Kwa enzi hii iliyopo believe me hakuna Kiongozi yeyote wa upinzani ambaye anaweza kupambana na CCM na kushinda.Sisemi hivyo kwa ushabiki wa kisiasa bali nazingatia hali halisi ya kisiasa iliyopo hapa nchini hairuhusu.Watanzania wengi bado mbumbumbu.90% hawajui maana ya katiba,serikali au siasa ni nini.Njaa inatawala kila sehemu na ufisadi umeenea nchi nzima.Chungulia hapo jirani Kenya tu utajua kuwa huko kumekucha wakati sisi tunaendelea kuuchapa usingizi mzito.
Ni rahisi sana to make your way up to top of any opposition party kama utakua jasiri, na more than that viongozi shupavu kambi ya upinzani ni wachache sana.
Wajameni, kweli hamna viongozi wengi shupavu kambi ya upinzani?? Nyerere alisema kweli!!!!
Viongozi wa serikali ijayo wamo humu humu jambo forums, tuache woga, tujitokeze na kupanda majukwaani tuyaongee haya tunayoyaandika humu. Ni rahisi sana to make your way up to top of any opposition party kama utakua jasiri, na more than that viongozi shupavu kambi ya upinzani ni wachache sana.
Nakubaliana na umairi wa wana jambo forums lakini hata uongee vipi kama Katiba isipobadilishwa kukidhi mahitaji ya current politics then hiyo ni ndoto.Pili kama hatutaweza kupromote elimu then bado pilao inatosha kuipeleka ccm ikulu.Tatu elimu ya uraia ni muhimu kwani itawapa wananchi ujasiri since watakuwa aware na haki zao hivyo kuwa imara na kutokuyumbishwa hata kama nguvu ya dola inatumika!
Jamani, au njaa nayo ni tatizo??!! Vipi hata daresalama CCM wajizolee kura??? Viti vyote vya ubunge, halmashauri zote wanaongoza wao! Hivi kweli hata DSM kuna tatizo la ufahamu kiasi cha kumfanya mtu asijue wapi pa kuweka kura yake??? Yawezekana ni matokeo ya mchezo mchafu tu???
Kweli jameni upinzani uliopo sasa unakubalika kisawasawa? ua kuna haja ya kupanga safu mupya???
Ni percentage ndogo sana ya wapiga kura wenye uwezo wa kuvisit hii website kila siku ndo maana nimesema nadhani we need to do a little bit more, lets take our fight further- tuzunguke kila kona ya nchi tupande majukwaani na kuyasema haya tunayoyaandika humu.Ni jukumu la viongozi wa upinzani kupoint out vipengele vinavyohitaji kubadilishwa na kuwafahamisha wananchi, hata wale wa vijijini, do you think all of them are doing enough on this? Elimu yetu ya uraia imekwepo siku zote, ukiachilia mbali higher learning insitutions, chini kwenye mashule ya msingi na sekondari- ni kama wanafunzi wanafundishwa namna ya kuiheshimu na kuigopa serekali iliyoko madarakani, hakuna mwalimu mwenye guts za kusimama mbele ya darasa na kuppoint out kipengele kibovu kwenye katiba au kucritise government, we all know the reason. Proper elimu ya uraia inatolewa humu, tuendelee kusambaza habari za mtandao huu kwa means zozote zile zinazowezekana- na kama nilivyosema tuanze kupanda majukwaani ili tusikike na kufikisha ujumbe kwa walio wengi, there are subscribers hapa ambao naamini they are good enough kuwa kwenye cabinet!
NA MATOKEO YA MCHEZO MCHAFU PIA NI POSSIBILTY!Jamani, au njaa nayo ni tatizo??!! Vipi hata daresalama CCM wajizolee kura??? Viti vyote vya ubunge, halmashauri zote wanaongoza wao! Hivi kweli hata DSM kuna tatizo la ufahamu kiasi cha kumfanya mtu asijue wapi pa kuweka kura yake??? Yawezekana ni matokeo ya mchezo mchafu tu???
Kweli jameni upinzani uliopo sasa unakubalika kisawasawa? ua kuna haja ya kupanga safu mupya???
Hizi ndoto za mchana hivi mnatarajia upinzani kutoa Raisi,japo ni maoni naona bora muangalie upande wa CCM ni nani anaweza kufanya kweli,maana bado CCM ina watu wana uchungu na nchi hii lakini naweza kusema wamebanwa kwa maoni yangu kama Salum angeukwaa Uraisi basi Tanzania ingechukua muda mfupi sana kupiga hatua ya maendeleo,kwa ninavyomuona ni mtu yupo seriaz kabisa,inaonekana hana mchezo na kucheka cheka na wavivu.Na ni katika wale watu wachache tulio nao ambao nina uhakika kabisa wanaweza kuivusha Tanzania kutoka hapa ilipo,na pengine sababu ya kukosa Uraisi kipindi hiki ni kuwa CCM wenzake wanamuogopa maana hana muhali na mtu anakupa maneno yako kwenye uso nilimfahamu alipokuwa Waziri wa Ulinzi,huyu jamaa alikuwa ni hatari kwani hata wakuu wa majeshi walikuwa wanamwogopa,sababu akikuona goigoi anakupa ukweli na ukifanya upogo anakuweka kando.