Mbunge aamua kuwalipia walimu kodi za nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge aamua kuwalipia walimu kodi za nyumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, May 3, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii inaonyesha jinsi wabunge wanavyolipwa pesa nyingi zaidi ya mahitaji yao. Serikali inatakiwa iwape waalimu mishahara inayotosha kukidhi huduma zao muhimu, na sio kupewa misaada na watu wanaotafuta kujiendeleza.

  Mbunge aamua kuwalipia walimu kodi za nyumba

  Na Thobias Mwanakatwe
  3rd May 2010

  Katika hatua inayotafsiriwa kuwa ni kampeni za mapema kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, Mbunge wa Songwe wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, Dk. Guido Sigonda, ameahidi kuwalipia kodi za nyumba walimu wa shule za sekondari na msingi wa Kata ya Galula wilayani hapa.

  Mbunge huyo aliahidi kuchukua hatua hiyo kutokana na kata hiyo kutokuwa na nyumba za kuishi watumishi.

  Dk. Sigonda alitoa ahadi hiyo juzi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi ambayo ngazi ya kata yalifanyika katika Kijiji cha Magamba. Mbunge huyo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

  Uamuzi wa mbunge huyo kutangaza kuwalipia kodi ya pango la nyumba walimu wa kata hiyo, ulifuatia maelezo yaliyotolewa na walimu hao kuwa wanaishi katika nyumba za kupanga kwa muda mrefu hali inayowapa usumbufu kutokana na serikali kutowajengea nyumba za kuishi.

  Walimu hao walimweleza Sigonda kwamba wanaishi katika maisha magumu kutokana na kiwango kidogo cha mishahara wanachokipata kutumia kiasi fulani kulipia kodi za pango la nyumba.

  Walimweleza kuwa hali hiyo ni miongoni mwa mambo ambayo yanachangia kuzorota kwa kiwango cha elimu katika Jimbo la Songwe.

  Dk. Sigonda alisema wakati serikali kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji husika, inafanya mipango ya kujenga nyumba za kuishi kwa ajili ya walimu, yeye atawalipia kodi ya nyumba kila mwezi hadi hapo zitakapojengwa na kuwaagiza viongozi wa kata kumpelekea idadi ya walimu wanaoishi kwenye nyumba za kupanga.

  “Tatizo la nyumba za kuishi watumishi ni la nchi nzima, hata hivyo, mimi kama mbunge wenu, natangaza kuanzia sasa kwamba nitaanza kuwalipia kodi ya nyumba hadi hapo serikali itakapowajengea nyumba za kuishi,” alisema Dk. Sigonda.

  Baadhi ya wananchi waliohudhuria waliichukulia ahadi hiyo kuwa huenda ni kampeni za uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa kukosekana kwa nyumba za walimu ni tatizo la muda mrefu.


  Mmoja wa wakazi wa kata hiyo ambaye hakutaka kutajwa, alihoji inakuwaje mbunge huyo awaonee huruma walimu hao kwa kuwalipia kodi za nyumba wakati hakufanya hivyo miaka mitano iliyopita.
  Dk. Sigonda alitoa ahadi hiyo huku baadhi ya wananchi nchini wakiwalalamikia wanasiasa, wakiwemo wabunge wanaotoa misaada katika maeneo yao hivi sasa wakati uchaguzi mkuu ukikaribia.

  Wananchi hao wanasema inakuwaje wanasiasa hao hawakutoa misaada hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne tangu waliposhika nafasi hizo.

  Katika maeneo mengi nchini, ukiwemo Mkoa wa Mbeya, wanasiasa hususan wabunge, wamekuwa wakitoa misaada ya fedha taslim, vyombo vya usafiri kama pikipiki na misaada mingine kwa wapigakura wao wakidai kuwa wanatimiza ahadi walizozitoa kwao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

  Jana mchana, Nipashe ilipowasiliana na Dk. Sigonda ili kutoa ufafanuzi wa ahadi yake kwa walimu na kampeni za uchaguzi, alisema kuwa alikuwa kwenye kikao.

  Hata hivyo, alipotafutwa baadaye, mara zote simu yake ya kiganjani ilikuwa imefungwa.
  Katika hatua nyingine, Dk. Sigonda alisema serikali imekubali kuwalipa wakulima fedha za pamba na kwamba zimeshapelekwa wilayani na utaratibu wa kulipa unaandaliwa.

  Alisema madeni hayo yatakayolipwa ni yale ambayo yamelimbikizwa toka mwaka 1995 hadi 1996 na kuwataka wakulima ambao majina yao hayatajitokeza katika malipo hayo wawasilishe nyaraka ili walipwe.

  Mbunge huyo pia alitoa Sh. 400,000 kwa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Watumishi wa Kata ya Galula ili kusaidia kutunisha mfuko wa chama kiweze kuwakopesha wanachama wake.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huku ndiko kukumbuka shuka 'usubuhi'..lol
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ina maana mbunge mmoja analipwa extras za kutosha kulipa walimu kodi za nyumba?sasa why wasipunguziwe hilo fungu na wakapewa walimu?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bora...nyie waalimu kaeni kwa amani kwenye hizo nyumba, na kama inawezekana mumwombe na baiskeli za kufuatia mishahara mjini...Hakuna namna ingine ya kufaudu hela ya sirikali zaidi ya hiyo...Kuleni wala msijishaue!...Hazina mwenyewe hizo fedha!
   
 5. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mmoja wa wakazi wa kata hiyo ambaye hakutaka kutajwa, alihoji inakuwaje mbunge huyo awaonee huruma walimu hao kwa kuwalipia kodi za nyumba wakati hakufanya hivyo miaka mitano iliyopita.

  Words are enough for the wise! need we say more?
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo JK uko wapi na sheria yako ya gharama za uchaguzi..Kampeni ndio zishaanza hivyo.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ama kweli sasa tunapoteza kabisa maana ya MBUNGE.. Takrima at the best, na kinachofuata ni kutawaliwa na kina Rostam, Manji na matajiri wote watakaogombea Ubunge, maanake Ubunge sasa unatokana na uwezo wa mfuko wa mgombea.
  Hivi kweli huyu mbunge anaweza bado kuwalipia hao walimu kodi za nyumba hata kama asiposhinda uchaguzi huu wa mwaka 2010?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu Mh naona anawauzia deni hao waalimu! malipo Oct 2010! kwenye kibox cha kupigia kura
   
 9. Bright

  Bright Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wamsanishe mkataba wa miaka mitano: 2010 - 2014 ili pesa za maendeleo ya majimbo zitumike muda wote.
   
 10. Bright

  Bright Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakisha msainisha mkataba wa miaka mitano kulipia kodi na wenye nyumba, hakikosa ubungo ndio ataona tamu ya siasa chafu.
   
Loading...