Mbowe, Mwanya huo Utumie Vyema Sasa

Mbowe, Mwanya huo Utumie Vyema Sasa

Obfuscation or obsession...have your pick son.

Nimeileta huku knowing that small minds ni wengi, jukwaa la kwanza nilipo I post wengi ni akili kubwa, hao tunaenda sawa , huku wengi bado wanaelea tu
 
Umetoa ushauri wako na wanaokujibiu wana haki ya kukujibu wapendavyo au wafikiriavyo. Mawazo au maoni yako yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Kama ulivyokwisha sema siasa ni mchezo mchafu na kila mtu anachanga karata zake ili aweze kushinda. Yaliyotokea nyuma yametokea na ni kwa maslahi ya vyama husika na watakuwa wamenufaika kiasi chao.
Hili la Rasimu limekuja na mvuto wa aina yake na bahati nzuri wachezaji ni wale wale. Walichofanya CCM vyama vingine hawakuridhika hata kama wana mshikamano na CCM. Kama wana nia za dhati kuwatetea wananchi watajitoa mhanga mpaka kieleweke! Sasa kikeshaeleweka kwa nini CDM iwatose? Hili gurudumu n letu sote tunatakiwa tulibiringishe hadi kileleni CCM wamshindwa UKAWA umejitokeza kujitosa kulipokea hilo gurudumu.
Kama ulivyoasa sio lelemama kuitoa CCM madarakani na wao wanatumia kila njia kurubuni wengine tatizo ni kwamba lengo lao limehamakuwatetea wananchi wanataka katiba ya kuwatetea wao viongozi wa CCM hata wakitoka madarakani wasiguswe! Kwa mwananchi anayejua haki ni nini hawezi kukubali huo mchezo mchafu. Kila MTZ lazima awajibishwe hapa nchini kwa mema au mabaya aliyoyatenda akiwa raia au kiongozi.

IDUMU RASIMU YA WARIOBA!
 
Pembe, ahsante sana kwa mchango wako, nakubaliana na wewe kwa Uchambuzi wako kwa namna moja.

Napinga vikali wachangiaji wanaochangia nje ya hoja Bali kwa hisia binafsi na Ushabiki kitu ambacho binafsi sikiabudu kamwe!!!

Lakini hata Kama mtu atakuwa na Ushabiki basi usiwe wa Mawazo mgando, hakuna anayefurahia hari ya nchi ilivyo kwa sasa na ktk safari hii tuliyonayo, Kama hatutakubali Changamoto za mawazo na kuzifanya kuwa fursa, hatutafika.

3,3,3,3,3
 
"It is better to be a human being dissatisfied than being a pig satisfied" ngoja niendelee kusoma comments za with.
 
"It is better to be a human being dissatisfied than being a pig satisfied" ngoja niendelee kusoma comments za with.

John Stuart Mill alikuwa sawa sana kusema hivyo, na zaidi aliongezea " non of us is infallible, the opinion we disagree may be true, we need to test the truth no matter how widely held"....bado watu wana Mawazo mgando ya enzi za kina Plato za kuamini kuwa hakuna mtu wa kuweza ku achieve knowledge of the truth isipokuwa philosopher kings pekee....to suppress an opinion is to rob human race..
 
Ninaiona hoja yako kwa uzito wake

Morally is wrong to use people as mean to an end, as far as human dignity is concerned na hii iko wazi sana kwa kila mtu na kwa hari ya kawaida wengi Mtazamo wangu kwa hari ya kawaida( hari ya kibinadamu) sio mzuri kuufuata Bali ni wa kukemea, lakini politically ,wazo langu kwa Mbowe kulifuata ni sahihi kabisa( kisiasa). Kama nukuu moja wapo ya Machiaveli inasema " the end justify the mean"

Bandiko langu ni kutahadharisha tu kuwa ground ya Siasa haikutokea ktk kanuni za ki maadiri, Bali sisi ndio tunafanya na tunajitahidi sana kuweka pamoja maadiri na siasa, ni kweli vinaweza kukaa kwa kiasi furani lakini pia vinaweza visikae pamoja kwa kiasi kikubwa.

Mifano ni sera ktk kampeni na Maneno Mazuri ili kushawishi kura za wananchi, hapa tukio la kushawishi wananchi ni sawa na kuwatumia as a mean to an end ambayo ni ushindi , according to Kanti's Moral theory this is wrong. Na haina tofauti na Ushauri wangu kwa Mbowe

Sasa inakuja kitu kimoja kwamba, Kama tunaingia ktk siasa, kuna mipaka ya kuaminiana, na maadiri yana nafasi ndogo sana( si Rahisi kujua), hivyo Kama mwanasiasa unajua jinsi gani huwa una CHEZA na Maneno kupata kura, juwa kabisa hata wenzio huwa wanafanya hivyo sasa SUALA la kutiliana mashaka ( mwanasiasa mahili) hutakiwi kulitupa kapuni, ni lazima uwe tayari kwa lolote lile na uweke mazingira ya kuzuia na pia at any time lazima ujue kuwa hata wenzio wako hivyo hivyo Kama wewe na Kama kila mtu atakuwa ktk hari Kama hiyo, basi hapa kunafungua mwanya wa Timing as to an end ambapo ukitumia vyema unafupisha safari ndefu

Concept ni ndogo sana iliyopo, lakini nimezunguka sana kufafanua kutoa mwanya wa mtu kuwa na Thought experiment..

Ukiwaza vizuri utaelewa nini Namaanisha
 
Huyu jamaa ni muandishi mzuri nimesoma alichoandika bila kuchoka. Ukawa ni urafiki wa mashaka kila mtu ana malengo yake, wanatumiana. Chadema haiwezi kuwa mkombozi wa nchi hii kwa sura yake ya sasa. Rangi ya chadema ya ubaguzi ni lazima ijitakase nayo kwanza. Huwezi kutaka kuigawa nchi vipande vipande kwa misingi ya ubaguzi ubaki salama. Mbowe hana uwezo wa kuwafanyia ujanja wowote kina Jussa.
 
Back
Top Bottom