Mbowe, Lipumba, Lyatonga wanaweza???

bokassa

JF-Expert Member
May 19, 2007
401
11
Ni hakika kuwa CCM imepoteza mwelekeo. Viongozi na makada wake. Nimekata tamaa kiasi cha kuombea waondolewe madarakani haraka.

Sina shaka na vyama shindani vya CCM, japo ni vichanga lakini vimeonyesha ukomavu mkubwa ki-sera. Hata hivyo mara nyingi huwa najiuliza nani baada ya kikwete. Hivi kweli Mbowe, Lipumba, Lyatonga wanaweza??? ikibidi, nani awatangulie wenzake jumba jeupee!!?

Hebu tuwajadili kwa umakini na kwa tahadhari, 2010 si mbali tusije tukafanya makosa yale yale!!!
 
Simfahamu vizuri Mbowe zaidi ya kumfahamu wakati wa Kampeni zake 2005. Ni muongeaji mzuri na anaonekana ni mpiganaji mzuru kwenye uwanja wa vita. Nimesoma humu JF baadhi ya members kumwelezea kama ni mtu anayehitaji muda kuendelea kujinoa na siasa za bongo. inawezekana huko baadaye akawa mkomavu wa hakika.

Lipumba, ni mzuri, msomi mzuri na anyejua mambo, bahati mbaya kwake hana bahati ya kuumngwa mkono TZ bara. lakini pia waTZ wengi wanakihusisha chama cha CUF na Udini kutokana na siasa chafu za kupakana matope kutoka CCM na hata baadhi ya vyama wenza vya upinzani.

Lyatonga, Hapana, huyu keshasema siasa basi, kama kweli amedhamiria kwa hiyo huyu tumwache apumzike. Lakini pia enzi zake zimekwisha. Technical error ya 1995 ilimkosesha ushindi.

Kama vyama vinne (Chadema, CUF, TLP na NCCR Mageuzi) vitaendelea na mkakati wao wa muungano, basi hawana budi kumwandaa mtu anayekubalika na jamii ya WaTz kuanzia sasa na isiwe miongoni mwa hao uliowataja hapo juu.

Waanze na mkakati wa kufanya ajulikane kila pembe ya nchi, hapo tutashuhudia mpambano mkali 2010
 
Mimi napendekeza vyama vya upinzani vitafute watu wa "kuwaplant "katika kila kata ama kila kijiji nchini.hii iwe ni long term stratergy. wanaweza kuplant watu wa kufanya kazi ya miaka 15 ijayo na kuendelea

watu wa namna hii wawe supported financially ikibidi. ili kutatua matatizo yao madogo madogo.

lakini kikubwa ni kwamba watu hawa wajiingize ndani katika taasisi za kijamii. mathalani wawe ni walimu wa shule za msingi n.k

Kijijini ukiwa ni mwalimu unaheshimika na kukubalika sana kwa wazazi.

halafu muda muafaka ukifika, ambao mnaona tayari hawa watu wameshawateka wananchi kutokana na kukubalika kwao mnawasimamisha kugombea viti mbali mbali,ubunge, udiwani,uenyekiti wa kijiji n.k

wakati huo huo mnawatumia watu hawa kuandaa mazingira ya kampeni kwa mgombea uraisi kupitia kambi ya upinzani.

hili mimi naona linawezekana kabisa, kwa kuanzia vyama vikubwa vya upinzani vinaweza kugawana vijiji vya kuplant watu wao.
 
Gamba ya Njoka,

Mawazo mazuri, lakini utamaduni na desturi ya watanzania hawataki kuangali mbali asilani... labda uendelee kuomba dua.

Watanzania wengi wanataka biashara asubuhi, mahesabu jioni
 
Kwa enzi hii iliyopo believe me hakuna Kiongozi yeyote wa upinzani ambaye anaweza kupambana na CCM na kushinda.Sisemi hivyo kwa ushabiki wa kisiasa bali nazingatia hali halisi ya kisiasa iliyopo hapa nchini hairuhusu.Watanzania wengi bado mbumbumbu.90% hawajui maana ya katiba,serikali au siasa ni nini.Njaa inatawala kila sehemu na ufisadi umeenea nchi nzima.Chungulia hapo jirani Kenya tu utajua kuwa huko kumekucha wakati sisi tunaendelea kuuchapa usingizi mzito.
 
Alnadaby, tatizo ni wapiga kura au viongozi wa upinzani??
 
Viongozi wa serikali ijayo wamo humu humu jambo forums, tuache woga, tujitokeze na kupanda majukwaani tuyaongee haya tunayoyaandika humu. Ni rahisi sana to make your way up to top of any opposition party kama utakua jasiri, na more than that viongozi shupavu kambi ya upinzani ni wachache sana.
 
Ni rahisi sana to make your way up to top of any opposition party kama utakua jasiri, na more than that viongozi shupavu kambi ya upinzani ni wachache sana.

Wajameni, kweli hamna viongozi wengi shupavu kambi ya upinzani?? Nyerere alisema kweli!!!!
 
Wajameni, kweli hamna viongozi wengi shupavu kambi ya upinzani?? Nyerere alisema kweli!!!!

Kaka Bokasa kuna viongozi watatu tu kambi ya upinzani ambao naamini wakipewa nchi tutaona mabadiliko lakini the rest- nahisi hali itakua mbaya kuliko ilivyo sasa.Anyway huu ni mtazamo wangu tu.....
 
Viongozi wa serikali ijayo wamo humu humu jambo forums, tuache woga, tujitokeze na kupanda majukwaani tuyaongee haya tunayoyaandika humu. Ni rahisi sana to make your way up to top of any opposition party kama utakua jasiri, na more than that viongozi shupavu kambi ya upinzani ni wachache sana.

Nakubaliana na umairi wa wana jambo forums lakini hata uongee vipi kama Katiba isipobadilishwa kukidhi mahitaji ya current politics then hiyo ni ndoto.Pili kama hatutaweza kupromote elimu then bado pilao inatosha kuipeleka ccm ikulu.Tatu elimu ya uraia ni muhimu kwani itawapa wananchi ujasiri since watakuwa aware na haki zao hivyo kuwa imara na kutokuyumbishwa hata kama nguvu ya dola inatumika!
 
Ni percentage ndogo sana ya wapiga kura wenye uwezo wa kuvisit hii website kila siku ndo maana nimesema nadhani we need to do a little bit more, lets take our fight further- tuzunguke kila kona ya nchi tupande majukwaani na kuyasema haya tunayoyaandika humu.Ni jukumu la viongozi wa upinzani kupoint out vipengele vinavyohitaji kubadilishwa na kuwafahamisha wananchi, hata wale wa vijijini, do you think all of them are doing enough on this? Elimu yetu ya uraia imekwepo siku zote, ukiachilia mbali higher learning insitutions, chini kwenye mashule ya msingi na sekondari- ni kama wanafunzi wanafundishwa namna ya kuiheshimu na kuigopa serekali iliyoko madarakani, hakuna mwalimu mwenye guts za kusimama mbele ya darasa na kuppoint out kipengele kibovu kwenye katiba au kucritise government, we all know the reason. Proper elimu ya uraia inatolewa humu, tuendelee kusambaza habari za mtandao huu kwa means zozote zile zinazowezekana- na kama nilivyosema tuanze kupanda majukwaani ili tusikike na kufikisha ujumbe kwa walio wengi, there are subscribers hapa ambao naamini they are good enough kuwa kwenye cabinet!
 
Jamani, au njaa nayo ni tatizo??!! Vipi hata daresalama CCM wajizolee kura??? Viti vyote vya ubunge, halmashauri zote wanaongoza wao! Hivi kweli hata DSM kuna tatizo la ufahamu kiasi cha kumfanya mtu asijue wapi pa kuweka kura yake??? Yawezekana ni matokeo ya mchezo mchafu tu???

Kweli jameni upinzani uliopo sasa unakubalika kisawasawa? ua kuna haja ya kupanga safu mupya???
 
NAJUA HLIO JUHUSU DAR ILA SJUI NI ASILIMIA NGAPI YA WAKAZI HAO WA BONGO WANA ELIMU,NA KUHUSU NJAA BADO PIA VILEVILE SIJUI NI ASILIMIA NGAPI YA WABONGO WENYE UWEZO WA KUJIKIMU KWA MILO INAYOTAKIWA KWA SIKU!NA KAMA UKITAKA NINA UWEZO WA KUEXPLAIN IN DETAILS KWAMBA NI KWA NAMNA GANI NJAA INAWEZA KUMFANYA MTU AKAUZA UHURU WAKE!
 
Ni percentage ndogo sana ya wapiga kura wenye uwezo wa kuvisit hii website kila siku ndo maana nimesema nadhani we need to do a little bit more, lets take our fight further- tuzunguke kila kona ya nchi tupande majukwaani na kuyasema haya tunayoyaandika humu.Ni jukumu la viongozi wa upinzani kupoint out vipengele vinavyohitaji kubadilishwa na kuwafahamisha wananchi, hata wale wa vijijini, do you think all of them are doing enough on this? Elimu yetu ya uraia imekwepo siku zote, ukiachilia mbali higher learning insitutions, chini kwenye mashule ya msingi na sekondari- ni kama wanafunzi wanafundishwa namna ya kuiheshimu na kuigopa serekali iliyoko madarakani, hakuna mwalimu mwenye guts za kusimama mbele ya darasa na kuppoint out kipengele kibovu kwenye katiba au kucritise government, we all know the reason. Proper elimu ya uraia inatolewa humu, tuendelee kusambaza habari za mtandao huu kwa means zozote zile zinazowezekana- na kama nilivyosema tuanze kupanda majukwaani ili tusikike na kufikisha ujumbe kwa walio wengi, there are subscribers hapa ambao naamini they are good enough kuwa kwenye cabinet!

ONCE AGAIN NI LAZIMA UELEWE SERIKALI YA CCM HAIWEZI KUFANYA HIVYO KWANI HAITAKUWA NA MANUFAA KWAO!WANAJUA UKIWAPA WATU ELIMU WATAKUWA NA UWEZO WA KUJUA UTUMBO WANAOUFANYA HIVYO KUHATARISHA ULAJI WAO!PILI UNAPOSEMA HATA WALE WA VIJIJINI UNAKOSEA,BADALE YAKE ULITAKIWA USEME "HASWA WALE WA VIJIJINI"NI KWANINI NASEMA HIVYO?KUMBUKA ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI IKO VIJIJINI,SINA TAKWIMU HALISI ILA NAWEZA KUGUESS KUWA NI ZAIDI YA 80%.FANYA TATHMINI UONE TANZANIA INA WANANCHI WANGAPI NA NI WANGAPI WAMEPIGA KURA,UTAKUJA KUSHANGAA KUWA WANAOTUCHAGULIA VIONGOZI TANZANIA HAWAFIKII HATA NUSU YA WANANCHI WOTE,KWA MAANA HIYO BASI INAWEZEKANA KUWA NI CHINI YA ASILIA HAMSINI YA WATANZANIA WANAOAMUA NI NANI AINGIE MADARAKANI!SASA BASI TUJIULIZE NI KWA NINI WANANCHI WALIOWENGI HAWAPIGI KURA?MOJA NI KUTIKUJUA UMUHIMU WAKE,MBILI NI UKOSEFU WA ELIMU UTAKAOWAFANYA WASIJUE KUWA UPIGAJI KURA WAO NDIO UNAOPELEKEA MATOKEO YA MAISHA YAO,KWA MAANA HIYO KUTOKUPIGA KURA NI SAWA NA KUUZA AMA KUWEKA REHANI HAKI YAKO AMBAPO ULIYEMUUZIA AMA KUWEKA REHANI ANA HAKI KUICHEZEA NA KUIFANYIA LOLOTE HAKI HIYO YAKO ULIYOIUZA AMA KUIWEKA REHANI!
 
Jamani, au njaa nayo ni tatizo??!! Vipi hata daresalama CCM wajizolee kura??? Viti vyote vya ubunge, halmashauri zote wanaongoza wao! Hivi kweli hata DSM kuna tatizo la ufahamu kiasi cha kumfanya mtu asijue wapi pa kuweka kura yake??? Yawezekana ni matokeo ya mchezo mchafu tu???

Kweli jameni upinzani uliopo sasa unakubalika kisawasawa? ua kuna haja ya kupanga safu mupya???
NA MATOKEO YA MCHEZO MCHAFU PIA NI POSSIBILTY!
 
Hizi ndoto za mchana hivi mnatarajia upinzani kutoa Raisi,japo ni maoni naona bora muangalie upande wa CCM ni nani anaweza kufanya kweli,maana bado CCM ina watu wana uchungu na nchi hii lakini naweza kusema wamebanwa kwa maoni yangu kama Salum angeukwaa Uraisi basi Tanzania ingechukua muda mfupi sana kupiga hatua ya maendeleo,kwa ninavyomuona ni mtu yupo seriaz kabisa,inaonekana hana mchezo na kucheka cheka na wavivu.Na ni katika wale watu wachache tulio nao ambao nina uhakika kabisa wanaweza kuivusha Tanzania kutoka hapa ilipo,na pengine sababu ya kukosa Uraisi kipindi hiki ni kuwa CCM wenzake wanamuogopa maana hana muhali na mtu anakupa maneno yako kwenye uso nilimfahamu alipokuwa Waziri wa Ulinzi,huyu jamaa alikuwa ni hatari kwani hata wakuu wa majeshi walikuwa wanamwogopa,sababu akikuona goigoi anakupa ukweli na ukifanya upogo anakuweka kando.
 
KWANZA NI WAZI UNADIDIMIZA FIKRA ZA KIDEMOKRASIA,PILI KUMBUKA HATA MH RAIS MWENYEWE AMEKIRI HIVI MAJUZI TU PALE KANISANI AZANIA FRONT KWAMBA HAUSIKI KUZIANDAA ILANI ZA CHAMA.YEYE NI MGOMBEA TU MWENYE KUKIWAKILISHA CHAMA PAMOJA NA SERA NA ILANI ZAKE.KWA MANTIKI HIYO BASI;HATA SALUM LABDA ASINGEWEZA KULETA UTOFAUTI WOWOTE KWANI HATA YEYE ANGEKUMBWA NA YALE YALE YALIYOWAKUMBA WENZAKE.KUTOKANA NA HILO BASI NI JAMBO LA WAZI KUWA MABADILIKO HAYAWEZI KUWA YA KWELI KAMA KIONGOZI ATATOKA KWENYE CHAMA KILEKILE CHENYE SERA NA ILANI ZILEZILE AMBAZO MPAKA SASA ZIMEPROVE FAILURE KWASABABU PENGO KATI YA WALIZONAZO NA WASIONAZO LINAZIDI KUONGEZEKA!KAMA NI MABADILIKO YA KWELI BASI CCM HAIWEZI KUYAFANYA KWASABABU HATA MWAKILISHI WAO ALIPATA USHINDI MNONO WA ZAIDI YA 80%,WALETE MABADILIKO YA NINI WAKATI NI WAZI WANANCHI WANAWAKUBALI?SIJUI NI ASILIMIA NGAPI YA WATANZANIA WALIOPIGA KURA ILI KUWEZA KUIPA NGUVU ZAIDI HIYO 80% YA USHINDI.LAKINI USHINDI HUO ULITOKA KWENYE KUNDI LA WALIOPIGA KURA.KWAMBA KUNDI HILO LINA WANANCHI WANGAPI,HILO NI JUU YA WAPINZANI KULIFANYIA UTAFITI NA KUHAKIKISHA KUWA ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI WANAPATA NAFASI YA KUWACHAGUA VIONGOZI WAO BADALA YA FUNGU DOGO TU LA WANANCHI KUWACHAGULIA WANANCHI WOTE VIONGOZI!,SIO NIA YANGU KUJADILI HILO KWASASA KWANI WANANCHI WENZETU WALIOTUWAKILISHA BADO TUNAWAHESHIMU,NDIO DEMOKRASIA ILIVYO,WASHATUWAKILISHA.CHANGAMOTO HAPA KWA VYAMA VYA UPINZANI,WAPENDA MAENDELEO NA WAPENDAO DEMOKRASIA YA KWELI POPOTE PALE WALIPO NI KUHAKIKISHA KWAMBA WANANCHI WANAELIMISHWA UMUHIMU WA KUPIGA KURA ILI KUWEZA KUTOA FURSA KWA WANANCHI WENGI ZAIDI KUWEZA KUSHIRIKI KWENYE TUKIO HILO MUHIMU LA UCHAGUZI.NA KWA VIONGOZI WENGINE WA UPINZANI KAMA KUNA SUPPORT YOYOTE WANAYOIPATA KUTOKA KWA WANANCHI THEN WAHAKIKISHE KWAMBA WANAELEWA UMUHIMU WA KUPIGA KURA,NA KUCHAGUA VIONGOZI KUTOKANA NA SERA NA SIO MAPENZI BINAFSI YA KIITIKADI AMA YA AINA NYINGINEZO ZOZOTE!
 
Ni kweli kabisa kama elimu haitapewa kipaumbele bado pilau itaendelea kupeleka mafisadi ikulu na maeneo yote nyeti ya nchi hii. Imefikia mahali nchi yetu inaingiliwa na utawala wa kifalme kwa maana ya kurithishana, leo tunaelekea mahali utakuta baba ni rais, mama waziri mkuu na mtoto waziri wa fedha. Bila elimu hatutaachwa kuburuzwa hapo, siyo kwamba hakuna wenye sifa hizo ila kuipata hiyo nafasi ndiyo ngumu. Kumbukemi ni hivi majuzi tu kuna mtoto mdogo kutoka huko pembezoni mwa Tanzania alimtoa jasho waziri wetu mkubwa kuliko
wote kwa swali rahisi na lakini zito!
Turudi kwenye mada, inawezekana kabisa yeyote kati ya hawa anaweza kuwa lakini Lyatonga hapana; Nampendekza Mbowe kama atakosekana mpya kabisa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom