Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Freeman Mbowe na Lema walipotinga kituo cha polisi
Msimamo wa Mbowe - Tume huru ya kimahakama si polisi watuhumiwa
Kuhusu ushahidi anaodai unawahusisha polisi na tukio la bomu, Mbowe alisisitiza kuwa Chadema kina ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo lakini alisema hakitaukabidhi mikononi mwa polisi.
Alisema hakitafanya hivyo kwa kuwa jeshi hilo ni watuhumiwa wakuu hivyo hawawezi kuwa na dhamira na nia njema katika upelelezi wao. Alisema ndiyo maana badala polisi kuwaona ni msaada, kimeanza kutoa vitisho kwa wote wanaosema waliwashuhudia askari wakishambulia watu kwa risasi kabla ya kuondoka na aliyerusha bomu kwenye gari lao.
Chadema tuko tayari kukabidhi ushahidi huu kwa tume huru ya uchunguzi ya Mahakama. Rais Kikwete atumie mamlaka yake ya kikatiba kuunda tume kuchunguza tukio la bomu Arusha ili ukweli ujulikane. Polisi ni watuhumiwa katika jambo hili, hivyo hawana dhamira safi na ushahidi wetu, alisema Mbowe.
Busara Lema na Mbowe kufika kituo cha polisi kuitika mwito
Lema, Mbowe wahujiwa kituo cha polisi kutokana na mkusanyiko wa kuaga miili ya marehemu iliyosababishwa na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha vifo pamoja na zile zilizofuatia wakati polisi ilipowasambaratisha wafuasi wa chama hicho kwa mabomu walipokusanyika kwenye Viwanja vya Soweto kwa lengo la kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Wakiongozwa na mawakili watatu, Mbowe na Lema waliwasili polisi saa 3.50 asubuhi na kuhojiwa hadi saa 9.10.Viongozi hao walipokewa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Diwani Nyanda kabla ya kutenganishwa kwenye vyumba viwili tofauti kwa mahojiano.
Polisi waliwahoja mambo mawili:
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbowe, Lema na wakili Albert Msando walitaja mambo mawili ambayo polisi waliwahoji kwanza ikiwa ni:
- Ushiriki wao katika mkusanyiko usio halali kwenye Viwanja vya Soweto, Jumanne iliyopita ambao ulisambaratishwa na polisi.
- Kauli yao ya kuwa na ushahidi unaohusisha polisi na tukio la bomu lililorushwa kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha vifo vya watu wanne huku zaidi ya 60 wakijeruhiwa.
Hoja za utetezi Lema na Mbowe dhidi ya shutuma za polisi
Mbowe - Polisi ilituruhusu kuzungumza na wananchi
Mbowe alisema kwa pamoja wamewaeleza polisi kuwa hawaamini kama mkusanyiko wa Jumanne iliyopita haukuwa halali kwa sababu waliruhusiwa kuzungumza na wananchi waliokusanyika ili kuwashawishi watawanyike.
Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) wa Arusha, Gilles Mroto ndiye aliyeturuhusu kuzungumza na wananchi wale kuwataka watawanyike na ndicho tulichofanya, lakini tukashangaa kuanza kupigwa mabomu mara baada ya kuwataka watu wanaotaka kutoa heshima za mwisho kwa marehemu kwenda Hospitali ya Mount Meru, alisema Mbowe.
Alisema Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja kuwa naye aliyewaomba viongozi wa Chadema kuwatawanya wafuasi wa chama hicho baada ya kuzuiwa kutoa heshima za mwisho katika viwanja hivyo vinavyomilikiwa na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Police waanza kuchanganyikiwa na kutaka ushauri wa kisheria baada ya kuzidiwa hoja ya Mbowe
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi inawasiliana na wanasheria kutafuta ushauri wa hatua za kuchukua... Polisi ndiyo wenye jukumu la kuchunguza na kukusanya ushahidi wote kuhusiana na matukio ya uhalifu. Hili ni jukumu la kisheria la polisi. Chadema wakabidhi ushahidi wao badala ya kupiga danadana ya kutaka tume huru ya uchunguzi ya kimahakama.
Alisema hata ikiundwa tume, bado jukumu la kuchunguza na kukusanya ushahidi litarejeshwa mikononi mwa polisi, hivyo Chadema wanapaswa kutimiza wajibu wa kusaidia uchunguzi kwa kuwasilisha ushahidi wao wa polisi kuhusika katika tukio la bomu.