Mbowe: Mimi kisiki, anayetaka kujipima ubavu na mimi aje

Mh. Mbowe tokea arudishe lile gari halafu akarudi kulichukua kwa mlango wa nyuma sijawahi kumuamini tena.

1.jpg
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa
fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali.

LAKINI KWA KAULI HII:"“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba
viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,”


Hii inaleta picha gani kwa watu wanaopenda demokrasia na haki???


Mandla,
Wa Dodoma!!!
 
ukiona kocha wa yanga anaomba eti simba wasimcheze mchezaji flani, hapo ujue kocha ameshapanic ameshaona kushindwa kwake kabla hata mechi haijaanza.
Ni kwanini kocha wa CCM anataka kutupangia safu ya wachezaji wetu wa CDM??

usijitoe ufahamu, Huu sio upinzani wa CCM na CDM Huu ni mgongano wa mawazo baina ya Wandemokrasia dhidi ya Wahafidhina
 
Tulikuwa tunaomba usiku kucha Mbowe arudi ulingoni naimekuwa inatosha kumshukuru mungu kwa hilo..... Wenye chama chetu tunajua kwa nini tunamtaka Mbowe
 
Shibuda alikimbia nini ccm? Alichukuwa fomu kugombea urais nini kilimtokea? Mtikila na DP lini amefanya uchaguzi? CUF je mbona hamsemi? Uoga umewabana. Acheni hizo njooni na sera za kisayansi za kuimarisha chama na sio ----- kama huu.
 
wewe ni mchezaji wa team ya simba, team ya yanga ikipanga safu mbovu ndo usindi wa simba.
ni kweli unataka kuimarisha team ya mshindani wako ili akushinde??

ni mfirisikaji wa mawazo tu ndio anaweza kuthubutu kuwaza kama unavyowaza! sikia ili pawepo na simba bora inahitajika pawepo na yanga makini kinyume chake timu zote zitakua mbovu na sie mashabiki kukosa kabisa radha ya mpira
 
usijitoe ufahamu, Huu sio upinzani wa CCM na CDM Huu ni mgongano wa mawazo baina ya Wandemokrasia dhidi ya Wahafidhina

kwanini hao unaowaita wanademokrasia wanaolilia swala hili ni ccm tu, na sio CDM?
kama unajiamini kwanini unamuhofia uiamara wa mshindani wako??
 
ni mfirisikaji wa mawazo tu ndio anaweza kuthubutu kuwaza kama unavyowaza! sikia ili pawepo na simba bora inahitajika pawepo na yanga makini kinyume chake timu zote zitakua mbovu na sie mashabiki kukosa kabisa radha ya mpira
hata malaika hawezi kumuombea uimara mshindani wake.
huu utoto dandanyaneni watumwa wa fikra.
biashara ya kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe kama inakuingizia kipato endelea nayo ila in logic and reasoning hakuna atakayekubaliana na utoto huo.
 
Ahaaa wapi. Kisiki baada ya kumfukuza mwanamume mwenzako Zitto Zuberi Kabwe? Unafanya mazingaombwe? Tangu uwe Mwenyekiti hujawahi kushindana, unapewa ushindi wa mezani. Wewe ni mwoga, huna chochote! Ungemuacha Zitto aingie kwenye uchaguzi angekuliza saa nne na nusu asubuhi. Wadanganye wajinga wenzako!

Wanawake ndio wanafukuzwagwa siyo wanaume wewe. Wanawake ndio wanafanyaga mambo ya siri siri ila wanaume huja jukwaani hadharani na kusema mimi ni mbabe sipigiki. Siyo kujifungia na mshositi kupanga mipango ovu ya makundi. Mbowe kasimama kasema mimi ni kisiki. Angekua jasir angesubiri leo akachukua form siyo kijifungia na kina mkumbo na kuandaa maandiko ya kugawa chama.
 
Baada ya ile kauli tata kabisa kutoka kwa Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA kuwa tatizo siyo kuchukua pesa kwa Nimroad MKONO bali tatizo ni unatumiaje pesa hizo, hii ni kauli nyingine tata kutolewa na kiongozi huyo kutoka makao makuu ya chama hizo mtaa wa Ufipa KINONDONI. Akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho kwa mara nyingine , MBOWE bila kumumunya maneno akasema yeye ni KISIKI ndani ya Chadema na kuwataka wote wanaodhani wanaweza kujipima ubavu naye katika kuwania nafasi hiyo wajitokeze

Hakika mungu ni wajabu sana, ameamua kuuweka udikteta wa Mbowe hadharani na hii ni aibu kwa wale wote waliokuwa wakimkingia kifua kiongozi huyu kuwa siyo Dikteta. KAULI hii imekidhalilisha Chama na wanachama wake kwa ujumla kwa vile ni wazi kabisa ndani ya CHADEMA hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kukiongoza chama na pengine sasa, watanzania tunaweza kujiaminisha kuwa hata migogoro inayokikumba chama hicho na kupelekea baadhi ya makada wa chama hicho kufukuzwa na wengine kujiengua wenyewe ni kutokana na ukweli kwamba makundi hayo yalionesha nia ya kuwa na kiongozi mbada wa chama hicho.
kwa habari zaidi juu ya ubabe wa Mbowe, soma magazeti ya Tanzania na Mwananchi
wewe kweli kichwa maji akili yako aina. Waledi kazi kuropoka usicho kijuwa ya cdm tuwachie cdm kenge wa ACT we.
 
Wote si akili zenu sawa, wajanja watajiondokea mbaki mazuzu

Wajanja wanajiondokea au wanafukuzwa? Hivi Zitto nae ni mjanja!? Teh teh teh....na Kitila Mkumbo aliyedhalilisha utu, heshima, weledi, usomi na familia yake kwa Tsh 200,000/- nae mjanja?
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa na uwezo mkubwa na ubabe wengi watakupisha na hakuna atakaye kuzuilia. Hii ndiyo asili ya mbowe ni aina ya mtu ambaye hazuiliwi kwa uwezo mkubwa alionao hadi wote wamenyamaza maana koti lake hakuna wa kulivaa na hata kama yupo hajiamini ka litamkaa na chadema wote wanamwamini. Mbowe chapa kazi maana wanaotaka uondoke ni maccm adui namba moja wa chadema sababu imewashika pabaya na mziki wako ni mnene.
 
Ahaaa wapi. Kisiki baada ya kumfukuza mwanamume mwenzako Zitto Zuberi Kabwe? Unafanya mazingaombwe? Tangu uwe Mwenyekiti hujawahi kushindana, unapewa ushindi wa mezani. Wewe ni mwoga, huna chochote! Ungemuacha Zitto aingie kwenye uchaguzi angekuliza saa nne na nusu asubuhi. Wadanganye wajinga wenzako!
Kama unampenda sana zito mwambie agombee ACT na urais urais aone balaa lake
 
Back
Top Bottom