Mbowe: Rushwa imekithiri uchaguzi wetu mwaka huu

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe ameshangaa na kusikitika kuwa baadhi ya viongozi ndani ya chama chake kutumia rushwa na kushinda nafasi mbalimbali.

Akiongea mbele ya Kamati Kuu ya Chadema amesema kuna ushahidi ulio wazi uchaguzi wao ulija arushwa na kuonya kuchukua hatua 'unatumia pesa zako ili uwe kiongozi chamani 'alisikika akikaripia Mwenyekiti Mbowe.

Chanzo: ITV

===
My take:

Ni wazi kuwa wengi walioshinda walitumia rushwa na wale walishindwa walishindwa kwa uadilifu wao ni vema sasa uchaguzi ufanyike upya ili kuiruhusu haki itendeke ndani ya chama.

Kuna ulazima viongozi wajiondoe kabla wanachama hawajachukua hatua kali dhidi ya wahusika.

Kuna ulazima wa mbowe kupeleka majina TAKUKURU ili jinai ichunguzwe na walihusika wapelekwe mahakamani.

Namuomba Msajili wa vyama kufuta uchaguzi unaoendelea wa chadema kwani hata mwenyekiti amekili ulijaarushwa na mzee sumaye kusema ulijaa figisu, hila, vitisho, upendeleo na rushwa.

Kuna haja wanachadema humu JamiiForums kujiunga nami kutaka rushwa kukomeshwa ndani ya Chadema.

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kama kiongozi mkuu analalamika tena kwenye mkutano, ni nani basi atachukua hatua. Mbowe kwa kujua au kutokujua anakipeleka chama kaburini.
 
Unajua kwa Chadema iliyojaa uadilifu mwenyekiti kulalamikia rushwa kuwa kubwa ni kwa kiasi gani?
Basi yaweza kuwa 3-5% ya uchaguzi mzima, lakini kwa chama kama chadema hilo jambo haliwafurahishi.
Jee kwa kiwango hicho waweza kuutangaza uchaguzi mzima kuwa ni batili na urudiwe? Hapana gharama za uchaguzi ni kubwa mno na kwa kiwango hicho kinaweza kudhibitiwa kwa hatua za kinidhamu tuu.
Unadhani kwa nini CCM ambayo uchaguzi wao karibia 90% wanaingia madarakani kwa rushwa wanashindwa kurudia?
 
Hivi kama kiongozi mkuu analalamika tena kwenye mkutano, ni nani basi atachukua hatua. Mbowe kwa kujua au kutokujua anakipeleka chama kaburini.
Hahahaa hilo kaburi liko umbali gani ambako chama hakijafika mpaka sasa? maana yake hadithi za chama kufa na kupelekwa kaburini ni za muda mrefu na chama hakijafa na kaburini hakijafika, inamaana kuwa umbali wa kaburi ni kama aridhi na mbingu ambako mpaka sasa chama hakijafika?.
 
Hivi kama kiongozi mkuu analalamika tena kwenye mkutano, ni nani basi atachukua hatua. Mbowe kwa kujua au kutokujua anakipeleka chama kaburini.

Mbowe kama mtu mzima anapashwa alione kaburi lake na chama chake mapema na si kwa kuambiwa kama hivi, maamuzi ya kipuuzi ya hivi karibuni ni kaburi lake namba moja na bado kaongeza na kuubaliki uchaguzi uliojaa rushwa maana yake ni mamluki wameamua kuja kimatakotako wakiwa hawaonyeshi sura zao halisi halafu yeye kama mwenyekiti anakaa kimya na leo anaanza kulalamika kwenye vikao visivyo rasimi huo ni ujuha gani?

Watu makini wanatoa alarm yeye kapiga kimya hata kusema au kudanganya kuwa "ohhh Sumayi kashindwa kura kwa kuwa alikuwa hashiriki vikao and nrabrabrahhhh" nayo kashindwa?

Ukweli Mbowe amechoka au turudie kusema hana pumzi za kushindana zimemuishia sio kama zamani na hao mamluki ndio watakaomtoa uenyekiti na baadae wakiue kabisa chama mpaka kiwe kama updp au kama Mbowe anataka kuunga juhudi na maridhiano yake basi ni vizuri aende yeye na wanaomuunga na akiache CHADEMA kikiwa salama
 
Haa Mbowe anafanya watu nyumbu sana, yeye mwenyewe ndio mtoa rushwa mkubwa CDM.
 
USSR, Kuna kitu nakiona kinanukia eeh Mungu saidia iwe ni Ile bangi niliyovuta ujanani tu inanipeleka peleka.

Kwanza kahudhuria maadhimisho ya siku ya Uhuru na Sasa Mwenyekiti wa Chama ANASEMA uchaguzi wao ulijaa rushwa.

........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufipa kwa povu ndo mmefika sasa, badala ya kujadili namna rushwa inavyotafuna chadema mnatukana watu. Hamtaki kabisa kusikia kibaya kuhusu chadema hata kama mnaona kuna mambo yanaenda ndivyo sivyo, ndio maana mpo kimya ruzuku ya chama inatafunwa na wachache walioko makao makuu, hasa mkt. mpo kimyaaaa mmetulia kana kwamba hakuna kibaya.
 
Back
Top Bottom