Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,695
- 1,692
Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA amesema, Chama chake kiko tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni vyenye nia ya dhati ya kufanya hivyo.
Amesema, kwa maana hiyo CHADEMA imeacha milango wazi katika ushirikiano wa kumpata mgombea Uspika toka kambi ya Upinzani na pia kupata Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Kamanda Mbowe amesema, CHADEMA imedhamiria kutumia nafasi yake Bungeni kama official opposition party kuiwajibisha serikali kwa nguvu zaidi hasa katika suala zima la matumizi mabovu ya pesa na kuleta maendeleo. Amesema, kazi iliyofanywa na wabunge wa CHADEMA katika Bunge lililopita itaendelezwa kwa nguvu zote katika Bunge la sasa.
Kamanda Mbowe aliyasema hayo katika mahojiano na Elisha Elia mtangazaji wa TBC1 muda mfupi kabla ya yeye na Wabunge wengine wa CHADEMA kuelekea Dodoma tayari kwa shughuli zitakazoanza kesho.
Mbowe mesema Kamati kuu ya CHADEMA itakutana Dodoma na kujadili masuala muhimu kuhusiana na Bunge hili likiwepo suala la uteuzi wa Mgombea USpika na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.
Baada ya mahojiano hayo Mh. Mbowe, Dr. Slaa na Wabunge wa CHADEMA waliongozana kwa magari kuelekea Dodoma huku Bendera za CHADEMA zikionekana zinapepea.
Mpiganaji Mkuu na Kamanda wa Majeshi ya Ardhini Dr. Wilbrod Slaa alionekana akiongea na Mzee wa Siku Mteule Ndesamburo huku wote wakionekana wenye afya njema na huku sura ya Dr. Slaa ikiwa na tabasamu lenye haiba.
Source: TBC1 News Bulletin ya Saa 2.00 Usiku.
Naomba kuwakilisha.