Mbowe, nitagombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Mbowe, nitagombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Mwenzio MBOWE hagombei anathibitishwa tu.. Alimuuliza Mchange nimekukosea nini kamanda mpaka unamuunga mkono Zitto kugombea Uenyekiti
Nawewe mkuu!!! mwenyekitu wa ccm taifa ndiyo huthibitishwa tu wala hagombeagi na hakuna uchaguzi wa mwenyekiti ccm taifa, hivi Mwl. Nyerere aligombea na nani kweli; na mpinzani wake alipata kura ngapi? je mshindani wa Mwinyi alikuwa nani? mpinzani wake alipata kura ngapi? je ni nani alisimama na Mkapa kugombea uenyekiti? mpinzani alipata kura ngapi? Shibuda alijaribu tu kusema kuwa atapambana na JK kwenye uenyekiti ccm, yaani hata form tu hakuziona na alishia kufukuzwa chamani; je JPM alisimama kugombea uenyekiti na nani? je mpinzani wake alipata kura ngapi? chezea chichiem yetu wewe!!!

kwahiyo hata Mbowe naye akithibitishwa tu kuwa mwenyekiti anatuiga sisi chama tawala! hivyo tumpongeze tu na siyo kumshutumu.
 
mmmmmmmmh mbowe ukifanikisha ukuta hakika wewe utakuwa zaid ya wahujumu uchumi japo kwa maslahi ya cheo chako itabidi ufanye tu
 
1471421472313.jpg
 
WanaJamvi na Wapenda Demokrasia,

Tusikubali kuingia kwenye mtego wa kututoa katika ajenda ya kupambambna na udikteta kupitia operesheni UKUTA(Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania)

Tutaona kadiri tunapoelekea Septemba Mosi baadhi ya Mijadala ikianzishwa humu kuzua chochoko ndani ya Upinzani

Mfano;Kushambulia Personalty za Viongozi wa Upinzani au kuzusha mijadala inayozua confussion

Huu ni mkakati maalumu unaoratibiwa na Serikali na kwa kushirikiana na Chama Tawala

Hatua hii itaelekea kwenye Vyombo vya Habari kuanzia wiki ijayo

Ben...com on maaan

Kwani mtoa mada kakosea nini?

Hivi kusema nia yake ndio ame ku distract?

Mbowe amechoka...hana ubunifu wowote mpya....tunahitaji akili zingine
 
ww ndo umechoka mkuu na b7 za lumumba.. sisi bado hatujamchoka mbowe.. Lini nyie uvccm mkamtaka mbowe aendelee kuwa mwenyekiti ndani ya chadema? Mbowe ndo kiboko yenu na ataendelea kuwa.. Mpka aseme imetosha na kwa ridhaa yake na si vinginevyo

Aisee....sio kila mtu anayemkosoa Mbowe ni CCM ....Hebu ulizia wenzako humu jukwaani watakueleza kuwa wengine sisi hatujawahi hata kuitamani CCM...Na CHADEMA tupo tangu 1992
 
CHADEMA wangeanza na Kupinga UDIKTETA wa Mbowe kugombea kila wakati Uenyekiti wa Chama ningeona wa maana. Igeni CCM wenzenu wanabadilishana Uongozi
Umesema kugombea? Nilidhani hagombei bali anapitishwa bila kupingwa kama ule utamaduni wetu pale "Yanga"
 
Ben...com on maaan

Kwani mtoa mada kakosea nini?

Hivi kusema nia yake ndio ame ku distract?

Mbowe amechoka...hana ubunifu wowote mpya....tunahitaji akili zingine
Huyo mtoa mada tunamfahamu humu JF, na kwa status yake hayo maneno ni sh.t...labda angetuambia ni c&p from somewhere.
 
Sababu zangu ni zifuatazo

1: Mimi ni mwanachama halali wa CHADEMA

2: Mimi ni mjumbe wa halimashauri kuu ya CHADEMA Taifa

3: Ni kutokana na wewe kushindwa kutimiza baadhi ya maazimio ya kamati kuu

4: Ukishindwa kufanikisha operation UKUTA!!


Ujue utapambana na Mh. Edward Lowassa kwenye kinyanganyiro cha uenyekiti wa CHADEMA. Hutapambana na Mbowe kama unavyodhani.
 
Aisee....sio kila mtu anayemkosoa Mbowe ni CCM ....Hebu ulizia wenzako humu jukwaani watakueleza kuwa wengine sisi hatujawahi hata kuitamani CCM...Na CHADEMA tupo tangu 1992
Acha uongo chadema imeanzishwa 1992 ? usifikiri unachati na watoto wenzio hapa.. kawadanganye lumumba na Act wenzio.. tuachieni chadema yetu
 
Kwanini jamani hakuna MTU mwingine wa kutake over nafasi ya uwenyekiti?? Mbona ni dubwasha/dj mbowe tu ndio anawakalia?? Kweli chadema ni one man show?[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom