Mbowe, Mwanya huo Utumie Vyema Sasa

Mbowe, Mwanya huo Utumie Vyema Sasa

maguzu masese

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
283
Reaction score
141
10 October 2001, kulifanyika muafaka baina ya CCM na CUF, nakutiwa saini na Philip Japhet Mangula, na Seif Sharif Hamad, na kushuhudiwa na Kingunge Ngombale-Mwiru, Ali Haji Pandu, Mohamed Aboud Moham na Hamad Rashid Mohammed. Mbele ya: Benjamin William Mkapa Ibrahim Haruna Lipumba na Amani Abeid Amani Karume. Moja ya malengo: Kuimarisha mazingira ya maelewano na kuaminiana
Angalia hii orodha, ni ya watu wa aina gani Kirahisi rahisi tu eti leo kweli hawako pamoja, Kingunge ninayemsikia ( nakujifanya namjua), Mkapa ( huyu jamaa tunamchukulia poa sana) Kiukweli tu Lipumba mi hata simzimii kabisa ( kibinadamu sina sababu ya msingi basi tu nimeamua hivyo, nim kama vile Masha mwaka 2010) Kisiasa sioni anachokifanya chenye manufaa kwa taifa hili Zaidi ya asili ya mwanadam ‘selfishness’, CV yake ya kuhama madarasa ndio inampa jianbut sio Kiongozi , any way inferiority complex ni kubwa sana miongoni mwa watanzania , Hata mimi niliyemaliza Form IV ya zamani ( kabla ya division 5) nahisi namzidi mbali sana na hata tukifanya mjadala nitamshinda vizuri tu hili halina ubishi.
Hamadi ( inasemekana ) kuwa anahusika na ADC, So to speak, ni kama ilikuja kwa nia ya kuweka upinzani CDM ( hoja Hii nitaitetea). Mbowe umesahau kuwa kipindi frani kadi za CDM zilikuwa zinachapishwa nchi ya Jirani na zinatumika kwa propaganda? Nadhani hadi sasa bado zinaendelea!!


September28,2012 moja ya vichwa vya habari ni ‘’ CUF yaisaidia CCM kushinda Umeya Mwanza’’ Turufu ya nani anakuwa Meya wa Jiji ilikuwa mikononi mwa CUF ambao walikuwa na wajumbe wawili ndani ya baraza hilo, ambapo ilikuwa wakiamua kuunga mkono upande wowote huo ndio ungeibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho’’ Hatimaye leo Ndg, Mabula ni Meya wa jiji, kwani hata miaka miwili bado haijatimia. Brother hii pia umesahau?


January 4, 2012 Moja ya vichwa vya habari ‘’HAMADI RASHIDI AFUKUZWA ( huyu kumbuka alikuwa moja wa shuhuda wa makubaliano) nab ado siri ya makubaliano anayo. Hii ndio sababu imekufanya leo uone CUF ni washkaji ? anyway hii acha tuipotezee kiaina lakini kwani Kwani ‘’ Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV’’ kipindi kile ulikuwa na sura gani hasa ama mimi ndio mjinga ( mtu asiyekuwa na uelewa juu ya mambo.) na niliendelea kuwa mjinga kabla na baada ya mdahalo ( Nakumbuka hapa kulikuwa na burudani ya aina yake- Mbowe nilikukubali sana kamanda) Tukiachilia mbali Seif Sharif Hamad na cheo chake baada ya Makubaliano


Juzi tu, hata siku mwaka mmoja haujaisha CUF ilifahamika kama ‘ CCM B’, wameolewa na CCM etc , ni lini hiyo ndoa ilivunjika ama hiyo herufi B ilifutika? Vipi Kama ilikuwa ni ya kikristo? Kampeni za Mbatia Kawe ilikuwaje kwani? Baadaye si alienda mahakamani ? Na si ndio CCM wamempa pa kujishikiza naye for the mean time? Na huyu si tulikuwa na mashaka naye juzi juzi tu baada ya kupewa ubunge? Na si tulisahau yote baada ya kusanua issue ya Mtaala wa elimu , so does it mean hii tukio moja tu ndio kawa mshkaji eti? Huyu si aliwahi kuwa na jamaa yake enzi zile baadaye ikatokea TLP ambapo Lema alianzia kutokea huko, na ja,maaa mmoja namkubali sana kamanda Alphonce Mawazo pia alianzia huko, Hawa vijana Wawili wakamkimbia Mrema maana alikuwa ni pandikizi na leo hii kazi wanayo ifanya inaonekana, does it mean wewe leo hii unataka MABELE na MBATIA wapige kazi pamoja eti? Je tofati zao za zamani zimeisha eti? Au bado unasimamia ule msemo wa kushusha mioyo ya matumanini ya wapiga kura na kuwafanya waamini kuwa siasa ni mchezo mchafu ‘’ kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu’’ All in all my point is


Kama mimi ningekuwa WEWE ( kama vipi niachie kwa muda tu), baada ya hili la kujiunga nao kwa sasa baadaye lazima NINGEWAPIGA CHINI, na hata moja ya sababu ambazo zingenifanya niungane nao ni hii ya kwamba niwavutie MWANYA kisha INAKULA KWAO, ( Hapa ndio siasa inakuwaga tamu sana), ningecheza na kufunga Kama Maradona katika mechi ya robo fainali ya kombe la dunia kati ya Argentina na England ,22 June 1986 (One of the most famous goal in football history) na hapa lazima ningejipatia ujiko kinoma maana sasa ningeanza kuwatumikia wananchi ile kwa kwenda mbele kisha nawakumbushia kale ka msemo ketu ‘’ kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu’’.YOU SEE


Iko hivi, hawa washkaji UKIZUBAA wanakupiga chini, na kwenye ramani ya siasa ndio inakuwa KWAHERI mimi ninsingekubali ujinga huu, maana CDM ilipofikia kwa sasa, NCCR, CUF hazikuwahi kufikia. Obvious hawa washkaji kuwa na wewe inawezekana ni moja ya strategies za CCM ili baadaye ile kwako. Hata mimi ndio ningekuwa Strategist wa CCM hapa ningecheza hivi na NINGEKUPIGA kirahisi sana ( hapa kuna njia Zaidi yah ii), sema CCM hawezi na pia hawajui maana hii ni mbinu ni advanced sana kwao hivyo sio size yao hao kina lowasa na kinana ni STANDARD LEVEL tu. Nape wala usimhesabu sema tu yuko juu maana hana mpinzani ktk nafasi yake, Mnyika anapwaya hachezi ipasavyo, nadhani ifikie kipindi sasa hii nafasi mpe mtu aliye nje na huru na majukumu ya bunge( I can defend my argument) Nape angekuwa Chadema angekuwa mzuri sana, hii ndio maana ya Siasa za upinzani……jaribu kunielewa….


Lazima tukubali kuwa CCM wana watu ambao ni strategies wazuri sana ( Kinana na lowasa) na wengine wengi, sema tu upepo wa wananchi umewakataa na kuegemea kwetu hivyo hii ni nafasi ya pekee kuhakikisha kombe tunabeba, ambapo pia kwa hari ya kawaida tu hata kama mimi ningekuwa Ni Kikwete ama kiongozi wa CCM kukupa nchi kirahisi rahisi tu hivi katika democrasia ya herufi ndogo ni impossible, ningekupa nchi pale tu nikiona kweli umepambana vya kutosha na sina jinsi kunusuru hari ya usalama but kwa sasa kuna jinsi ya kufanya na Nchi lazima tunabeba hii haina ubishi kamanda.


Kama mimi ningekuwa wewe, hawa washkaji ningeungana nao kwa nia ya kudai TANGANYIKA TU, kisha nawatosa, kama wanataka kuungana na mimi basi wavue jezi za vyama vyao, wavae ya kwangu kasha twende sawa, wakivaa jezi yangu tunaungana tunasakata kabumbu safi sasa. Lakini bila hivyo hawa washkaji wakisha saidia kuleta Tanganyika tu tunawafanya maaduni maana hata sasa hivi ni maadui, ukiwaamini utakuwa mjinga, kama washauri wako wanakuogopa kukuambia ( washauri waoga sio wazuri)


Tukubali tu kuwa hii Katiba ya sasa haitakuwa nzuri pamoja na kuwa tumeungana na hawa jamaa, hapa mwanya ni mmoja tu, tudai TANGANYIKA, Kisha tukipata katiba ya kutusaidia kuchukua Nchi, tunakaa chini ( watu wachache tu) haiitaji watu 500, tunafanya katiba ya maana ‘ YENYE AKILI’ ambayo itakufanya TOMAS JEFFERSON wa TANGANYIAKA ( Hapa vipi nimekushawishi?)


Moja kati ya watu ambao huwa nawakubali sana Albanie Marcossy aliwahi kusema kwamba hii nchi ili mambio yaende lazima kujitoa mhanga. Sasa hebu niruhusu mimi sasa nikushauri namna ya kuwashinda hawa ccm, hawa ni wepesi sana , kama ni jumapili unawashinda ‘’ KABLA YA MISA YA KWANZA’ msemo mzuri sana nimeunukuu toka kwa Ally Bananga
lakini kwanza acha nijadili na wadau wapenda mabadiliko wenzangu


Karibuni....


'' Dont go into Politics Expecting to be the next Alphonce Mawazo''
- Andrew Nkumbi
 
taarifa yako tunaipuuza kama tunavyokupuuza wewe mwenyewe
 
taarifa yako tunaipuuza kama tunavyokupuuza wewe mwenyewe

Hiyo sio taalifa, jitahidi ufahamu zaidi taalifa ni nini. Pili don't generalize kuwa unapuuza, mpuuzaji huwa hathubutu hata kupoteza Muda kuandika, instead sema huna cha kuchangia ....taratibu utanielewa tu hata kwa nguvu ikiwezekana nitakulazimisha unielewe
 
Unaweza ukatumwa kupima upepo kama ni mzito au kawaida,ila tu kwa ufupi umechemka na kama wewe ndiyo usyalamya wa taifya basi karudi kwa ma master wako upya akupe mbinu nyigine za kutuletea jukwaani.
Unaongelea vitu kwa historia mbovu na mfu bila kuzingatia wakati na mazingira halisi,
kumbe mzunguko wote bado unaakili za kilumumba maana hakuna shujaa ambaye hujipendekeza na kujiinua bali huinuliwa na anaowapigania hata kama nafsiye itakuwa umautini.
Ukawa ni tishio kwa uhai wa c.c.m.
Freeman mbowe ni kiongozi aliye tukuka.
 
Unaweza ukatumwa kupima upepo kama ni mzito au kawaida,ila tu kwa ufupi umechemka na kama wewe ndiyo usyalamya wa taifya basi karudi kwa ma master wako upya akupe mbinu nyigine za kutuletea jukwaani.
Unaongelea vitu kwa historia mbovu na mfu bila kuzingatia wakati na mazingira halisi,
kumbe mzunguko wote bado unaakili za kilumumba maana hakuna shujaa ambaye hujipendekeza na kujiinua bali huinuliwa na anaowapigania hata kama nafsiye itakuwa umautini.
Ukawa ni tishio kwa uhai wa c.c.m.
Freeman mbowe ni kiongozi aliye tukuka.

Hujachangia chochote zaidi ya kulaumu, jipange umekurupuka,hii sio kombolela kijana, Kama siasa ndio unajifunzia JF, umepotea, watu wamekaa darasani mamia ya masaa, sijakurupuka kuandika...

" Don't go into politics expecting to be the next Alphonce Mawazo "
 
hiyo sio taalifa, jitahidi ufahamu zaidi taalifa ni nini. Pili don't generalize kuwa unapuuza, mpuuzaji huwa hathubutu hata kupoteza muda kuandika, instead sema huna cha kuchangia ....taratibu utanielewa tu hata kwa nguvu ikiwezekana nitakulazimisha unielewe

kijana unamapungufu fulani katika kuandika,kujenga hoja na kuwasilisha maoni yako binafsi yasiyo zingatia weledi wowote.
 
hujachangia chochote zaidi ya kulaumu, jipange umekurupuka,hii sio kombolela kijana, kama siasa ndio unajifunzia jf, umepotea, watu wamekaa darasani mamia ya masaa, sijakurupuka kuandika...

" don't go into politics expecting to be the next alphonce mawazo "

hivi ukniita mimi kijana na jei kei naye utamwita nani?
Ila tu kwa ufupi unamapungufu sana kijana naamini utakuwa ni zao la division mulugo.
 
kijana unamapungufu fulani katika kuandika,kujenga hoja na kuwasilisha maoni yako binafsi yasiyo zingatia weledi wowote.

Kazi yako sinkuangalia mapungufu ya kuandika, suala la msingi hapa jukwaani ni hoja kwa hoja, Kama una akili nzuri rejea andiko langu kisha urudi tena...pinga hoja nitakuelewa zaidi na sio Maandiko AMA mpangilio, hata huo bado hujajua vizuri, jipange usikurupuke...
 
hivi ukniita mimi kijana na jei kei naye utamwita nani?
Ila tu kwa ufupi unamapungufu sana kijana naamini utakuwa ni zao la division mulugo.

Unadhani ujana ni umri tu, age is just a number, akili yako kwa yangu bado ni kijana, hapa huna pa kukwepea, wewe ni akili ndogo katika ndogo... AMA John Stuart Mill angeweza kukuita satisfied fool.....
 
Umejamba tu mkuu. Sijaona ulichosema

Ni kwasababu akili yako haina macho ya kuona, sishangai sana maana watu wa aina yako wanahitajika ili dunia iwe Kama jinsi ilivyo...haya mambo yana wenyewe jipange uje tena
 
unadhani ujana ni umri tu, age is just a number, akili yako kwa yangu bado ni kijana, hapa huna pa kukwepea, wewe ni akili ndogo katika ndogo... Ama john stuart mill angeweza kukuita satisfied fool.....

nikishajua we ni dizaini ya wenye dozi milembe lazima nikupeleke kama ulvyo ili mi mzima nisije onekana mdiye mwenye dozi.
Siwezi jibu hoja za ualipyoto zenye mtazamo wa umaligwengwe,na kauli za kimsemembo zilizo kosa ufani wa kimafikiri na ujwabini wa hakima mujarabu.
La haula kwata yakheeee karibu kisiwandui.
 
nikishajua we ni dizaini ya wenye dozi milembe lazima nikupeleke kama ulvyo ili mi mzima nisije onekana mdiye mwenye dozi.
Siwezi jibu hoja za ualipyoto zenye mtazamo wa umaligwengwe,na kauli za kimsemembo zilizo kosa ufani wa kimafikiri na ujwabini wa hakima mujarabu.
La haula kwata yakheeee karibu kisiwandui.

Satisfied fool, huna hoja ya kujibu hoja za akili kubwa, watu wa dizaini Kama yako, hapa unapoteza Muda tu, long time sana nilishavuka huko, hata Mimi zamani nilikuwa Kama wewe, emancipate yourself, watu Kama wewe ni hasara kwa Taifa...
 
Eleanor Roosevelt aliwahi kusema

"Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people."

Hapa jukwaani wengi ni Small minds, hivyo wawanipi tabu kabisa, average mind angalau ninaweza kujadili nao na wakanielewa na wakahamia ktk great minds, lakini Great minds wanajua nini namaanisha, hao tunaweza kujadili na kufikia hatua nzuri, hivyo we Kama akili yako ni ndogo hapa sio pahara pako, lakini karibu itakusaidia wakati mwingine

"Don't go into politics expecting to be the next Alphonce Mawazo"
 
Kuungana kwao mpaka sasa sijawa na uelewa mkubwa maana yaonekana kama wanataka kuungana na kufikia kumsimamisha mtu mmoja kama mgombea uraisi, walijaribu kwa kuanzia jangwani lakini haikufanya kazi vizuri sasa inatumika nguvu ya ziada,
Tusubiri tuone hii movie mie sina ushabiki nataka katiba bora itakayo nilinda lwa mema na neema tele.
 
Kuungana kwao mpaka sasa sijawa na uelewa mkubwa maana yaonekana kama wanataka kuungana na kufikia kumsimamisha mtu mmoja kama mgombea uraisi, walijaribu kwa kuanzia jangwani lakini haikufanya kazi vizuri sasa inatumika nguvu ya ziada,
Tusubiri tuone hii movie mie sina ushabiki nataka katiba bora itakayo nilinda lwa mema na neema tele.

Kiongozi, binafsi nimejaribu kufuatilia kwa kina sana, inawezekana kabisa kuwa jambo hili ni kwa mapenzi mema wala sikatai, lakini hiyo usiwe sababu ya kuzuia Mawazo mapya eti kisa Ushabiki.

Na ndio maana katika andiko langu hapo juu, nimesema wazi kuwa Mimi ningekuwa Mbowe hayo ndiyo ningefanya kwa nia njema pia, na pia nimejaribu kutoa picha ya upande wa pili ili Kama ktk Mawazo ya Mbowe haikuwemo, basi ajue kuwa inawezekana ikawa hivyo. ( chochote kinaweza kutokea, japo hatuombei)

CCM sio wajinga wajinga tu.Hawapendi nchi iondoke mikononi mwao kirahisi Rahisi mpaka pale tu mbinu zao zote zikishindwa, huko ndiko nadhani tunaelekea... Ahsante sana kwa mchango wako
 
Back
Top Bottom