiwa Waziri Mkuu, mnataka niunge mkono hoja hii? Nasema sitaki japokuwa nakushukuru kwa kunipa Sh milioni 10, kiwanda kimeanzishwa tena ni kizuri kweli kweli, Serikali mkiombwa msaada hamtaki, kwa nini mko hivyo?" Alihoji.

  Livingstone Lusinde: Adui wa CCM si Chadema, ni watendaji serikalini
  Wakati wanasiasa hao wakisema hayo, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), aliishambulia Serikali ya CCM na kusema udhaifu wa utawala unaoonekana ndani ya chama hicho hausababishwi na vyama vya upinzani kama baadhi ya watu wanavyosema.

  "Ile kauli ya kwamba ‘Kilimo ni Uti wa Mgongo' sasa hivi haipo tena, uti wa mgongo umeshavunjika na mtu mwenyewe anasubiri kuzikwa.

  "Nawaambia adui mkubwa wa CCM siyo Chadema wala nani, adui mkubwa wa CCM ni
  watendaji wa Serikali, watendaji hao ndiyo watakaotuua.

  "Bodi ya Zabibu hawataki kuiunda, lakini wako tayari kuunda Bodi ya Tumbaku wakati wanajua tumbaku inaua watu, wataalamu wanaojua walitengeneza ‘pen', walipoona imepitwa na wakati wakatengeneza ‘calculator', walipoona imepitwa na wakati wakaunda kompyuta, lakini hawa watalaamu wetu mbona hawabadiliki?

  "Tanzania ndiyo nchi pekee duniani inayomshangaza Mungu, mvua ikinyesha ni balaa, jua likiwaka ni balaa yaani kila wakati balaa tupu.

  "Hawa wataalamu wa Serikali mimi siwaelewi, juzi Rais alikwenda Malaysia akiongozana na watalaamu wengi, baadaye tukaona Rais ndiye anaomba ‘business card' za wawekezaji wakati watalaamu wetu wamekaa tu, yaani mambo ya aibu kabisa na sijui kwa nini anakwenda nao, yaani wanatia aibu.

  "Mimi nawaambia kilimo kina tija kuliko hata huo umeme wenu mnalolalamikia baada ya nyama zenu kuoza kwenye friji, kama mnadhani kilimo ni kazi rahisi, basi tuanzishe shamba la Bunge tulilime sisi halafu muone kama mtaweza kulima.

  "Hivi sisi tumelogwa na nani, kila kitu tunalalamika, nakwambia wewe waziri kuna siku tutakataa bajeti yote potelea mbali hata tukirudi kwenye uchaguzi, nawashangaa sana nyie mko tayari kupeleka maboksi ya kura kila kijiji, lakini ukifika wakati wa mbolea, mbolea inaishia wilayani.

  "Waziri sikwambii haya kwa sababu sitaunga mkono hoja, hoja nitaunga mkono, lakini mwakani kama mtakuja na mambo yenu haya, tutaikataa kabisa bajeti yako," alisema Lusinde.


  Mbunge wa Nkasi: Picha ya Rais iondolewe kwenye kitabu

  Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), aliishutumu Serikali huku akimnyooshea kidole Waziri Maghembe kutokana na uamuzi wa Serikali wa kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula nje ya nchi.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo, kilichofanywa na Serikali ni uonevu kwa wananchi kuwa baada ya hatua hiyo, mahindi yameanza kuoza mkoani Rukwa kwa kuwa hakuna soko na Serikali haina uwezo wa kuyanunua.

  "Kwanza nakwambia siungi mkono hoja, halafu wewe waziri nakuomba uondoe picha hii ya Rais wetu katika kitabu chako hiki cha bajeti ambapo Rais Kikwete ameshika power tiller ambazo sisi Rukwa hatuzitaki kwa sababu hazifai.

  "Wewe waziri unafunga mipaka ili watu wasisafirishe chakula nje wakati Serikali haina uwezo wa kukinunua, sasa umefunga mipaka na sisi Rukwa mahindi yameanza kuoza, nakwambia hatutaki sheria zenu hizo tafadhali fungua mpaka haraka watu waanze kuuza nje.


  Hiki si ‘Kilimo Kwanza', ni ‘Kilimo Mwisho'

  "Wananchi wameshaanza kutwambia watatupiga mawe kwa sababu umewazuia kuuza mahindi nje wakati nyie hamna uwezo wa kuyanunua, nakwambia hatutaki kupigwa mawe na lazima uyanunue mahindi yote na kama utashindwa lazima uwafidie wananchi kwa sababu baada ya agizo lako wanaishi maisha ya shida kwa sababu yako.

  "Hii Serikali gani hii? Mnazuia watu wasiuze nje wakati mnasema kasi mpya, hii kasi gani hii, mnatwambia Kilimo Kwanza -hiki siyo kilimo kwanza- hiki ni Kilimo Mwisho.

  "Wewe Profesa unafunga barabara hadi Januari wakati unajua Januari barabara kule kwetu hazipitiki, nakuuliza hizo barabara utazitengeneza wewe ili sisi tupite, nakuuliza utazitengeneza wewe, sitaki kabisa mambo yenu, asante Mwenyekiti," alisema Kessy na kupigiwa makofi.

  Katika hatua nyingine, mbunge huyo alitaka kujua ni kampuni gani inayoingiza matrekta madogo nchini kwa vile kuna kla dalili kwamba huo ni mradi wa wakubwa ambao wanajinufaisha nao na kuwaumiza wananchi.


  Chakula kinazuiwa kwa sababu hakuna uchaguzi

  Mbunge wa Nkasi Kusini, Deusderius Mipata (CCM), kama walivyosema wenzake, naye aliishutumu Serikali kwa kuzuia chakula kisiuzwe nje ya nchi na kusema uamuzi huo umefikiwa kwa sababu hakuna uchaguzi wowote wa kisiasa.

  "Hivi nyinyi mnatuzia tusiuze chakula kwa sababu gani, hivi kama kungekuwa na uchaguzi mngeyafanya haya? Mijini wakati wa Uchaguzi Mkuu waliwakataa mkakimbilia vijijini kwa wakulima wakawakubali, lakini leo mnawageuka, hatukubali.

  "Tunataka hiyo mipaka ifunguliwe turuhusiwe kuuza chakula nje ya nchi kwa sababu jukumu la kuilisha nchi siyo la wakulima, bali hilo ni jukumu la Serikali, nawaambia hatutaki tabia hiyo," alisema Mipata.

  Baada ya wabunge hao kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa Serikali, jana mchana wabunge wa CCM walikutaka katika Ukumbi wa Msekwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuwekana sawa kabla mjadala wa bajeti hiyo haujahitimishwa jana jioni.
  …mwisho.


   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni kweli, Mbaya wa CCM ni Serikali yake. Walafi na wavunja Sheria ni Serikali ya CCM; Kama Chama Cha Mafisadi kilijivua Magamba Serikali yake lazima izaliwe upya, wabaya wa nchi wako ndani ya hiyo Serikali from Wazee to Vijana...

  That's the real change needed - Tutapata Umeme na Madini yetu yote!!!
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni kweli msigano wa wao kwa wao ndiyo unaokiua chama chao!!
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,834
  Likes Received: 2,306
  Trophy Points: 280
  anayeunda serikali ni nani? ni CCM yenyewe chini ya Mwenyekiti wao, sasa sisi tunajua kwamba Chama legelege huunda serikali degedege. kwa hiyo anna makinda umekosea, kilaumu chama chako cha Mapinduzi kwa kushindwa kuisimamia serikali ili iwatetee wananchi wake wanyonge hasa hao wakulima na sisi wafanyakazi tunaoishi kwa matumaini.

  Hili ulilosema Anna nalo ni GAMBA tena hili ni kubwa kuliko yale magamba ya mapacha watatu.
   
 14. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wote wasanii hao, wanawapiga changa la macho watanzania!
   
 15. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mwendo huu wa Moto huu ukiendelea ukawashwa mpaka Serikalini basi kidogo Nchi itaanza kuwa na mwanga.Na kwa Serikalini na Makampuni ya UMMA Wafanyakazi waanze kuweka Madudu ya viongozi wao au watendaji wanaohujumu Serikali kwenye magazeti na taarifa hizo zianze kujadiliwa na umma kwenye forum kama hivi na kisha kuingizwa kwenye vyombo vya habari kama Magazeti na Televisioni ili jamii ijue madhambi ya wakuu hao.
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Wacha wenyewe kwa wenyewe watafunane.
   
 17. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Lusinde, yoote uliyoongea sawa, lakini hapa............"Waziri sikwambii haya kwa sababu sitaunga mkono hoja, hoja nitaunga mkono, lakini mwakani kama mtakuja na mambo yenu haya, tutaikataa kabisa bajeti yako," alisema Lusinde.

  Sijui umelalamika kwa sababu......... Makelel yoooteee yale mwisho wa siku unaunga mkono hojaaaaaaaaa.......... AMA KWELI NYOKA NI NYOKA HATA AVUE NGOZI ACHILIA MBALI GAMBA
   
Loading...