Mbowe: Ruksa kugombea uenyekiti CHADEMA

Mbowe: Ruksa kugombea uenyekiti CHADEMA

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameweka bayana msimamo wake kuhusu hali inayoendelea ndani ya chama hicho, hasa kuhusu nafasi ya uenyekiti, akisema hana tatizo na yeyote anayetaka nafasi hiyo ilimradi utaratibu ufuatwe.

Mbowe pia amesema angependa vijana wengi wajitokeze kuwania nafasi hiyo baada ya mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe kutangaza nia ya kugombea uenyekiti huku kukiwa na mjadala kuhusu muda wa miaka takriban 15 ambao mbunge huyo wa Hai amekuwa madarakani.

Mbowe (58) amejikuta katika wakati mgumu katika miaka ya karibuni, akipata changamoto kutoka nje na ndani; biashara na mali zake zikikumbana na mkono wa dola, huku kukiwa na chokochoko kutoka kwa watu ambao hawajajiweka bayana wanaohoji ukomo wa muda wake.

Lakini juzi, Mbowe ambaye ameiongoza Chadema tangu mwaka 2004, hakuonekana kuyumbishwa na hali hiyo.
“Sina shida kabisa kwa wanaojitokeza kugombea, lakini pia ni vema wakajua taratibu za chama zinataka nini mtu anapotaka kugombea nafasi ndani ya chama ikiwemo hiyo ya uenyekiti,” alisema Mbowe katika mahojiano na Mwananchi.

“Kama Chadema, hatupo tayari kuendesha chaguzi zitakazoleta vurugu isipokuwa (zinazoleta) mshikamano na kukifanya chama chetu kiendelee kusonga mbele kama chama kikuu cha upinzani.”
 
Nakubaliana asilimia mia moja na Mbowe. Demokrasia ndiyo hiyo sasa!
Petro are you sure hiyo nikauli ya Mbowe? Wakili mzima unaamini mambo ya mitandaoni bila ushahidi usio na mashaka au on the balance of probability! Hivi Punde ni Lumumba , unategemea nini kutoka kwake?
 
ni muda wa wanahisa kukaa chini kumchagua kiongozi mpya wa SACCOS kuu ya kaskazini
Itakuwa ni SACCOS ya kwanza duniani kuwa na nguvu kubwa ya kumtia hata uchizi kiongozi wa nchi.
Niambie unadhani katika siku ya kawaida ya Rais Magufuli inaweza kupita bila kuwaza au kuitaja hiyo SACCOS ya Chadema?
Siku nyingine uwe na adabu katika kuki address chama kikuu kama Chadema.
 
Nakubaliana asilimia mia moja na Mbowe. Demokrasia ndiyo hiyo sasa!
FB_IMG_1570488518462.jpg
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameweka bayana msimamo wake kuhusu hali inayoendelea ndani ya chama hicho, hasa kuhusu nafasi ya uenyekiti, akisema hana tatizo na yeyote anayetaka nafasi hiyo ilimradi utaratibu ufuatwe.

Mbowe pia amesema angependa vijana wengi wajitokeze kuwania nafasi hiyo baada ya mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe kutangaza nia ya kugombea uenyekiti huku kukiwa na mjadala kuhusu muda wa miaka takriban 15 ambao mbunge huyo wa Hai amekuwa madarakani.

Mbowe (58) amejikuta katika wakati mgumu katika miaka ya karibuni, akipata changamoto kutoka nje na ndani; biashara na mali zake zikikumbana na mkono wa dola, huku kukiwa na chokochoko kutoka kwa watu ambao hawajajiweka bayana wanaohoji ukomo wa muda wake.

Lakini juzi, Mbowe ambaye ameiongoza Chadema tangu mwaka 2004, hakuonekana kuyumbishwa na hali hiyo.
“Sina shida kabisa kwa wanaojitokeza kugombea, lakini pia ni vema wakajua taratibu za chama zinataka nini mtu anapotaka kugombea nafasi ndani ya chama ikiwemo hiyo ya uenyekiti,” alisema Mbowe katika mahojiano na Mwananchi.

“Kama Chadema, hatupo tayari kuendesha chaguzi zitakazoleta vurugu isipokuwa (zinazoleta) mshikamano na kukifanya chama chetu kiendelee kusonga mbele kama chama kikuu cha upinzani.”
Cecil Mwambe anajua taratibu zote za chama........ Naona kwa mbali mnaanza kutengeneza figisu.

Chadema ni chama kidogo sana hata diwani tu kama mh Jacob wa ubungo anajua taratibu zote za uchaguzi wa Chadema achililia mbali mtu mkubwa kama mbunge na Mwenyekiti wa kanda ya kusini mh Mwambe.

Maendeleo hayana vyama!
 
Halafu kuna watakao amini , na kujaribu kugombea.
 
Kwa muda mrefu sana CCM imeonekana wazi kukosa raha kutokana na mhe. Mbowe kuwa mwenyekiti wa Chadema kiasi cha kujaribu mbinu mbalimbali na vitisho vya kumng'oa. Jambo la kujiuliza ni uenyekiti wa mhe. Mbowe kwanini unawanyima usingizi wanaccm kuliko wanachadema?
 
Wenye Nia njema na nchi wanaona viashiria vyote vya udikteta na usultani ndio maana wanavipinga. Hiyo tabia Mbowe ya kutoheshima ukomo wa madaraka ni sawa? Siku CHADEMA wakishika nchi huoni tabia waliyoilea ndani ya chama itamea kwenye nchi?
 
Back
Top Bottom