MKWEPA KODI
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 28,700
- 71,104
Wanajua watanzania tunamwamini mbowe hawezi kujiuza Kama Malaya wengine wa kisiasa







Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameweka bayana msimamo wake kuhusu hali inayoendelea ndani ya chama hicho, hasa kuhusu nafasi ya uenyekiti, akisema hana tatizo na yeyote anayetaka nafasi hiyo ilimradi utaratibu ufuatwe.
Mbowe pia amesema angependa vijana wengi wajitokeze kuwania nafasi hiyo baada ya mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe kutangaza nia ya kugombea uenyekiti huku kukiwa na mjadala kuhusu muda wa miaka takriban 15 ambao mbunge huyo wa Hai amekuwa madarakani.
Mbowe (58) amejikuta katika wakati mgumu katika miaka ya karibuni, akipata changamoto kutoka nje na ndani; biashara na mali zake zikikumbana na mkono wa dola, huku kukiwa na chokochoko kutoka kwa watu ambao hawajajiweka bayana wanaohoji ukomo wa muda wake.
Lakini juzi, Mbowe ambaye ameiongoza Chadema tangu mwaka 2004, hakuonekana kuyumbishwa na hali hiyo.
“Sina shida kabisa kwa wanaojitokeza kugombea, lakini pia ni vema wakajua taratibu za chama zinataka nini mtu anapotaka kugombea nafasi ndani ya chama ikiwemo hiyo ya uenyekiti,” alisema Mbowe katika mahojiano na Mwananchi.
“Kama Chadema, hatupo tayari kuendesha chaguzi zitakazoleta vurugu isipokuwa (zinazoleta) mshikamano na kukifanya chama chetu kiendelee kusonga mbele kama chama kikuu cha upinzani.”
Kwa muda mrefu sana CCM imeonekana wazi kukosa raha kutokana na mhe. Mbowe kuwa mwenyekiti wa Chadema kiasi cha kujaribu mbinu mbalimbali na vitisho vya kumng'oa. Jambo la kujiuliza ni uenyekiti wa mhe. Mbowe kwanini unawanyima usingizi wanaccm kuliko wanachadema?