Katika hili nampongeza Freeman Mbowe kwa sababu hajawahi kuwa mjamaa na amesimamia itikadi yake.
Njoo CCM sasa, utamkuta Hamis anatembea na kifimbo cha kama mwalimu Nyerere yaani fix tu...
Yawezekana unachosema ni kweli, lakini kwa tamaa ya madaraka ameiharibu sana Chadema.
Sasa Chadema ni chama cha wajamaa. Walitushawishi wakati wa ujana wetu tujiunge na chadena kwa kuwa tuliamini ubepari ndio njia halisi ya mwanadamu hasa baada ya kufa na kusambaratika Soviet Unioni.
Leo tuna makamanda wavaa makombati kwenye chama na hatuna tofauti na wajamaa CCM, kwa hali hiyo ni bora tujiunge CCM ili ijulikane moja, kuliko kuwa Popo: myama wakati huo huo ndege.
Matajiri tumekuwa tunataka serikali itusaidie, wakati falsafa ilikuwa sisi wanachama tuisaidie serikali kwa kuionyesha njia bora ya kutawala bila kutamani mali ya wananchi.
Sasa wote tunaonekana tunakimbilia mabaki kwenye jaa kama wajamaa wa CCM wakati hatuna ulazima.
Badala ya kuvaa suti tunabaki kung'ang'ania makombati kama wafanyakazi wa viwandani waliokuwa wawe wapagazi wetu.
Wacha Mbowe afungwe chama kirudi katika ubepari. Kwanini kujaza watu wenye elimu isiyo eleweka katika uogozi wa juu wa Chama ili afanane nao kielimu kwa kuogopa ushindani wa maarifa na nguvu ya mali kwenye chama.
Awe huru bila ushindani kuwatumikisha viongozi wenye elimu ya wasiwasi na maisha tegemezi ili iwe rahisi kuwatumikisha na kuishi kwa rehema za Mwenyekiti.
Chadema ni chama cha mabepari na wenye kuamini falsafa ya kutajirika. Walala hoi waachwe na chama chao.
Mfyuuuuuuuuu.