Mbowe siyo mnafiki ameiishi itikadi ya Ubepari tokea ujana wake tofauti na CCM wengi wanaojifanya Wajamaa kumbe fix tu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,539
Katika hili nampongeza Freeman Mbowe kwa sababu hajawahi kuwa mjamaa na amesimamia itikadi yake.

Njoo CCM sasa, utamkuta Hamis anatembea na kifimbo cha kama mwalimu Nyerere yaani fix tu.

Kangi anavaa koti la bendera ni yale yale.

Waziri anavaa tai ya bendera nyuma ya pazia ukwasi wake hauhesabiki.

Na kadhalika...... nk!
 
IMG_20201006_152320.jpg

Halafu kesho utasikia maendereeoo hayana chama...
 
Ujamaa ni mfumo wa kitapeli tu. Kwa Hili mwalimu alipotea na kutupoteza, hakujuwahi kuwapo mtu mjamaa labda Yesu tu.
Hakuna nchi duniani ambayo ni capitalistic 100%..., Hakuna; Haya mambo ni theory on paper.

Hata marekani unapoweza ukaita they are capitalists lakini kuna welfare kuzidi hata huku, England tunakuwaona ni mabepari angalau kule kuna NHS (Bima kwa Wote) kuliko huku tunakojiita wajamaa.

Dunia inapoelekea Capitalism per se can never work.., kutakuja kuwa na system ya kuchukua the best in both worlds... Pia vision ya nyerere haikuwa kilichotokea, Yeye alitaka Ujamaa na kujitegemea Yaani the Commanding Heights of the Economy kuwa kwenye mikono na faida ya wote..., ila kilichotokea ni kulikuwa na Capitalists in Socialists Cloths..., As Human Nature will Have it.

Kwahio duniani pote what we have is Mixed Economy
 
Katika hili nampongeza Freeman Mbowe kwa sababu hajawahi kuwa mjamaa na amesimamia itikadi yake.

Njoo CCM sasa, utamkuta Hamis anatembea na kifimbo cha kama mwalimu Nyerere yaani fix tu...
Tofauti iko wazi!! Mbowe amepata kwa jasho lake na wazazi wake! wengine ni majizi ya kodi za wananchi. Ni shuruti mwizi ajifiche kwenye kivuli salama!!
 
Pole pole yeye kaiga sauti ya Nyerere kwny kuongea

Joseph Butiku yeye kaiga kukunja uso kwny paji la Uso ila Bepari anaemiliki ma shule

Warioba ana kimpango chake nakihifadhi

Usanii usanii mwingi tu
 
Katika hili nampongeza Freeman Mbowe kwa sababu hajawahi kuwa mjamaa na amesimamia itikadi yake.

Njoo CCM sasa, utamkuta Hamis anatembea na kifimbo cha kama mwalimu Nyerere yaani fix tu...
Ujamaa ni imani wala hutamsikia mjamaa wa siku hizi kutaka serikali kumiliki kila kitu au wanavijiji kuwekwa kwenye vijii vya ujamaa. Ujamaa ni sayansi ya jamii.

Msingi wake watu kuishi bila kuwepo tabaka la wanyonyaji kuwanyonya wenzao kiuchumi. Kwenye sayansi unajifunza na kurekebisha. Ccm kama vyama vingine vya kijamaa iliamua kutumia sekta binafsi kwa kudhibitiwa na umma kujenga uchumi usiokua na wanyonyaji.

Ndio mwanzo wa kuwepo mamlaka za udhibiti kwa kila sekta. Mamlaka hizo ni kama ewura kwenye mafuta, latra kwenye usafiri taa viwanja vya ndege etc etc.

Kuna sekta za uwekezaji matokeo ni muda mrefu serikali itawekeza. Pia kuna mashirika machache serikali itawekeza na kumiliki kwa ustawi wa taifa.

Wanachama wakongwe tunayajua haya ila siku hizi kuna wanaccm viherehere hadi viongozi hawayajui haya au wanafichwa.
 
Katika hili nampongeza Freeman Mbowe kwa sababu hajawahi kuwa mjamaa na amesimamia itikadi yake.

Njoo CCM sasa, utamkuta Hamis anatembea na kifimbo cha kama mwalimu Nyerere yaani fix tu...
Yawezekana unachosema ni kweli, lakini kwa tamaa ya madaraka ameiharibu sana Chadema.

Sasa Chadema ni chama cha wajamaa. Walitushawishi wakati wa ujana wetu tujiunge na chadena kwa kuwa tuliamini ubepari ndio njia halisi ya mwanadamu hasa baada ya kufa na kusambaratika Soviet Unioni.

Leo tuna makamanda wavaa makombati kwenye chama na hatuna tofauti na wajamaa CCM, kwa hali hiyo ni bora tujiunge CCM ili ijulikane moja, kuliko kuwa Popo: myama wakati huo huo ndege.

Matajiri tumekuwa tunataka serikali itusaidie, wakati falsafa ilikuwa sisi wanachama tuisaidie serikali kwa kuionyesha njia bora ya kutawala bila kutamani mali ya wananchi.

Sasa wote tunaonekana tunakimbilia mabaki kwenye jaa kama wajamaa wa CCM wakati hatuna ulazima.

Badala ya kuvaa suti tunabaki kung'ang'ania makombati kama wafanyakazi wa viwandani waliokuwa wawe wapagazi wetu.

Wacha Mbowe afungwe chama kirudi katika ubepari. Kwanini kujaza watu wenye elimu isiyo eleweka katika uogozi wa juu wa Chama ili afanane nao kielimu kwa kuogopa ushindani wa maarifa na nguvu ya mali kwenye chama.

Awe huru bila ushindani kuwatumikisha viongozi wenye elimu ya wasiwasi na maisha tegemezi ili iwe rahisi kuwatumikisha na kuishi kwa rehema za Mwenyekiti.

Chadema ni chama cha mabepari na wenye kuamini falsafa ya kutajirika. Walala hoi waachwe na chama chao.

Mfyuuuuuuuuu.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom