Kwa sheria zetu hizi za kikoloni ni ngumu sana kufanya hivyo na kufanikiwa!!la muhimu ni Kumshukuru Mungu tu, kwa kurudishiwa uhuru wako!!kwani si ajabu ukaanza mchakato huo ukasikia tena wamerudisha mashitaka yako tena!
Mtu ameshinda kesi mahakamani baada ya kukaaa miaka 10, gerezani na kuonekana hana hatia, lakini hawezi kuishitaki serikali sembuse , mtu aliyeachiwa kwa mamlaka ya DPP?
sheria zetu bado sana, yaani binadamu anakuwa nusu MUNGU.
Hizi za kikoloni Zita backfire, Jedi itafufuliwa, ndio maana Katina mpya inatakiwaSheria haziruhusu?
Sheria za Tz ni za hovyo sn DPP amepewa mamlaka ya kimunguKiukweli ingeleta maana hata kwa hao walioshiriki kukandamiza haki za watu. Maana italeta uelewa hata kwenye kesi zingine kabla ya kushitakiwa au kushitaki wahusika wajue Kuna faini mbele iwapo itagundulika hi kesi ya uongo. Kila mpenda haki ajitokeze kutujuza hasa wanasheria.
Hakuna kiti kama hicho duniani. Kwani alifungwa kimakosa? Hajapewa kifungo chochote. Yeyte atulie tu na shida zake.Wasalaam!
Jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza baada ya serikali kuweka wazi kuwa haito endelea na case ya Mbowe na wenzake ambo walikuwa na tuhuma za ugaidi. Mbowe na wenzake wanayo haki ya kudai fidia au kudai fidia ya gharama za case hiyo iliyochukua siku zaidi ya miambili!
Mh Mbowe amenukuliwa akisema alitamani kuona case hii inaendelea hadi mwisho ili dunia ijue ukweli kuliko ilivyofutwa!
Mbowe na Wenzake wana haki ya kusamehe kama walivyofanya!
Lakini najiuliza ikiwa wakiamua kudai fidia ya gharama za case na muda waliopotezewa bila kusahau madhira waliopata wanayo haki kisheria kudai fidia kwa case iliyoondolewa na wanao shitaki?
Jisomeeni jamani, ili mjue mfumo wa haki ktk nchi! Mahabusu siyo adhabu. Angeomba fidia kama angekuwa amefungwa kimakosa na baadaye kuachiwa.Mimi natamani wafungue kesi ya madi ya gharama za kusi, kuchafuliwa jina na muda waliomzuia gerezani bila hatia
Jibu la swali lako ni kwamba watuhumiwa walioachiwa huru hawana fursa kama hiyo. Mahakama ilitamka kwamba watuhumiwa wana kesi ya kujibu. Hiyo inamaanisha kwamba polisi walipowashika na kuwaweka mahabusu walikuwa na sababu ya kuridhisha kwamba njama za uhalifu zilikuwepo kweli. Hivyo huwezi kuilaumu Serikali kwa kumshika mtuhumiwa baada ya kujiridhisha kwamba kuna uhalifu unaobuniwa kufanywa. Kwamba DPP ameamua kutoendelea na kesi ni jambo jingine kabisa.Wasalaam!