kigogo warioba
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 6,048
- 9,405
ha ha haaa.. Nyie watu siwawezi!Mbowe ndo kiboko ya CCM hata akila yote amna shida......Mboja Jiwe anahonga mahawara sio rudhuku tu, anahonga paka wilaya[emoji23][emoji23], Bado hajahonga nchi nzima kwa ma hawara zake.
Mkuu safi sana. Hawa jamaa wanadhani kila mtu ni mjinga. Kwa kuongezea tu, hivi utafiti gani usio na hata mchanganuo? Kwanza watuambie hao wafanyakazi 70 wanalipwa kiasi gani kila mmoja (ingawa hana uhakika kama ni 60 au 70) ili tujue gharama kwa ujumla. Ofisi za kanda zinapewa kiasi gani. Hizo chaguzi anazozipigia mahesabu zinafanyikaga kila mwezi? Kwanini wanazihesabia kama vile ni matumizi ya kila mwezi. Mwisho, yaani hata CAG aliekagua mahesabu yao akakuta kuna ubadhirifu nae ni mjinga pia.Hahahaaa huu utafiti kiboko hako ka ofisi hapo ndio kana wafanyakazi 60 hadi 70?? Kwa kazi zipi?? Na wanajibanza wapi hapo au kule uwani maana vyumba vya hiyo guest sidhani kama vina accommodate watu wote hao...halafu ma.signatories wenu hapo si wawili wanaruhusiwa yan Mugabe taifa na katibu mkuu..sasa hapo kuna swali?? Halafu taja ofisi zenu zinazopokea ruzuku za kuendeshea ofisi hapa zitaje....hahahaa yajayo yanafurahisha
mabilion gani wewe? Hivi katika ukaguzi uliopita cag si kaonyesha ccm ndio imepiga zaidi tena ni zaidi ya bil 11, hebu niambie ni chama kipi kimeifikia ccm ?Hivi inakuwaje hujaelewa kamanda...hivi unataka nirudie maelezo yoooote...hahahah..naomba kamuulize CAG yale mabilioni yaliyofisadiwa aliyatoa wapi...mueleze pamoja na utaratibu wako wa ruzuku huu unaousema
Kaka hakuna mchanganuo hapo ni porojo tu. Mchanganuo gani haulezi hata ni kiasi gani wafanyakazi 60 hadi 70 wanalipwa.safi kwa mchanganuo! Upande ule nao waweke mchanganuo wa drimulaina na vingine!
Hivi wewe hujasoma ripoti ya CAG au? Ndo maana wenzio wanang'ang'ana na ile 1.5 trillion ili madudu yao yasiongelewe. Lakini CAG kafichua kila kitu. Ufisadi mkubwa CDM kwenye fedha za ruzuku.Nisingependamaneno hayo yatoke lumumba kwani ni kama kuitukana serekali yetu kuwa hawana vyombo vya kichunguzi miaka yote anapokula hizo ruzuku ambazo ni kodi zetu.
CAG naye hajui kitu hadi lumumba wamshitaki Mbowe?? Poleni. Nadhani tutafute tuhuma zingine zenye mashiko sio hizi
Ofisini za raisi ziko Kila mkoa Na ikulu ndogo ziko Kila mkoa.Ofisi za makao makuu chadema ziko Kila mkoa?Nenda
Kaulize ikulu ina wafanyakazi wangapi ndio utajua kama wengine wananing'inia kwenye mapangaboi au kwenye swichi za umeme
1.5 Trillion unasemaje ngojera?! Kweli ccm hamna uchungu na nchi hiiHizi ngonjera kama ngonjera nyingine mzee...hoja za kisanii za kujaribu kukwepa hoja makini na zinazochoma kumoyoo
Tuleteeni mchanganuo wa 1.5 ilivyotumikaTuwwkeeni hapa mchanganuo wote wa matumizi ya ruzuku kila mwezi tujiridhishe kama kweli pesa zimetumika vizuri ........
Hapa kamanda unapigia mbuzi gitaa..hivi unawezaje kumtenganisha Mbowe na chadema..chama cha baba mkwe...??? Mtei mwenye chama amesisitiza mkwe wake aendelee kusimamia chama vizuri asisikilize maneno ya watu..aendelee kupigania demokrasia..hahahaha...chama kinaonekana kama kitega uchumi cha Mtei eti...nahisi tu..na wengine wanafuatia kwa nyuma..sasa utawapigaje chiniKwenye management kujua mtu mwizi ofisini ni rahisi njia moja kumjua ni kungangania ofisi.Haendi hata likizo ili mwingine ashike Na mchoyo kufundisha wengine kazi aliyonayo ili aendelee kuonekana yeye ndie anajua!! Mbowe ana dalili zote za mwizi yeye ndie star chadema hataki kuondoka anataka kuatamia madudu yake anajua akija mwingine atayafukunua Na yeye aweza ishia jela.Miaka 20 Na zaidi aliyokaa yatosha chadema mfungasheni virago aingie mwingine Ruzuku hata Mimi pesa yangu ya Kodi imo kwenye ruzuku ya chadema ndio maana Nina hoji napendab kuwaambia chadema Mbowe apishe mtu mwingine.Wezi wa Ruzuku Na Mbowe wanataka kuendelea kuatamia madudu yao ya ulaji wa ruzuku Na fedha za wafadhili.Anataka kuatamia madudu yeye Na genge lake.Chadema nawashauri ipigeni chini kamati kuu yote wekeni wapya Na kurugenzi zote za chadema wekeni wapya
Hivi wewe hujasoma ripoti ya CAG au? Ndo maana wenzio wanang'ang'ana na ile 1.5 trillion ili madudu yao yasiongelewe. Lakini CAG kafichua kila kitu. Ufisadi mkubwa CDM kwenye fedha za ruzuku.
Una mtindio wa ubongo bila shaka.Blah blah blah, tunataka fedha zetu, Mbowe rudisha fedha zetu!
Wambea mna mahangaiko yasiyokoma.mmekuwa waganga wapiga ramli.Hahahaha ubwabwa mtupu..wewe umetuandikia utaratibu wa kawaida wa kifedha ambao kila chama kuwa kinatakiwa kiufuate kisheria...kwani unadhani sehemu zote ambazo ulaji unatokea huwa hakuna utaratibu wa kifedha..? Je umeshaona kuna sehemu yoyote ambayo mlaji anawekewa hela mijakwamoja kwenye akaunti...???? Usitudanganye kamanda hapa...pesa inaliwaga kwa kutumia taratibu hizo hizo unazosema..kunakuwa na aidha malipo hewa ambayo hayana ushahidi, ama kuongeza bei katika huduma mbalimbali zinazotolewa kwa chama, kuobgeza bei kwenye manunuzi mbalimbali na hapa ndipo pesa inapigwa sana..na ndio maana msema kweli anakuwa CAG..Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambaye ana vigezo vya kuweza kugundua pesa kiasi gani ambayo imepigwa..na ndio maana CAG alugundua ufisadi mkubwa ndani ya chama wa mabilioni...hivi unadhani hili alikaa na kubuni mahesabu au...????????be careful usidanganye umma kamanda..kuwa mzalendo
Haya tukubali wananchi wanatuhumu...lakini hata CAG naye anatuhumu kamanda....?????? Hata wale wabunge wanotoka chadema nao unawaweka kundi lipi ...la CAG au la wale wanaotuhumu tuu...?
blabla tunataka nyumba zetu zilizouzwa kwa vimada.bila kusahau 1,5 trilion zetuBlah blah blah, tunataka fedha zetu, Mbowe rudisha fedha zetu!
ulishawahi ona simba ikichagulia kocha yanga!? punga wewe! madudu yapo kwenye ripoti ya Bashir mbona huzungumzii? bwabwa kabisa wewe! kutwa kucha mbowe akakuoe basiMleta mada mwongo kwanza hajui idadi ya wafanyakazi wa makao makuu anasema wako kati ya 60 au 70!!!!! halafu wote tunajua ofisi ya makao makuu ya chadema pale waweza kaa ofisini watu 60 au 70 kwenye kale kajumba ? Uongo mtupu.Aweke majina ya hao wafanyakazi Na kazi zao.Kile kiofisi huwezi weka wafanyakazi 60 au 70.uongo.Wezi wa ruzuku nyie.M Mbowe akiondoka madudu mengi yatagundulika
OK! HIyo ni nadhalia ya matuizi. Tuelezee uhalisia wake uko vipi? Mashtaka ya hao jamaa wanaohama kila kuchao, ilikuwa ni uhalisia wa matumizi, siyo nadhalia hii uliyoweka hapa. Hebu sikiliza tena clip hii:Kumekuwa na maneno mengi na tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe kuwa anatafuna pesa za Ruzuku za chama,
Tuhuma hizo zimekuwa zikiendelea kila mara na sasa zikichagizwa zaidi na wanaohama kutoka Chadema kwenda kwenye vyama vingine hususani Ccm,
Yafuatayo ni matokeo ya Utafiti;
*NAMNA FEDHA INAVYOTOKA SERIKALINI MPAKA KUFIKA KWENYE AKAUNTI YA CHADEMA*
Serikali hutoa ruzuku kwa Chadema kila mwezi,
Fedha ikitoka Hazina (Serikalini) hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,
Msajili huiingiza pesa hiyo kwenye Akaunti ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (Board of Trustee Bank Account),
Bodi ya Wadhamini wa Chadema ndio hupeleka pesa hiyo kwenye Akaunti ya Chama tayari kwa matumizi. Pesa haiingizwi kwenye Akaunti binafsi ya kiongozi yeyote wa Chadema wala mwanachama wa Chadema. Huingizwa kwenye akaunti ya chama,
*NAMNA PESA INAVYOTOKA KWENYE AKAUNTI YA CHADEMA*
Wapo Watia Saini Wanne (4 Signatories) kwenye Akaunti ya Chadema Taifa. Ambapo watu wawili kati ya hao Wanne wanaruhusiwa kusaini Hundi (cheque) kwa ajili ya kufanya Malipo,
Watu hao kwa nafasi zao ni;
i) Mwenyekiti wa Chadema Taifa
ii) Katibu Mkuu wa Chadema Taifa
iii) Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara
iv) Mkurugenzi wa Fedha
Pesa yoyote haiwezi kutoka kwenye Akaunti ya Chadema mpaka Wawili kati ya hao wanne Watie Saini,
*WAKATI GANI PESA INATOKA KWENYE AKAUNTI*
Pesa yeyote ya Chadema haiwezi kutoka kwenye akaunti kama haijathibitishwa na Kamati Kuu,
Kamati Kuu ya Chadema tayari ilishaidhinisha matumizi ya kila mwezi ya chama (Normal Operation expenditures),
Lakini kama kuna matumizi mengine ya ziada ama dharura (mfano Uchaguzi wa marudio, kesi, matibabu), lazima Kamati Kuu ya Chadema ikae, ipime umuhimu wa kufanya matumizi ndio iidhinishe au ikatae matumizi hayo,
Sio Mbowe aidhinishe, sio Mashinji aidhinishe wala yeyote yule. Ni Kamati Kuu.
*CHADEMA INAPELEKA WAPI FEDHA YA RUZUKU WANAZOPATA KILA MWEZI*
i) Zipo fedha ambazo hutumika Makao Makuu kulipa Mishahara na Posho,
Chadema inao wafanyakazi kati ya 60 hadi 70 ambao wapo Makao Makuu ama hulipwa moja kwa moja toka Makao Makuu kuanzia nafasi za Wahudumu wa ofisi, Walinzi mpaka Mwenyekiti wa Taifa,
Mwenyekiti wa Taifa na wafanyakazi wengine walioko Makao Makuu ambao ni wanufaika wa Serikali (yaani wanaolipwa mishahara kutoka Serikalini), hawalipwi mishahara na Chadema,
Freeman Mbowe _(Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Hai)_, John Mnyika _(Naibu Katibu Mkuu - Bara na Mbunge wa Kibamba)_, hawa wawili ni mfano wa wasiolipwa mishahara kwa sababu ni wanufaika wa Serikali. Badala yake hulipwa posho pale wanapotumwa na chama kwenda kufanya shughuli maalum mikoani au nje ya nchi,
ii) Fedha nyingine hupelekwa kwenye Ofisi 10 za Kanda (Kanda Mbili zipo Tanzania Visiwani na Kanda 8 zipo Tanzania Bara)
Fedha hizo kwenye Kanda hutumika kulipa Mishahara ya Wafanyakazi, Posho na Ruzuku kwenye Majimbo yote 264 ya Uchaguzi,
iii) Kuna fedha hutumika kushughulikia kesi mbalimbali za Viongozi na Wanachama wa Chadema. Fedha hizo hutumika kuwasafirisha Mawakili na kuwalipa Posho.
iv) Matumizi ya dharura ambayo hayaepukiki. Mfano Chaguzi za Marudio za Ubunge (ambazo hugharimu kati ya Milioni 100 hadi 120), chaguzi za Madiwani, gharama za Matibabu na Vifaa vya Uenezi wa Chama.
Kwa kuangali mchanganuo huo hapo juu, utaona kabisa Ruzuku ya Milioni 236 wanayopata Chadema kwa mwezi, haitoshi kwa matumizi yote ya Chama kwa mwezi.
Kitendo cha kumtuhumu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ama kiongozi mwingine yeyote kuwa anakula fedha za Ruzuku, itabaki kuwa ni propaganda za kisiasa ambazo hazina ukweli wowote,
Na ikumbukwe, hakuna kiongozi yeyote anayeweza kutoa pesa ya ruzuku kutoka kwenye akaunti ya chama mpaka watia saini wawili wasaini hundi ndipo pesa itoke,
Mbowe anakulaje fedha ya ruzuku ya chama???
*Utafiti hupingwa kwa Utafiti. Nasubiri utafiti utakaoupinga utafiti huu.*
Asanteni