Mbowe, Steven Nyerere mikononi mwa polisi

Mbowe, Steven Nyerere mikononi mwa polisi

Hata hivyo haiwezi kubatilisha kwamba Mwigulu, Napee na baadhi ya wabunge walikuwa wanamtetea Wema. Mtatenda haki kama mtawakata wote waliotajwa kwenye clip ikiwemo msukuma....
 
Kamanda Ziro tumechoka ukanjanja wako
 
Steve%20Nyerere%202.jpg

Kufuatia kusambaa mtandanoni kwa clip ya sauti inayodhaniwa kuwa ya Steve Nyerere akizungumza na Mama yake msanii Wema Sepetu, utata umeibuka mara baada ya kuwepo taarifa kuwa Steve Nyerere amedakwa na polisi kwa mahojiano maalumu.

Akizungumza leo na wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Sirro amesema yeye hajamuita Steve Nyerere lakini huenda akawa ameitwa na maafisa wake wa upelelezi kwa ajili ya mahojiano, jambo ambalo ni sahihi.

Sirro amesema kuna kikosi maalum alichokipa kazi hiyo ya kumkamata na kumhoji Steve Nyerere na endapo msanii huyo anahojiwa ataweza kuachiwa kama kikosi hicho kitajiridhisha kuwa anastahili dhama, lakini kama kitaona bado kinamuhitaji, kitaendelea kumshikilia.

Msanii huyo ameingia kwenye kadhia hiyo baada ya kusambaa kwa sauti zinazodaiwa kuwa ni mazungumzo kati yake na Mama wa Msanii Wema Sepetu, kuhusu sakata la dawa za kulevya linalomkabili Wema Sepetu.

Source: Eatv
 
Wanahisi huenda na yeye akaanza kuwa msaliti
Waangalie 2020 huyu STEVE NYERERE aweza hamia CHADEMA
maana tangu uthubutu uoneshe na Mzee Lowassa watu hawana cha kupoteza
 
Yaan kwenye yale mazungumzo yoote polisi wanacho hoji ni nini hasa cha kuwasaidia!!?
Maana nilikuwa naskia pumba tu na nilisikitikia taifa langu linako kwenda.
Pia aliye vujisha taarifa za siri za watu naye akamatwe ahojiwe maana kavunja privacy, japo ya watu waliokuwa wana ongea pumba ki aina.
 
Hata mimi sikuipenda. Ila mie nimeona (samahani if I am wrong) ni mama ndie aliyerekodi na kuiweka hadharani. And the timing was right, just after waking up, most people find it hard to put their defenses up.
 
Hili sasa litakuja Wimbi la wasanii kihama chama kwa staili hii hapana ni uonevu mkubwa kama hata yale maongezi ni uchochezi duuu
 
Mnamo January mosi mwaka 1990. Pound moja ya uingereza GBP £ ilikua sawa na Shilingi 300 za Tanzania Tshs.

Je wajua thamani ya pound moja ya uingereza kwa shilingi ya kitanzania leo.

Haya ya Wema Sepetu, haya ya Steve Nyerere wala hayatorudisha thamani ya Shilingi yetu.

Tuyapuuze, tufanye kazi, tuinue uchumi wetu.
ic-9349.jpg
 
Hii selikari vip kutwa mahakamani hizi kesi huwatunashinda ila tukumbuke tumetoa Hadi nyingi kwa wanainchi tunge elekeza nguvu vitu vya msingi lakini sio kukomohana
 
Steve%20Nyerere%202.jpg

Kufuatia kusambaa mtandanoni kwa clip ya sauti inayodhaniwa kuwa ya Steve Nyerere akizungumza na Mama yake msanii Wema Sepetu, utata umeibuka mara baada ya kuwepo taarifa kuwa Steve Nyerere amedakwa na polisi kwa mahojiano maalumu.

Akizungumza leo na wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Sirro amesema yeye hajamuita Steve Nyerere lakini huenda akawa ameitwa na maafisa wake wa upelelezi kwa ajili ya mahojiano, jambo ambalo ni sahihi.

Sirro amesema kuna kikosi maalum alichokipa kazi hiyo ya kumkamata na kumhoji Steve Nyerere na endapo msanii huyo anahojiwa ataweza kuachiwa kama kikosi hicho kitajiridhisha kuwa anastahili dhama, lakini kama kitaona bado kinamuhitaji, kitaendelea kumshikilia.

Msanii huyo ameingia kwenye kadhia hiyo baada ya kusambaa kwa sauti zinazodaiwa kuwa ni mazungumzo kati yake na Mama wa Msanii Wema Sepetu, kuhusu sakata la dawa za kulevya linalomkabili Wema Sepetu.

Source: Eatv

Steve Nyerere ulinistaajabisha mno nilipokusikia katika ile clip inayosambaa kila mara ukirudia rudia kusema Uwoga nao ni Silaha na Ushujaa kwani sidhani kama akina Mzee Kwame Nkurumah, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Patrice Emelly Lumumba na Nelson Tata Madiba Mandela wangekuwa waoga kama Wewe leo Ghana, Tanzania, DRC ( formerly Zaire ) na South Africa zingefika hapo zilipo baada ya kuwa chini ya Mateso ya Wakoloni kwa muda mrefu.

Labda leo nikusaidie tu kuwa siku nyingine ukiwa na ukweli na uhakika juu ya kitu fulani kiseme tu moja kwa moja bila kupepesa, kumung'unya wala kutikisa kwani kusema Kwako ukweli juu ya jambo fulani lenye utata utakuweka huru na vile vile utakuwa pia umempendeza Mwenyezi Mungu ambaye humpenda zaidi Mtu Mkweli.

Sasa mbona sioni tofauti kwani jana ulisema uwoga ni ushujaa na kwamba usingeweza kusema lolote tena juu ya sakata zima la Wema Sepetu na RC Makonda halafu leo tena umekamatwa na kwenda kuhojiwa. Je huoni kama jana ile ungefunguka tu moja kwa moja ingekusaidia zaidi na hata sisi wengine tungekuunga mkono kwa hali na mali katika kukusaidia pindi mtiti wa kukamatwa ukianza.

Ukimaliza kuhojiwa huko tafadhali badilisha jina lako na sasa badala ya kujiita Steve Nyerere sasa jiite Steve Yaya Jammeh kwani mnafanana kwa vitu vingi mno. Kila la kheri!
 
Back
Top Bottom