Wakuonea huruma ni babaako aliye kuzaa ukiwa na mtindioKwa ku-declare interest, binafsi sijawahi kukubali siasa za huyu mheshimiwa tangu dunia ianze, ila kwa udhaifu wa kibinadamu, kiukweli kabisa ningependa kum-favor na kuona akiachiliwa huru tu!
Naamini amejifunza sana sasa na ataweza kutofautisha kati ya siasa na sheria (ambazo kazitunga mwenyewe). Kujua pia ni ipi kati ya habari 100 za Mange ya kuichukua (Kama ipo).
Naamini pia ataweza kutambua japo kwa kuchelewa kuwa utawala umebadilika kweli na kuona kuwa yeye mwenyewe anatakiwa kubadilika kulingana na hali, maana utawala wa mazowea umepita.
Atatambua kuwa Tanzania kama nchi tulipoamua kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano tulitaka kubadilisha flavour, mambo yasiwe yale yale kila siku eti. Ni bahati nzuri ngalau kwa mara ya kwanza sasa kama nchi tunamaanisha.
Hapa nakumbuka enzi za JK yeye na wenzake walikuwa wanaitisha maandamano kadri wanavyojisikia bila hata kufuata taratibu, watu wanakufa na wengine wanapata vilema vya kudumu, lakini nani alijali? Just the next morning JK anawaita Ikulu kwenda kugonga glass, hapo hapo jioni yake tena wanamtukana matusi yote ndani na nje ya bunge pamoja na kumwita dhaifu. Mwenyewe anacheka tu, hana habari! Sana sana atasafiri siku mbili tatu nje ya nchi kidiplomasia hata kukwepa harufu ya samaki pale Feri.
Walikuwa serikali kivuli na nusu hasa ambapo serikali halisi ilikuwa mbili. Mheshimiwa ana msongo mkubwa wa mawazo kwa mambo mengi ndani ya chama yanavyokwenda hovyo na msongo wa mwili kwa kukaa mahabusu muda mrefu mpaka sasa, obvious, halafu ongeza na la ENL! Karibia kila kitu kimebadilika ndani ya miaka mitatu.
Daah! Binafsi natamani, pengine hata #1 angetamani kuona anatoka. Lakini ndiyo tunafanyaje sasa na nchi yetu ni ya kidemokrasia, tumechagua kufuata utawala wa sheria? Itakavyoamua mahakama ni sawa, ama siyo sawa kwa kukata rufaa, kwao ama kwa serikali. Ni pole tu kwa kweli! Hilo lipo ndani ya uwezo wangu, nalimudu.
Nawasilisha, Tindikali
View attachment 1039905
View attachment 1039907
View attachment 1039816
Kwa ku-declare interest, binafsi sijawahi kukubali siasa za huyu mheshimiwa tangu dunia ianze, ila kwa udhaifu wa kibinadamu, kiukweli kabisa ningependa kum-favor na kuona akiachiliwa huru tu!
Naamini amejifunza sana sasa na ataweza kutofautisha kati ya siasa na sheria (ambazo kazitunga mwenyewe). Kujua pia ni ipi kati ya habari 100 za Mange ya kuichukua (Kama ipo).
Naamini pia ataweza kutambua japo kwa kuchelewa kuwa utawala umebadilika kweli na kuona kuwa yeye mwenyewe anatakiwa kubadilika kulingana na hali, maana utawala wa mazowea umepita.
Atatambua kuwa Tanzania kama nchi tulipoamua kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano tulitaka kubadilisha flavour, mambo yasiwe yale yale kila siku eti. Ni bahati nzuri ngalau kwa mara ya kwanza sasa kama nchi tunamaanisha.
Hapa nakumbuka enzi za JK yeye na wenzake walikuwa wanaitisha maandamano kadri wanavyojisikia bila hata kufuata taratibu, watu wanakufa na wengine wanapata vilema vya kudumu, lakini nani alijali? Just the next morning JK anawaita Ikulu kwenda kugonga glass, hapo hapo jioni yake tena wanamtukana matusi yote ndani na nje ya bunge pamoja na kumwita dhaifu. Mwenyewe anacheka tu, hana habari! Sana sana atasafiri siku mbili tatu nje ya nchi kidiplomasia hata kukwepa harufu ya samaki pale Feri.
Walikuwa serikali kivuli na nusu hasa ambapo serikali halisi ilikuwa mbili. Mheshimiwa ana msongo mkubwa wa mawazo kwa mambo mengi ndani ya chama yanavyokwenda hovyo na msongo wa mwili kwa kukaa mahabusu muda mrefu mpaka sasa, obvious, halafu ongeza na la ENL! Karibia kila kitu kimebadilika ndani ya miaka mitatu.
Daah! Binafsi natamani, pengine hata #1 angetamani kuona anatoka. Lakini ndiyo tunafanyaje sasa na nchi yetu ni ya kidemokrasia, tumechagua kufuata utawala wa sheria? Itakavyoamua mahakama ni sawa, ama siyo sawa kwa kukata rufaa, kwao ama kwa serikali. Ni pole tu kwa kweli! Hilo lipo ndani ya uwezo wangu, nalimudu.
Nawasilisha, Tindikali
View attachment 1039905
View attachment 1039907
View attachment 1039816
Labda nikuulize..taaluma yako ni nini..umesomea sheria au ndio nyie wa division five unajifanya unajua kila kitu..
Sheria zote zilikiukwa kama unavyosema, na walikuwa na haki ya kuandamana.
Je taratibu za maandamano zilifuatwa?