Tayari wajumbe kadhaa wameshawasili wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.
Kikosi kamili cha habari Chadema kitawaletea live coverage kuanzia sasa.
Karibuni
Updates....
Tayari Mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe ameshawasili ukumbini huku akisindikizwa na Katibu Mkuu Dr Vicent Mashinji,Wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi wakuu wa mabaraza ya chama.
Mwenyekiti Mbowe analakiwa kwa bashasha kubwa na wajumbe wa Baraza Kuu huku waandishi wa habari wakiwa wamefurika katika ukumbi huu.
Updates no 2....
Sasa Mwenyekiti Mbowe anatoa hotuba rasmi kuashiria kulifungua Baraza Kuu mjini hapa Dodoma.
Hii ni sehemu ya maneno ya Mwenyekiti Mbowe katika Hotuba yake:
"Ni vema baadhi yetu tuondoke lakini tulikomboe Taifa Hichi chama kupitia baraza hili lazima tutoke na Maamuzi Magumu"
"Tusikimbilie kumtukana anaetuibia, tumemtengenezea utaratibu atuibie alafu tunapiga kelele.
Tunahitaji marekebisho makubwa ya sheria zetu ili kuondoa mianya hii"
""Rais Magufuli awaeleza watanzania ukweli kuwa hata kama kuna hayo mabilioni ...Sisi hatuna haki ya kupata asilimia 4 tu kwa mujibu wa sheria zetu na Mikataba ambayo tumeingia"
"Rais huyu ana historia ya kuvunja sheria na kuliingiza taifa kwenye hasara kubwa .....aliwahi kuagiza kuvunja kituo cha mafuta Mwanza serikali ikalipa mabilioni ...alikamata Meli ya wavuvi tumelipa mabilioni ......Hata hili la Mchanga wa Dhahabu tutalipa mabilioni"
"Rais kafukuza watu 10 elfu kazi kwa kufoji vyeti ...mbona Bashite hajachukuliwa hatua ?"
"Nimalizie kwa kuzungumzia uchaguzi unaotarajia kufanyika nchini Kenya.
Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza taifa hilo.
Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu, rafiki wetu huyu alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu.
Hivyo sisi kama chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Kenyatta na umoja wa vyama vinavyounda 8JUBILEE"
Mwisho:
Mwenyekiti Mbowe amemaliza hotuba huku akishangiliwa kwa mayowe ya furaha na wajumbe wote wa Baraza Kuu huku wakisimama kama ishara ya kuunga mkono hotuba hii.
Wachambuzi wa kisiasa hapa mjini Dodoma waliofuatilia hotuba hii wamesema ni hotuba nzito itakayotikisa anga za kisiasa hapa nchini kwa majuma kadhaa.Huku wengine wakisema huenda tayari CCM inajipanga kutizama namna ya kuijibu hotuba hii ili kupunguza athari kwa chama hicho tawala.
............
Baada ya Hotuba hii ya ufunguzi sasa waandishi wa Habari wanaruhusiwa kuondoka ili kikao cha Baraza kuu kiweze kuendelea na kutoka na maamuzi.
Asanteni sana kutufuatilia.
Molemo wa JF
Dodoma