Mbowe: Slaa anapumzika, msiwe na hofu

Mbowe: Slaa anapumzika, msiwe na hofu

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,316
Reaction score
23,178
Akizungumza na Radio one mda huu saa 4, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema Dr Slaa hawezi kuhama chama hicho na hafikirii kamwe, kwa sasa anapumzika kwa likizo ya wiki moja.

Alipoulizwa kuhusu Slaa kutokubaliana na ujio Wa Lowassa amejibu kila kitu tulikubaliana na Slaa mwenyewe aliunga mkono suala hilo.

Mbowe amesema wananchi na wanachadema kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwani hiki chama ni makini na hakiwezi fanya maamuzi bila maridhiano na akasisitiza kuwapuuza wanaoeneza habari kuwa Slaa amejiuzulu siasa.

Alipoulizwa mara ya mwisho kuwasiliana na Dr Slaa ni lini akajibu jana saa kumi na mbili jioni.

Alipoulizwa walizungumza nini akajibu anajua yeye na Slaa.

Walipomuuliza hasa mbona sisi tukimpigia hapatikani akajibu sijui lakini mimi nimewasiliana nae jana.


Chanzo: Radio one
 
kichwa cha habari, na uliyoandika ni tofauti..mbona mbowe hajasema slaa anapumzika
 
Slaa siyo strategist mzuri .... amepunguza kasi ya magamba kujivua magamba yao
 
kichwa cha habari, na uliyoandika ni tofauti..mbona mbowe hajasema slaa anapumzika


Nyie watu wengine unashabiki umewaathiri sana, umeharibu hadi akili zenu, hata kusoma kwa makini ili uelewe kilichoandikwa unashindwa, unakurupuka tu na kusema hajasema anapumzika. Iruhusu akili yako ijitegemee
 
mnyika anahangaikia ubunge kama hamtaki slaa agombee kupitia act
 
tunataka dr slaa mwenyewe amekataa kumsemea
 
Watu wanasambaza uongo sababu hawaitakii mema chadema, tuko imara zaidi. Dr yupo katika mapumziko, soon atasikika
 
Kuna vikao muhimu vya chama wiki hii Sasa katibu mkuu wa chama kuwa likizo ktk kipndi hiki ni ishara ya kutotaka kushiriki hivyo vikao au Ndio alivyoamua kupumzka kipnd hiki!!? Ni vizur kama hayo aliyosema mh Mbowe yakabaki hivyo na kusiwe na agenda nyingine ya siri kwa mh Dr Slaa kwan watawapa nafas wapnzan wao kujiimarisha tena wakt huu ambao wamepata mtikisiko baada ya ujio wa mh Lowasa ktk chama cha cdm..
 
Back
Top Bottom