Mbowe: Uchaguzi huu hatutaibiwa kura!

Mbowe: Uchaguzi huu hatutaibiwa kura!

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
18,925
Reaction score
13,280

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kimejipanga kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu hawaibiwi kura.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akizindua mafunzo ya Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha chama hicho (Red Brigade), kwa vijana 200 wa Kanda ya Kati pamoja na Kikosi maalum cha Karate.

“Katika uchaguzi huu hatutaki kulalamika tena kwamba tumeibiwa kura na tutahakikisha tutaomba kura kwa wananchi na tutazilinda,” alisema Mbowe.

Alisema endapo watakubali kuibiwa kura maana yake hawapo tayari kuongoza. Mbowe aliwataka vijana hao wa Brigade kutokukilinda

chama peke yake bali pia kiwe chachu ya ulinzi kwa jamii inayowazunguka kwenye maeneo yao.

Alibainisha kuwa Chadema kitaendelea kutoa mafunzo ya ulinzi kwa vijana nchi nzima. "Vijana hawa lazima wajenge moyo wa kujitolea, chama kilijengwa na watu wenye moyo huo ambao baadhi walipata madhara mbalimbali ikiwamo kupoteza maisha,” alisema Mbowe.

Alisema wajenge sifa ya kuwa wakombozi wa Taifa na malipo mengine siyo lazima walipwe hapa duniani bali watapata kwa Mungu
CHANZO: NIPASHE.

=======================================================================

Mbowe amekuwa akiwaaambia wafuasi wa CHADEMA kila uchaguzi ukaribiapo kuwa hakuna kura zitakazoibiwa, lakini uchaguzi unapopita tu, na CHADEMA kushindwa kwa kishindo, Wimbo wa kuibiwa kura unaanza tena.

Mbowe sasa uwahakikishie wafuasi wako kwa dhati kabisa kuwa mwaka huu hatutasikia ngonjera za kuibiwa kura baada ya uchaguzi.
 
Kiongozi ambae anawaza kwa kutumia miguu ni Freeman Mbowe,amekua kila mara akisema kura hazita ibiwa lakini baada ya matokeo ana mtuma Dr Slaa aseme kura zili ibiwa
 
CCM nanyi toeni tamko kuwa hamtaiba kura za wapinzani...
 
Ingawa natambua kwamba matumizi ya vikundi kufanya ulinzi sio mazuri, nakubali kwamba juhudi za kimakusudi zinahitajika kulinda kura. Uzoefu umeonyesha ukomavu wa tabia ya wizi wa kura unaofanywa na chama tawala. Nashauri juhudi za kuondoa wizi wa kura zisiishie kwa kuunda vikundi tu bali udhibiti wa mfumo mzima wa uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na zoezi la kuhesabu kura
 
Kiongozi ambae anawaza kwa kutumia miguu ni Freeman Mbowe,amekua kila mara akisema kura hazita ibiwa lakini baada ya matokeo ana mtuma Dr Slaa aseme kura zili ibiwa

Mkuu makamanda mwaka huu hawatoki, kila mara wanajidai wanaibiwa kura, lakini sasa wameshajifunga wenyewe kuwa kura hazitoibiwa tena, kwahiyo Single ya kuibiwa kura ndio imefia hapa, tunasubiri waje na kisingizio kingine cha kushindwa!
 
CCM nanyi toeni tamko kuwa hamtaiba kura za wapinzani...

Kamanda, nadhani umesahau kuwa CHADEMA kupitia Red Brigade huwa wanakesha nje ya vituo vya kuhesabia kura mpaka matokeo yatangazwe, na huko ndani kwenye uhesabuji CHADEMA wana mawakala wao!..

Kama kura zinaibiwa na majini, sawa, ila kwa namna ya kibinadamu hakuna kura ya CHADEMA iliyowahi kuibiwa!
 
mpango wa ukawa kusimamisha mgombea mmoja umegoma?? kweli hawa ni wasaka tonge
 
Mkuu si CDM pekee wanaolalamika kuibiwa kura bali imetokea kwa CUF na hata NCCR Mageuzi kipindi kile cha Lyatonga...

Halafu uzoefu unaonesha kuwa majimbo yote ambayo wapinzani huwa wakali na wizi wa kura huwa wanafanikiwa...

Kamanda, nadhani umesahau kuwa CHADEMA kupitia Red Brigade huwa wanakesha nje ya vituo vya kuhesabia kura mpaka matokeo yatangazwe, na huko ndani kwenye uhesabuji CHADEMA wana mawakala wao!..

Kama kura zinaibiwa na majini, sawa, ila kwa namna ya kibinadamu hakuna kura ya CHADEMA iliyowahi kuibiwa!
 
Mkuu makamanda mwaka huu hawatoki, kila mara wanajidai wanaibiwa kura, lakini sasa wameshajifunga wenyewe kuwa kura hazitoibiwa tena, kwahiyo Single ya kuibiwa kura ndio imefia hapa, tunasubiri waje na kisingizio kingine cha kushindwa!

Wewe jichekeshe tuu, style itakayo tumika ni kama ile uliyoiona kutumika leo kule Monduli ya kumtoa mtu kwa nguvu ambaye hakuchaguliwa na kumweka aliyechaguliwa kwenye kiti huku Polisi wakishuhudia. Au kama yale ya Migombani Segerea na kwingineko kama kile kipigo cha pale Land Mark hotel ambako mwenyekiti wa kuchonga alipokuja kuapishwa aliishia kujificha kama Gadaffi kwenye Kalavati na kurudi kwake kavaa shati vipande vipande.
Kama mmeamua kuwa hamtoki bali kwa mabavu basi mtaona itakavyo kuwa.
 
kikosi cha karate! jamani basi wangefanya siri kuna wengine watahofia kupiga kura
 
Mkuu si CDM pekee wanaolalamika kuibiwa kura bali imetokea kwa CUF na hata NCCR Mageuzi kipindi kile cha Lyatonga...

Halafu uzoefu unaonesha kuwa majimbo yote ambayo wapinzani huwa wakali na wizi wa kura huwa wanafanikiwa...
Umeshasema ni wapinzani, hakuna aliyewahi kuja na ushahidi unaojitosheleza kuwa kura ziliibiwa, wengi wao ni porojo tu baada ya kukataliwa na wananchi.

Mbaazi zikikosa maua, husingizia jua...
 
Wewe jichekeshe tuu, style itakayo tumika ni kama ile uliyoiona kutumika leo kule Monduli ya kumtoa mtu kwa nguvu ambaye hakuchaguliwa na kumweka aliyechaguliwa kwenye kiti huku Polisi wakishuhudia. Au kama yale ya Migombani Segerea na kwingineko kama kile kipigo cha pale Land Mark hotel ambako mwenyekiti wa kuchonga alipokuja kuapishwa aliishia kujificha kama Gadaffi kwenye Kalavati na kurudi kwake kavaa shati vipande vipande.
Kama mmeamua kuwa hamtoki bali kwa mabavu basi mtaona itakavyo kuwa.

Tusubiri tuone! Ila Porojo ya kuibiwa kura isisikike mwaka huu, sijui mtawaambia nini MAKAMANDA baada ya chama kushindwa kwa kishindo!
 
Unaanzisha Uzi lakini unajaza comments zako mwenyewe mwanzo mwisho. Lakini pia niseme kitu kwa CCM; Kuiba kura kila uchaguzi umeshakuwa mtindo na style yenu hapa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa basi tuwaombe tu mjitahidi kutoiba kula na badala yake enezeni sera zenu za ufisadi na ulanguzi wa mali za umma na matumizi mabaya ya ofisi tuone kma mtapata hata nusu ya kura za UKAWA kwenye nafasi ya Urais.
 
CCM hawawezi kushinda uchaguzi wowote hadi waibe kura, waweke Pingamizi ili wapite bila ya kupingwa ama kuwapandikiza mamluki wao... Uchakachuaji wa CCM umeendelea hadi pale wanaposhindwa hadharani hukimbilia kuwaapisha MAJIZI wenzao...

Mhe Mbowe ameongea Jambo la maana sana ... This time CCM ndo watalalamika kuibiwa kura....

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kimejipanga kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu hawaibiwi kura.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akizindua mafunzo ya Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha chama hicho (Red Brigade), kwa vijana 200 wa Kanda ya Kati pamoja na Kikosi maalum cha Karate.

“Katika uchaguzi huu hatutaki kulalamika tena kwamba tumeibiwa kura na tutahakikisha tutaomba kura kwa wananchi na tutazilinda,” alisema Mbowe.

Alisema endapo watakubali kuibiwa kura maana yake hawapo tayari kuongoza. Mbowe aliwataka vijana hao wa Brigade kutokukilinda

chama peke yake bali pia kiwe chachu ya ulinzi kwa jamii inayowazunguka kwenye maeneo yao.

Alibainisha kuwa Chadema kitaendelea kutoa mafunzo ya ulinzi kwa vijana nchi nzima. "Vijana hawa lazima wajenge moyo wa kujitolea, chama kilijengwa na watu wenye moyo huo ambao baadhi walipata madhara mbalimbali ikiwamo kupoteza maisha,” alisema Mbowe.

Alisema wajenge sifa ya kuwa wakombozi wa Taifa na malipo mengine siyo lazima walipwe hapa duniani bali watapata kwa Mungu
CHANZO: NIPASHE.

=======================================================================

Mbowe amekuwa akiwaaambia wafuasi wa CHADEMA kila uchaguzi ukaribiapo kuwa hakuna kura zitakazoibiwa, lakini uchaguzi unapopita tu, na CHADEMA kushindwa kwa kishindo, Wimbo wa kuibiwa kura unaanza tena.

Mbowe sasa uwahakikishie wafuasi wako kwa dhati kabisa kuwa mwaka huu hatutasikia ngonjera za kuibiwa kura baada ya uchaguzi.
 
Ntamshangaa sana mtanzania atakayeipigia kura ccm kwenye uchaguzi mkuu ujao
 
kazi imeanza. Kule Arusha wananchi wameukataa uongozi wa CCM amabao ulipatikana kwa wizi wa kura.
 
Back
Top Bottom