Mbowe na Dr Slaa, natoa saa 24!

Mbowe na Dr Slaa, natoa saa 24!

Status
Not open for further replies.

sixgates

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Posts
3,979
Reaction score
1,667
Najiuliza tu, hivi hiki chama chetu si kina mwenyekiti, na katibu? Haiingii akilini Zitto naibu katibu anashambuliwa na Lema na baadhi ya wanaoitwa makada wa chadema then mwenyekiti na katibu hawasemi lolote. Hivi angekuwa amesemwa John Mnyika, Josephine Mushumbusi ama Slaa si matamko yangetolewa? Mungekaa Kimya?

Binafsi nina matatizo na mwenendo wa Zitto, lakini katika hali ya kawaida uongozi wa chadema mmechemsha, badala ya kujibu hoja mnaleta risiti zinazomhusu Zitto sasa hizo risiti tuzifanyeje?

Ninachotaka kuona ni maamuzi yasiyo na double standard. Yaani hiki chama kimekuwa cha ajabu sana yani kwa mfano wapo vijana kama Yericko Nyerere anatoa matamko utafikiri chadema ni chama cha shangazi yake (naongea kama wanachama wanavyosema huku mitaani) na haoni madhara ya anayoyaandika humu.

Natoa saa 24 Mbowe na Dr Slaa najua mtasoma hii post, mchukue hatua na kuhakikisha Zitto hashambuliwi katika taratibu zisizo sahihi, laa sivyo nitaungana na wanachama wa kanda yangu tutatoa tamko latakalofuatiwa na kujitoa katika shughuli zote za kichama. Tunaweza!

More updates
---------------------
______________-

Sasa hivi ni saa sita mchana..Mpaka sasa yamebaki Masaa Tisa. Bado nasubiri kusikia Tamko la Mwenyekiti wa chama, ama Katibu... Laa sivyo tutachukua maamuzi magumu.

_____________
_____________

Sasahivi ni saa kumi na moja Jioni. Bado msimamo wangu upo pale pale.. Kama Dr.W.Slaa unapitia huu uzi usiupuuze njoo uje utoe kauli yako.
 
Last edited by a moderator:
Naunga mkono hoja yako mkuu....binafsi sio mshabiki wa Zitto lkn kwa hili linaloendelezwa na mh.Lema nadhani limevuka mipaka,Zitto ni Naibu Katibu wa Chama,anastahili heshima na sio dharau anayoonyesha Lema,ukimya wa Mbowe na Slaa unanifanya niamini kuwa kuna tatizo juu yao na Zitto.

Namsihi Lema aache kujifikiria kama gwiji wa SIASA za Arusha,aache kudhani kuwa kupendwa kwake arusha kunampa kiburi cha kumnanga kiongozi wake,kama kuna shida kwanini wasizungumzie ndani ya chama...

CHADEMA ACHENI KUTUCHEFUA,TUNAWAAMINI,TUNAWASAPOTI KATIKA MAGUMU MNAYOPITIA LAKINI SIO HILI MNALOJITAKIA.
 
Natoa saa 24 Mbowe na Dr Slaa najua mtasoma hii post, mchukue hatua na kuhakikisha Zitto hashambuliwi katika taratibu zisizo sahihi, laa sivyo nitaungana na wanachama wa kanda yangu tutatoa tamko latakalofuatiwa na kujitoa katika shughuli zote za kichama. Tunaweza!

mbona umechelewa?we chapa mwendo kwani daradara haitishiwi abiria.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
sifongo

Ni kweli kabisa, hawa watu wa chadema inaonesha wameshiba ruzuku zinazotokana na kodi tunazokatwa kwenye mishahara yetu na biashara zetu wanaanza kutunishiana misuli. Tusiruhusu
 
Last edited by a moderator:
Chadema ni kama gari lisilo na dereva

Linakwenda kwenda tu...
 
Halafu wewe ni nani mpaka utoe saa 24....Hujui makao makuu ya chama uende huko ukatoe hilo dukuduku lako...?
 
Mleta mada hujawa objective. Ningekuona una maana sana kama ungejaribu kuleta bandiko ukifocus kwenye reality. Unaposema Lema amemkosea naibu katibu mkuu bila kusema naibu katibu mkuu amewakosea wanachama wengine akiwamo Lema unaondoa kabisa maana nzuri uliyokusudia kwenye andishi lako hili.

Binafsi tangu mwanzo sijawahi na sitawahi kuja kuunga mkono malumbano ya kipuuzi ya namna hii. Kinachoumia ni chama. Chama hiki kuna watu wamekifia, kuna watu wamekaa rumande/gerezani kwa chama hiki. Kuna watu wametoa fedha zao halali kwa ajili ya chama hiki. Kujivua nguo hadharani kwa style ile ni kudemoralize nguvu kubwa ya sisi tilio baki. Ni ku water down nguvu ya damu iliyomwagika kwa kukipigania chama.

Mshindi katika vita hii atakuwa mi CCM. Chama ambacho wengine hatutaki hata kukisikia japo kwa sekunde hata moja.

Kwa ufupi Zitto na Lema wana 'dhambi' zinazofanana.

Nimefarijika baada ya kuambiwa Uongozi wa juu umeingilia kati. Nadhani hata Yericko Nyerere atakuwa ametaarifiwa aache mpango wake alionao.
 
Last edited by a moderator:
Najiuliza tu, hivi hiki chama chetu si kina mwenyekiti, na katibu? Haiingii akilini Zitto naibu katibu anashambuliwa na Lema na baadhi ya wanaoitwa makada wa chadema then mwenyekiti na katibu hawasemi lolote. Hivi angekuwa amesemwa John Mnyika, josephine mshumbusi ama Slaa si matamko yangetolewa?, mungekaa Kimya.
Kwa hiyo wewe msemaji wa ZITTO? Amesemwa ZITTO umechukia... Angesemwa John Mnyika, josephine mshumbusi ama Slaa ungeleta utumbo huu?
 
Tunaenda kulekule unakolalamikia. Hapa ni makao makuu ya Chadema? Umewapigia simu

In short nimempigia simu Mnyika na kasema atahakikisha anacontrol situation, Zitto hapokei simu. Dr Slaa na Mbowe sijazoeana nao.
 
Naunga mkono hoja yako mkuu....binafsi sio mshabiki wa Zitto lkn kwa hili linaloendelezwa na mh.Lema nadhani limevuka mipaka,Zitto ni Naibu Katibu wa Chama,anastahili heshima na sio dharau anayoonyesha Lema,ukimya wa Mbowe na Slaa unanifanya niamini kuwa kuna tatizo juu yao na Zitto.

hapo kwenye bold....Nilikuwa sifahamu kumbe Lema kusema ukweli mchungu ni dharau...Maajabu haya..
 
Chadema ni kama gari lisilo na dereva

Linakwenda kwenda tu...

khaaaaaaa be ndauli ...leo bungeni pameulizwa sawli tufate ya nani ....katibu mkuu wizara ya ellimu kaondoa sifuri waziri amasema bungeni sifuri ipo pale pale wachana na hii ya chadema watamaliza wenyewe........
 
mbona umechelewa?we chapa mwendo kwani daradara haitishiwi abiria.

Mkuu tatizo nalipa kodi na ruzuku zinaenda kwene hiki chama so usifikiri ntaacha kukikemea
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom