Mbowe, Slaa, Zitto kulipua bomu Mwanza

Sasa hii nayo ni breking nyuzi?

SiSiEmu ni mijambawazi ya mchana kweupe. Ni muhimu kuwang'oa madarakani ili washike adabu yao. Wakome kabisa kutuibia watanzania na kutufanya madaraja.
 
Sikumoja nilihudhuri mkutano wa Chadema mahali mahali fulani, Zitto Kabwe alikuwa anahutubia kuhusu hali ya ufisadi nchini na akawa anafafanua namna CCM walivyoifukarisha nchi hii na namna wanavyoendelea kuimaliza. Sasa pembeni yangu wakawepo jamaa tena vijana, wakasema kwamba,"Hata hawa wapinzani tukiwapa na wenyewe watakula tu, bora haohao CCM waendelee kwa sababu wameshakula na wameshiba". Hakyanani nilisikitika sana. Kwa kweli kwa hali na ujinga wa Watanzania kuing'oa CCM itachukua mda sana. mbumbumbu bado wengi sana. Tusikate tamaa wapenda mageuzi wa kweli ishalah iko siku tutashinda.
 
Ni kweli safari tunayo ndefu sana, lakini kama wasemavyo waswahili 'mwanzo wa safari hatua' Kwakweli Chadema kupitia mpango wao wa kupambana na ufisadi kwa kuumwaga hadharani ni hatua, Tusisahau kwamba mafisadi nao lazima wajihami kwa nguvu zote ili waendelee kutetea kujineemesha kwao kwa garama yoyote ile hasa kwa mtaji wao mkubwa wa umasikini wetu na uelewa mdogo has walio tuzinga nao wa elimu ya darasa la saba!

kwa mazingira ya kibongo jinsi yalivo ya demokrasia ya maneno bila matendo, hii njia ya kumwaga vyote kwa wananchi ndiyo pekee itakayo saidia. Walau wapo wachache japo kwa taratibu wataanza elewa na 'with time' elimu itafika mbali zaidi.

Nawataia shime CHADEMA songa mbele kwa nguvu zote, na kwa vile mnatetea kweli tupu Mungu wetu atakuwa upande wenu na kwa uwezo wake tutashinda.
 
nao waachane na maneno, wamtume Tundu Lissu aandae mashitaka dhidi ya mafisadi waende mahakamani
Mpita Njia,
Nakusheshimu, lakini sijui tueleze mara ngapi sababu ya kutokwenda mahakamani. Kesi ngapi ziko mahakamani miaka 10 au hazijaanza kusikilizwa au zimeanza zimekwama. Is that what we want. Kwa sisi tunaofuatilia, tunajua this is the only effective way, kwa sababu angalau sehemu ya matokeo yameanza kuonekana.

Matokeo ya Pressure ya Wananchi tangu tulipotangaza Mwembe Yanga asiyeyaona basi hataki tu kuyaona, hata kama hatujafika tunakotaka. Lakini mahakamani ya mafisadi ni kesi ya Jinai, Lisu kwa sheria hawezi kuifungua isipokuwa window pekee ni Private Prosecution, ambayo nayo kwa Tanzania process yake ni ngumu na hata ukipata DPP anauwezo wa kuweka "Nolle Prosequi" wakati wowote akaifuta.

Tumeeleza haya mara nyingi, lakini hatutachoka kutoa elimu. Njia pekee ya vita hivi ni shinikizo kutoka kwa wananchi. Ndani ya Bunge ni window nyingine, kwa composition ya Bunge lilivyo sasa hivi, ni ngumu sana mnaona hata maswala ya Richomond yaliyotokea Bungeni yanavyopigwa chenga. The only avenue ni wenye uchungu na nchi yao Wananchi kupiga kelele kwa nguvu zaidi.

Walipompokea Rais kwa mabango mwaka jana, walipowazomea Wabunge wa CCM kwenye majimbo yao, tulipata ahueni sana na midomo yao ikafunguka. Wananchi wakipiga kelele tena, wataacha kuunga hoja asilimia mia kwa mia na kwa pamoja tutaikaba serikali hadi iwajibike. Ndicho tunachojenga.

Kama hata kwenye JF hamtuelewi naona itakuwa kazi kweli kwa Watanzania wa vijijini kutuelewa!
 
Nimeshasema hapa ukumbini kwetu mwanana kwamba ufisadi hautakwisha Tanzania mpaka CCM wafundishwe adabu na wapiga kura kwa kuondolewa madarakani, vinginevyo hakutakuwa na la maana lolote kuhusiana na mapambano ya mafisadi.

Sasa ni karibu mwaka mmoja hakuna aliyekamatwa, majina ya waliorudisha hizo pesa ambazo hakuna anayejua zimewekwa wapi bado ni siri. Mafisadi bado wanaendelea kupeta na mabilioni yao haramu ndani na nje ya nchi. Hata Waziri Mkuu Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi walithubutu kutamka hadharani kwamba mafisadi ni matajiri wakubwa hivyo kuwakamata kutasababisha nchi iwake moto! Kwa maana nyingine serikali yenye jeshi lilimtoa nduli na "kuikomboa Comoro", polisi, FFU, na wananchi 40 millioni wanaounga mkono mapambano dhidi ya ufisadi linaogopa kikundi cha mafisadi kisichokuwa na watu hata 1,000! Only in Tanzania!
:(:(:(

Kwa kila mwenye akili timammu atajiuliza kama kweli CCM haikuhusika na fedha za EPA kwa nini JK hajathubutu kuwataja wezi wa fedha hizo hadharani?.Ushahidi upo na upo wazi sema tu tatizo ni kuwa wezi na waliofaidi kutokana na wizi huo ndio walioshikilia dola.

Zipo taarifa kuwa kuna usia wa Marehemu Balali kuhusu skendo la EPA.Wosia huo umeweka bayana kila kitu kuhusu EPA.Hakukuwa na haja ya kuunda tume.Kila kitu kipo wazi tu.

Kama kweli tunataka kuisafisha nchi yetu ni lazima watanzania wenye mapenzi mema na nchi hii wawajibike kwa kutumia nguvu ya kura kuwaweka CCM kando.Tufike mahala tuachane na unazi wa kisiasa badala yake tuitizame na kuisikitikia nchi.Hakuna anayeichukia CCM bali uovu unaofanywa na baadhi ya wanachama wake na chama husika kuwakingia kifua.Chama kinachojali taifa hakiwezi kutetea uchafu kwa maslahi ya chama.Huo ni usaliti na lazima upigwe vita.Nitaiheshimu CCM iliyo safi na siyo hii ninayoifahamu leo.
 
Mpita Njia,
Nakusheshimu, lakini sijui tueleze mara ngapi sababu ya kutokwenda mahakamani. Kesi ngapi ziko mahakamani miaka 10 au hazijaanza kusikilizwa au zimeanza zimekwama. Is that what we want. Kwa sisi tunaofuatilia, tunajua this is the only effective way, kwa sababu angalau sehemu ya matokeo yameanza kuonekana.

Matokeo ya Pressure ya Wananchi tangu tulipotangaza Mwembe Yanga asiyeyaona basi hataki tu kuyaona, hata kama hatujafika tunakotaka. Lakini mahakamani ya mafisadi ni kesi ya Jinai, Lisu kwa sheria hawezi kuifungua isipokuwa window pekee ni Private Prosecution, ambayo nayo kwa Tanzania process yake ni ngumu na hata ukipata DPP anauwezo wa kuweka "Nolle Prosequi" wakati wowote akaifuta.

Tumeeleza haya mara nyingi, lakini hatutachoka kutoa elimu. Njia pekee ya vita hivi ni shinikizo kutoka kwa wananchi. Ndani ya Bunge ni window nyingine, kwa composition ya Bunge lilivyo sasa hivi, ni ngumu sana mnaona hata maswala ya Richomond yaliyotokea Bungeni yanavyopigwa chenga. The only avenue ni wenye uchungu na nchi yao Wananchi kupiga kelele kwa nguvu zaidi.
Walipompokea Rais kwa mabango mwaka jana, walipowazomea Wabunge wa CCM kwenye majimbo yao, tulipata ahueni sana na midomo yao ikafunguka. Wananchi wakipiga kelele tena, wataacha kuunga hoja asilimia mia kwa mia na kwa pamoja tutaikaba serikali hadi iwajibike. Ndicho tunachojenga.

Kama hata kwenye JF hamtuelewi naona itakuwa kazi kweli kwa Watanzania wa vijijini kutuelewa!

Mhe.Slaa
Nakuunga mkono hoja uliyotoa.Vita yoyote dhidi ya CCM haiwezi kushindwa ndani ya mahakama yoyote nchini.CCM ni chama dola na nguvu zake zina mizizi kwenye arms zote za utawala (executive, parliament na judiciary).Nguvu hii ndiyo inayotumika kuua harakati zote za wapenda nchi yao kutafuta haki na maendeleo kwa njia za kisheria.

Njia pekee tuliyonayo sisi wenye uchungu na Tanzania ni kuelewa kuwa tunahitaji mbadala wa CCM ili kuweza kuvuka ng'ambo ya pili ya mto kuyafikia maendeleo.Shinikizo la wanachi ni muhimu kuliko njia nyingine yeyote.Kama tukiungana kupiga kelele na kukataa uovu ndani ya nchi kama wananchi kww ujumla ni hakika kuwa vita dhidi ya ufisadi na kila uovi itafanikiwa.

Hatua ya pili ni kwa bunge letu kuwa na composition inayoridhisha ya wabunge wa upinzani.Ili kuupa upinzani nguvu tuupe wabunge wasiopungua mia na hamsini kusudi udhibiti wa serikali uwepo.Hili ni jukumu la wananchi wanaopenda nchi yao.Kura zetu ndizo zitakazofanikisha kuwepo kwa uhai bungeni.Haiwezekan kwa Slaa, Zitto, Hamad,Mdee na wengine kwa uchache wao wakawa na nguvu dhidi ya idadi kubwa ya wabunge wa CCM ambao wengi wao wanafuata matakwa ya chama na siyo kuwatetea wananchi.

Kazi kubwa iko kwetu wananchi.Tukifunguka macho na masikio tukauona ukweli kabla ya 2010 ni hakika kuwa yatakuwepo mabadiliko ya kweli, uhuru wa kweli kwa kila mtanzania.
Kila mtanzania sharti aishi na kauli mbiu "Mpaka kieleweke"
 
Na ikipatikana nguvu kubwa zaidi ya upinzani bungeni itakuwa rahisi zaidi kuisafisha serikali, mahakama etc kwa haraka na urahisi.
 
Tanzania itakombolewa na wananchi wa Tanzania. Wananchi wa Tanzania wanahitaji kuelewa kisa cha wao kuwa maskini. Chadema kumwaga mabomu ni kuufunua umma wa waTanzania. Pia, huwapa hekaheka wanaotawala kujua kuwa hakuna lililofichika. Chadema tunawaombea kila lililo heri katika mapambano haya makali na Serikali isiyo na masikio.
 
CHADEMA yawasha moto

na Sitta Tumma, Mwanza
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA), kimesema Tanzania imegeuzwa shamba la mavuno ya mafisadi, pamoja na makampuni ya madini yanayomilikiwa na wawekezaji wageni.

Hali hiyo imetokana na baadhi ya viongozi na watendaji wakuu wa serikali kuanza kujichotea mabilioni ya fedha za umma, ikiwa ni kupitia kampuni za madini ambapo trioni 1.3, zimepotea kutokana na baadhi ya makampuni ya madini ya nje kuliibia taifa na kutokomea na fedha hizo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakati akihutubia maelfu ya wananchi mkoani hapa, katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu chama hicho kitangaze hadharani majina 11 ya mafisadi, Septemba 15, mwaka jana.

Mbowe ambaye alitumia muda mwingi kuzungumzia hatima ya vita dhidi ya ufisadi na maendeleo katika taifa hili, alisema makampuni hayo ya madini, yamekuwa yakitumia nafasi zake kuchota mabilioni ya fedha, huku Watanzania wenyewe wakiachwa watupu.

Huku akionyesha kukerwa na ufisadi ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete, alisema katika miaka 10 iliyopita, zaidi ya sh bilioni 850 ziliibwa nchini na makampuni hayo ya kigeni.

Mbali ya hayo, zaidi ya sh bilioni 155, zilipotea miaka ya hivi karibuni, fedha ambazo zimetumika katika mradi wa Meremeta na kutokana na hali hiyo, taifa limekuwa likipoteza fedha nyingi kwa njia ya udanganyifu.

"Jamani wananchi wa Mwanza, makampuni ya madini yamekuwa yakichuma fedha nyingi na kutokomea nazo na kuliacha taifa likiwa jeupe na wananchi wake, licha ya kuwa na rasilimali nyingi," alisema Mbowe.

"Trilioni 1.3 fedha za Kitanzania zimeibwa na makampuni hayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na zaidi ya sh bilioni 850 pia zimeibwa na makampuni ya kuchimba madini, huku tukijivuna tuna viongozi, hivi kweli tuna viongozi?" alihoji Mbowe.

Kuhusu wizi wa fedha zilizoibwa kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Mbowe alieleza kushangazwa kwake na hatua ya Rais Kikwete kushindwa kuwafikisha mahakamani wahusika waliochota fedha hizo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kuhusu ziara zinazofanywa mara kwa mara na Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti huyo wa CHADEMA taifa, alieleza wazi wazi kuwa hiyo ni hali ya kujikomba na kujidhalilisha kwa Serikali ya Marekani, kwani ndiyo inayochota mabilioni ya fedha na kuwaacha Watanzania wakiwa maskini wa kutupwa.

"Yeye anaachia mali inakombwa halafu anatoka hapa kwenda Marekani kuomba msaada wakati anaowaomba msaada ndio anaowapa vibali vya kusomba mali ya taifa lake...hii ni aibu na huenda yeye rais halijui hilo.

"Kila mara safari Ulaya, kila mara safari Ulaya...mmh! Huko Ulaya kunani?...utaombaje msaada kila siku tena kwa watu wanaokuibia? Hii ni fedheha kwake na kama hajui alitambue hilo na Watanzania tunadhalilishwa pia," alisema Mbowe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa yeye alimtaja mbunge mmoja wa CCM kuwa ndiye kinara mkubwa wa ufisadi katika fedha za EPA.

Dk. Slaa alisema, mbunge huyo ndiye kiongozi na injinia wa ufisadi, na kwamba mwaka 2005 alisajili kampuni moja ya kifisadi kisha akachota BoT sh bilioni 40 ndani ya wiki nane, fedha za umma.

"Nasema hivi, tunamfahamu kwa nyendo zake hapo Benki Kuu, akipenda aende mahakamani, lakini habari ndiyo hiyo! Na katika kampuni yake hiyo ya kifisadi alikuja kuimilikisha kwa aliyekuwa mlinzi wake.

"Kampuni hiyo ya kifisadi ilisajiliwa rasmi Septemba 29 mwaka 2005...lakini mtu huyu kwa kutaka kujivua ufisadi wake aliiandikisha kuwa ni mali ya mlinzi wake," alisema Dk. Slaa.

Aidha, alimtaka Rais Kikwete atangaze hadharani sababu za kutomhoji aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, juu ya upotevu wa fedha hizo za EPA, alhali yeye alikuwa ni mkuu wa taasisi hiyo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alitumia muda wake kuzungumzia suala zima la madini na ufisadi ndani ya sekta hiyo.

Zitto alianza kwa kusema kuwa: "Mikataba yote ya madini haina uhalali wa kisheria, taifa linaibiwa mabilioni ya fedha huku viongozi na serikali kwa ujumla wakishindwa kudhibiti hali hiyo."

Akitolea mfano hai kwa mgodi wa Bulyanhulu, Zitto alisema awali mgodi huo ulikuwa ukimilikiwa na serikali chini ya TAMICO, na baadaye mgodi huo ukauzwa kwa Wazungu kutoka nchini Canada kwa dola za Marekani milioni 20.

Alisema, baada ya Wazungu hao kunufaika na mgodi huo, mwaka 1999 waliuuza kwa dola za Marekani milioni 348, na kwamba ulitumika pia kujenga mgodi wa Buzwagi ambao mkataba wake bado umezua maswali mengi kwa Watanzania
.
 
Those numbers are ridiculous...can make you lose the purpose of living in
such a country.Yaani wamekomba mpaka zimeisha..duh!!!
 
Kuna BOMU lolote Jipya limelipuliwa huko Mwanza....?

Hakuna jipya ndo yaleyale ya EPA na buzwagi!Chadema mmeacha uchunguzi nini?mbona hayo ya buzwagi ndo mmeyang'ang'ania hadi leo tunataka mapya!au sasa hivi serikali ni safi?
 
Mgodi kuuzwa kwa million 20 si bei ya kununua mabasi tu hiyo!

Hakuna anayejali mradi wamemuuzia mtu mwenye ngozi nyeupe kutoka nchi za magharibi basi wao wanaridhika kabisa.
 
Huyo mbunge fisadi ni nani? Dr Slaa alimtaja kwa jina halafu gazeti limeogopa kumuandika au? Halafu taratibu za kusajili makampuni pale BRELA inabidi ziangaliwe upya.

Watu wanapiga picha mpaka vichaa wa barabara kisha wanazipeleka pale kwamba ndio picha za wakurugenzui. Kisha wakishachota fedha benki, mtawatafute hao wakurugenzi hewa mpaka mchoke!

Kwa kifupi biashara ya kuanzisha mtandao wa kifisadi Bongo inawezekana ikawa inalipa sana kwa sasa. Kwani watuhumiwa hawafungwi, wala kubughuziwa
 
Bahati nzuri nilikuwepo pale kwenye huo mkutano na Dr Slaa alimtaja wazi kwa jina Rostam Aziz kuwa ndiye mwenye Kagoda Agriculture na kule BRELA anaonyesha jina la mtu mwingine ambaye ni mlinzi katika kampuni yake ya Caspian kuwa eti yeye ndiye Mkurugenzi wa hiyo kampuni.

Kazi ipo kweli kweli, tumenyonywa damu na sasa yanaanza kutoka maji tu. Wadanganyika tuamke nasi tupate uhuru wetu kama wenzetu Wakenya na Wazimbabwe.
 
Mpita Njia,
Nakusheshimu, lakini sijui tueleze mara ngapi sababu ya kutokwenda mahakamani. Kesi ngapi ziko mahakamani miaka 10 au hazijaanza kusikilizwa au zimeanza zimekwama. Is that what we want. Kwa sisi tunaofuatilia, tunajua this is the only effective way, kwa sababu angalau sehemu ya matokeo yameanza kuonekana.

Matokeo ya Pressure ya Wananchi tangu tulipotangaza Mwembe Yanga asiyeyaona basi hataki tu kuyaona, hata kama hatujafika tunakotaka. Lakini mahakamani ya mafisadi ni kesi ya Jinai, Lisu kwa sheria hawezi kuifungua isipokuwa window pekee ni Private Prosecution, ambayo nayo kwa Tanzania process yake ni ngumu na hata ukipata DPP anauwezo wa kuweka "Nolle Prosequi" wakati wowote akaifuta.

Tumeeleza haya mara nyingi, lakini hatutachoka kutoa elimu. Njia pekee ya vita hivi ni shinikizo kutoka kwa wananchi. Ndani ya Bunge ni window nyingine, kwa composition ya Bunge lilivyo sasa hivi, ni ngumu sana mnaona hata maswala ya Richomond yaliyotokea Bungeni yanavyopigwa chenga. The only avenue ni wenye uchungu na nchi yao Wananchi kupiga kelele kwa nguvu zaidi.

Walipompokea Rais kwa mabango mwaka jana, walipowazomea Wabunge wa CCM kwenye majimbo yao, tulipata ahueni sana na midomo yao ikafunguka. Wananchi wakipiga kelele tena, wataacha kuunga hoja asilimia mia kwa mia na kwa pamoja tutaikaba serikali hadi iwajibike. Ndicho tunachojenga.

Kama hata kwenye JF hamtuelewi naona itakuwa kazi kweli kwa Watanzania wa vijijini kutuelewa!

Dr Slaa
Wanaelewa wanafanya makusudi kuwapotosha irregular members.Humu kwenye jf kuna watu wanalipiwa air time na mafisadi ndio maana wanafanya kejeli kukatisha wapiganaji tamaa.Lakini kazi mnayofanya ni ya kitume,mwisho wa yote mtafanikiwa.Robert Mugabe aliapa kuwa Tsivingarai hatatawala,lakini mazingira yamebadilika kwa kila mtu kuona.Pamoja na yote reality speaks for itself.
 
Yule yule mtuhumiwa wa ufisadi katika sakata la Richmond, ndugu Nazir Kalamagi last week alikwenda azania akitaka eti aweke mapesa yake aliyoiba na kuleta majina ya watu ambae yeye angetaka wakopeshwe fedha hizo kupitia benk. Kutokana na uzalendo wa mgt ya benki hiyo walikataa katu kufanya kitendo hicho cha kiibia taifa letu kwa njia za kiinimacho. Ndipo fedhuli huyu alipoondoka kwa aibu huku akilaani kitendo cha kutoswa.
 
Back
Top Bottom