Mh.Slaa, salaam:
Nakushukuru sana kwa majibu yako ya kistaarabu yaliyojaa hekima iliyotukuka. Natamani na wafuasi wako humu watakuwa wamejifunza toka kwako namna ya kutoa au kuchangia mada kwa lugha za kistaarabu zisizo na matusi na kashfa.
Salimia,...
"ushabiki wa kufumba macho na kusema ndio kwa kila kitu kinacho husu chadema" wa baadhi ya wana JF hapa ni utumwa mkubwa sana ambao inabidi kuuepuka!
Huu unaoitwa "uanachama damu,chadema damu,ccm damu" ni utumwa wa ajabu maana una kuzuia hata kuuliza kitu pale unapo ona hakiendi vyema!
Haiwezekani mtu tunaetaka awe raisi mkatae asikosolewe,asiulizwe,nk .
Matokeo yake ni kwamba akiwa raisi mkamchora katuni gazetini kosa
Mkiuliza kitu kwa mda huyo yuko raisi,kosa na mengine kama hayo!
Kama tunataka mabadiliko chini ya raisi bora,then acheni azoee maswali,kejeli,utani,katuni kila kitu otherwise mmmmmh
Haya yote yanatokea kwa sababu taarifa zinatolewa juu juu tu na sio officially e.g wangeweza kutoa taarifa zao kama hizo,updates kwamba viongozi wa chadema wameenda kwenye mkutano,maelezo yote mkutano una husu nini nk
Ukiangalia website yao
Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakuna taarifa inayo ongelea chochote kuhusu mkutano huo au safai,nini maana ya kuwa na website sasa fasheni au?
Wachangiaji wanasema usichangie kama hauna uhakika,uhakika au taarifa za kuondo mkanganyiko zinatoka wapi kama sio kwenye website yao?
Au tusikilize radio uhuru ndo tutazipata?
Kuna haja ya kua tofauti na sisiem kwa kila kitu,chadema kiwe chama cha kisasa kwa kila kitu