Kweli tuombe Mungu atupe uzima. Mi nina hakika CUF watabeba kwa msaada wa mume wao.Ni vizuri kujua nia ma dhumuni ya chama chochote cha siasa Duniyani ni kutaka kuchukua au kuongoza Doula. Hivyo Mbowe ana haki zote kutamka hivyo kwani ndio dhumuni lao la kuunda chama chao.
lakin uhalisia inabidi ajipime je itawezekana?
Tombe mola tuone 2015.
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?
Suala la mtu mmoja kuwa na vyeo vingi ndilo suala ambalo watanzania tumekuwa tukilipigia kelele siku zote.Sasa kama CHADEMA (Chama mbadala ) nacho kinajipamba kwa sifa hii hii kuna ubadala gani hapo? Kama chadema mnadhani ninyi ni chama mbadala kweli; basi onesheni ubadala kweli!Absolutely. Kama binadamu tulivyo, It is the unknown we fear when we look upon betrayal and party conflict.
Kwenye thread ya Mh. Mnyika aligusia hii kitu pale aliposema aliuomba mpaka uongozi kumpunguzia majukumu ya chama ili ajishughulishe na mambo mengine lakini uongozi ulikataa na kumuomba aendelee.
By consolidating the power kwa wachache, inaondoa hata maana/dhana nzima ya party decentralisation kwa sababu viongozi wa majimbo wanakuwa ni walewale wenye majukumu mengine ya chama kitaifa.
Kwahiyo wakati wa vetting kujuana inakuwa ni kigezo cha ngapi?Kipi kinaanza kati ya qualifications vs kujuana?
Wewe unachofanya humu mtandaoni ni kitu gani tofauti na hao unaowasema wanalalamika na kupiga majungu?Practice what you preach.Wakati mwingine watu msiishie tu kulalamika na kupiga majungu mitandaoni.
Mtu hajaonesha jitihada zozote za kukipigania chama, naye anataka apewe madaraka from nowhere.
Ndo yale yale ya akina Shonzi et al.
Mkuu unaposema mmoja wao kiutendaji unamaanisha kitu gani?Ukishasema "mmojawao kiutendaji",ina maana tayari wako kwenye system,mimi nazungumzia kabla hawajaingia kwenye system.Je kigezo cha kwanza hapo ni kipi?Merits ama kujuana?Mkuu,
Ninaposema kujuana haimaanishi kama ni rafiki wa kunywa naye chai bali ni mmoja katika wao kiutendaji. Nimebainisha kuwa uwezo wa utendaji unakuwa wa kwanza katika vetting na kinachofautia ndicho hiki tunachokisema kujuana.
Kama ni hivyo basi Chadema ikubali it cannot change the status quo. Maana movement yao nzima ni ya "anti establishment". Sasa kama on one hand utafanya yale yale unayo dai mwenzio kafanya na yanaiponza nchi on the other hand na wewe unayafanya meaning wewe ukija kuwa na nafasi ya mwenzio tutegemee yale yale.
Suala la mtu mmoja kuwa na vyeo vingi ndilo suala ambalo watanzania tumekuwa tukilipigia kelele siku zote.Sasa kama CHADEMA (Chama mbadala ) nacho kinajipamba kwa sifa hii hii kuna ubadala gani hapo? Kama chadema mnadhani ninyi ni chama mbadala kweli; basi onesheni ubadala kweli!
Very interesting topic. Let me add my two cents into the discussion.
".................... Mwaka 2010 kuna wanaJF wengi walio kuwa wakii support Chadema (at least humu ndani, sijui mchango wao kiuhalisia) ambao walikua wana apa humu kwamba lazima Chadema itashinda 2010. Sisi ambao hatukua emotional about it tukasema its a premature declaration tuka tukanwa na kuitwa "mamluki", "mafisadi", nk. Matokeo yake Chadema ikashindwa 2010 na kwa sababu walisha jiaminisha kwamba ushindi ulikua must badala ya kujichunguza baada ya uchaguzi what went wrong kimbilio ikawa kwamba kulikua na uchakachuaje nk..............................."
Mkuu unaposema mmoja wao kiutendaji unamaanisha kitu gani?Ukishasema "mmojawao kiutendaji",ina maana tayari wako kwenye system,mimi nazungumzia kabla hawajaingia kwenye system.Je kigezo cha kwanza hapo ni kipi?Merits ama kujuana?
Decentralization ambayo bado kila kitu kinaamuliwa na Ofisi ya Katibu mkuu kwa mujibu wa maamuzi yao ya Baraza Kuu, haitabadili mambo ndani ya CHADEMA. Kanda zitapendekeza majina halafu ni Ofisi ya Katibu Mkuu itakayoteua nani wawe watendaji wa kanda hizo. sijui kama hii ni decentralization ya aina gani?
Sidhani kama watu wa "Makao Makuu" wako tayari kuachia mambo yafanywe na watu wa kanda bila wao watu wa Makao Makuu kutia mikono yao!!
Na George
Ramadhan|21st February 2013
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema sera mpya ya
majimbo itakiwezesha chama hicho kushika dola na kuongoza nchi kwa
urahisi zaidi.
Akifungua kikao cha kazi za Chadema kilichofanyika jijini hapa jana,
Mbowe alisema sera ya majimbo ni mkakati uliobuniwa na chama hicho kwa
lengo la kusogeza madaraka kwa wananchi ili kushiriki kufanya maamuzi ya
jinsi ya kuongoza nchi.
Alisema utamaduni, ambao umezoeleka hapa nchini na ambao unatumiwa na
serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuongoza nchi kutokea Dar es
Salaam. Mbowe alisema hatua hiyo imeonyesha kushindwa kuboresha hali ya
maisha ya Watanzania wengi.
Kwa zaidi ya miaka 20 sasa Tanzania tumekuwa na utamaduni wa kutawala
nchi kutokea Dar es Salaam. Chadema tumeliona hili na tumegundua kasoro
zake. Ndiyo maana tumeamua kuja na sera ya majimbo ili kusogeza madaraka
kwa wananchi, alisema.
Alisema kwa kutumia mfumo huo, CCM imeonyesha kushindwa kushughulikia
matatizo ya msingi ya wananchi, ikiwamo mgawanyo sahihi wa rasilimali za
taifa. Pamoja na kusogeza madaraka kwa wananchi, sera ya majimbo
inalenga kutaka kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao
tofauti na sasa. Maeneo yenye raslimali nyingi kama madini, ndiyo yenye
kiwango kikubwa cha umaskini, alisema.
Alisema pia kwa kufuata mfumo huo, ndiyo sababu serikali ya CCM imekuwa
ikijipanga kuwadhibiti viongozi wa Chadema kila wanapojipanga kwenda
kufanya shughuli za kisiasa maeneo mbalimbali nchini.
Alisema kwa kufuata sera ya majimbo, serikali ya CCM haiwezi tena
kuwadhibiti viongozi wa Chadema isipokuwa watashtukia chama hicho
kimeshika dola na kuongoza nchi.
CHANZO: NIPASHE
Mkuu,
CCM siyo wajinga kama wengi wanavyopenda kuaminisha watu hapa. Hata viongozi wa CDM wanalijua hili hasa wakiangalia historia ya siasa za vyama vingi ilivyo nchini.
Viongozi wa CDM wako kwenye cross road katika maamuzi. Either, to take risk or continue doing the same. Matukio ya hivi karibuni ndani ya chama yanaonyesha viongozi bado wanasita sita na kwa kufanya hivyo, inabidi watumie njia rahisi isiyo na political risk.
Hawana jinsi huko mbeleni inabidi wachukue risk kwa manufaa ya kesho si katika utendaji wao tu bali hata katika macho ya wananchi. Kama unavyoona hapa JF kuna watu wameanza kuuliza uliza kuhusu hii kitu ( consolidation of power).
Naona kama tunatofautiana hapa.Kumbuka hii hoja imeanzia kwenye vetting.Mkuu katika siasa, practically, pale mtu anapokuwa mwanachama basi huyo anahesabika kama ameingia kwenye system ya chama kwa sababu kuwa mwanachama maana yake unaijua na kuikubali falsafa, itikadi, sera na malengo ya chama, na cha muhimu kabisa ni KUKIPIGANIA NA KUKILINDA CHAMA (LOYALTY), Kwa siasa zetu, hii kitu kwa sasa imekuwa ni zero, kwa maana kuwa, uanachama umekuwa ni nguzo mojawapo katika public spinning. Siyo kitu cha kushangaza kila siku watu wanabadilisha uanachama kama njugu.
Kwa jinsi siasa zetu zilivyo, kujuana imekuwa ni mojawapo ya merits ya kuwa kiongozi wa kisiasa kwa misingi ya sababu nilizoziainisha hapo juu. Kwa sababu kama hizo, hata viongozi wa CDM inawawia vigumu kujipambanua nje ya misingi hiyo ukichukulia kuwa, chama kwa sasa kina wanachama wa aina zote ( mamluki, loyal and neither mamluki nor loyal)
By the way, just for my benefit how many total votes cast for presidential candidates and for each in 2010....?? It is just a question, then you guys can continue with your so called analysis or discussion and cents adding business.
Good day all!
By the way, just for my benefit how many total votes cast for presidential candidates and for each in 2010....?? It is just a question, then you guys can continue with your so called analysis or discussion and cents adding business.
Good day all!