Mbunge Abood atoa Ambulance na kugawa maelfu ya Barakoa mji mzima ili kuwakinga Wananchi na Corona

Kiukweli huyu Mbunge amekuwa akijitoa sana kwa Wananchi na hanaga maneno wala show off.

Hizi hapa chini ni baadhi tu ya picha zinazoonyesha akitoa msaada na hakutaka hata kuziandika jina lake, gari la kubebea wagonjwa, ndoo za maji na sanitizers mji mzima.
View attachment 1430608
View attachment 1430614
Hawa ndio wanasiasa wanaopaswa kupewa heshima kwa sababu hawafanyi mambo kwa KIKI.
Mungu ambariki sana!.
P
 
sisi wengine mbona tupo mjini tena town centre kabisa lakin hatujanufaika na huo msaada? sasa ukisema mje mzima amezigawa wapi na wapi? sababu sisi ni wafanya biashara islam sehem maarufu sana morogoro mjin lakin huo msaada hatujauona sasa ukisema mji mzima utakakuwa unakosea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mara chache sana najitokeza kutetea wanasiasa, ila uongo ukiachwa utamalaki huaminika kirahisi.

Nimecheka sana nilivyoona kwenye thread ya Mbunge Devota Minja akitoa msaada wa barakoa kwamba eti mzee Mohamed Abood hasaidii wananchi wa Morogoro zaidi ya kutoa magari ya kubebea maiti kupeleka makaburini kuzika.

Kiukweli huyu Mbunge amedumu Morogoro kwa sababu amekuwa akijitoa sana kwa Wananchi. Sio mchoyo na hanaga maneno wala show off. Ndio maana wengine tukiona kashfa za ajabu kama hizi tunajisikia vibaya. Pia Morogoro nzima pale ukienda kuongea kashfa kama hizi wanakushangaa tu.

Hizi hapa chini ni baadhi tu ya picha zinazoonyesha akitoa msaada wa barakoa bora sio kama zile za kushona na hakutaka hata kuziandika jina lake, gari la kubebea wagonjwa, ndoo za maji na sanitizers mji mzima.


View attachment 1430607View attachment 1430608View attachment 1430610
View attachment 1430614

Hawa ndio wanasiasa wanaopaswa kupewa heshima kwa sababu hawafanyi mambo kwa KIKI.
Sidhani hata kama unajua maana na chimbuko la neno ''kiki'' hasa unaposema hafanyi mambo kwa kiki. Mbona mimi naona hapo kila kitu kimefanyika kwa sababu ya ''kiki''?
 
Safi sana... Inapendeza sana...

Zingepitia sehemu fulani kwanza, tusingezisikia wala kuziona... tungetajiwa figure tu...



Cc: mahondaw
 
Wakitoa bila kuvibandika majina yao wanahisi mchango wao hautaonekana?!
Mara nyingi vitu vya msaada hubandikwa majina ili kuepusha wanaopewa kuvisambaza bure, wasije kutumia fursa na kuviuza au kutumika nje ya malengo kusudiwa.
 
Wakitoa bila kuvibandika majina yao wanahisi mchango wao hautaonekana?!
Mara nyingi vitu vya msaada hubandikwa majina ili kuepusha wanaopewa kuvisambaza bure kutumia fursa na kuviuza au kutumika nje ya malengo kusudiwa.
 
Back
Top Bottom