Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,001
- 9,866
Mamilioni hayo ya shilingi yanadaiwa kuwa mali ya Mbunge wa Viti Maalum, Jackline Ngonyani (CCM).
Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Songea, Shabani Mwigole, jana alidai mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Kussaga Majinge kuwa kati ya Novemba 27, 2015 na Desemba 31, 2019, katika Benki ya CRDB Tawi la Songea, mshtakiwa, aliiba Sh. milioni 440, mali ya Jackline Ngonyani kinyume cha sheria.
Mwigole alidai kuwa mshtakiwa aliiba fedha alizopatiwa na mbunge huyo kwa lengo la kuzihifadhi kwenye yake ya benki, akifafanua kuwa badala ya kuzihifadhi, mfanyabiashara huyo anadaiwa kuzitumia kwa mambo yake binafsi, kinyume cha makubaliano yao.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka hilo na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Januari 17, mwaka huu.
Hakimu Mkazi Majige alisema dhamana ya mshtakiwa iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini watatu, wenye mali zisizohamishika zikiwa na thamani ya Sh. milioni 133 kila mmoja.
Chanzo: Nipashe