CHADEMA mmelewa sifa, Mnapoteza uhalali wa kukabidhiwa dola!

LENGEJU BOB

Member
Nov 1, 2010
53
29
Na. Robert Victor Lengeju

Naandika Makala haya nikiwa na maumivu makubwa moyoni. Kwamba yumkini tumaini langu, na la watanzania wengine la kuiona nchi Tanzania ikikomaa kidemokrasia na kuingia karne ya mabadiliko linayeyuka kwa mara nyingine tena. Tumaini limefifia, hakuna tena tegemeo. Kwa unyonge turudi tena ndani ya chama tawala tutafute anayefaa kutuongoza kwa miaka mingine mitano au hata kumi ijayo.

UTANGULIZI
Mihemko ya siasa za ushindani ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1990 na mwaka 1995, NCCR Mageuzi, chini ya Augustione Lyatonga Mrema (Sasa Dr. A.L.Mrema) kilikonga nyoyo za watanzania kwa kiwango ambacho hakikuwahi kushuhudiwa. Umaarufu ule wa NCCR-Mageuzi, kimsingi, ulijengwa na jina la Mrema, ambaye kwa wakati huo alijipambanua kuwa mpigania haki wa kweli na kwakweli amebaki kuwa shujaa wa fukuto la mageuzi ya siasa za vyama vingi katika Tanzania. Siyo azma yangu leo kuelezea harakati za Mrema na NCCR yake, lakini sote tunafahamu kuwa NCCR ilipita, ikaja TLP, kikaja CUF, ambacho nacho, bado ni miongoni mwa vyama mahiri vya upinzani Tanzania na ndicho chama pekee cha upinzani, kilichofanikiwa walau kunusa dola, CUF ni mshirika sasa wa Serikali ya umoja wa kitaifa (SUK)-Zanzibar.

KUIBUKA NA KUMEA KWA CHADEMA
Hata hivyo, kwa siasa za Tanzania kwa ujumla wake, kiliibuka chama cha Demokrasia na maendeleo, kikiwa na kasi ya kukua na kutanuka kila mwaka na kila awamu ya uchaguzi, hatimaye kujisimika kama chama kikuu cha upinzani. Kwa takwimu tu za haraka haraka, mwaka 1995 Chadema ilikuwa na wabunge 4 na madiwani 42. Mwaka 2000 Chadema kilifanikiwa kuongeza mbunge mmoja na kuongeza madiwani 33; kikawa na wabunge 5 na madiwani 75. Mwaka 2005 Chadema ilijizolea jumla ya wabunge 11 na madiwani 103. Kilele cha mafanikio kilikuwa ni mwaka 2010 ambapo Chadema kilipata wabunge 48 na madiwani 476. Kwa kasi hii, ilianza kudhihirika rasmi kwamba yumkini, chama hiki kinaelekea kushika dola.

Kuna tofauti moja ya msingi kati ya vyama vilivyowahi kuwa juu miaka hiyo yaani NCCR, TLP na CUF na hiki kilichosimama miaka ya hivi karibuni, yaani CHADEMA. Tofauti hiyo ni kwamba, wakati vile vingine vikitegemea zaidi nguvu ya waasisi wake ama watu Fulani maarufu katika kuimarisha ukubalikaji wake mbele ya jamii, CHADEMA kimejijenga haraka kimfumo, kikiwa na umaafuru wa ki-CHAMA, sio jina la mtu, japo kuna majina makubwa makubwa yanayoongezea umaarufu wake.

Taratibu jamii ilianza kuona nuru mbeleni, watu walianza kujiandaa kwa mabadiliko yaliyoonekana ni dhahiri. Watu walitembea (kama wakati wa Mrema), umbali mrefu kufuata sera za chadema, walikaa juani, wakanyeshewa na mvua, wakisikiliza sera za matumaini. Chadema ilizama mioyoni mwao, na midomo yao ilitamka People’s Power huku wakikariri kibwagizo cha M4C. Kila mtu akachangamkia gwanda huku bendera zikipepea mpaka bafuni. Ilikuwa ni fahari kuonekana umejipambanua na Chadema.

KOSA KUU

Kuna jambo muhimu ambalo Chadema na vyama vingine vya upinzani vimeshindwa kabisa kujifunza katika umri wote wa zaidi ya miongo minne ya siasa ya vyama vingi katika Tanzania. Chadema walisahau ukweli kwamba wanaowafuata wako katika makundi tofauti tofauti, kwa mfano, wapo waliochoshwa na chama tawala na wako tayari kufuata mabadiliko hata kama hawana uhakika na wanakoelekea. Wapo waliovutiwa na sera za Chadema na kuamini kwamba tumaini limewadia. Wapo wanaofuata mkumbo tu. Wapo ambao kukaa kwao Chadema kulitokana na udhaifu wa CCM na kwamba siku CCM ikijiweka sawa wanarudi nyumbani.

Kwa kutokujifunza huko, Chadema imefanya DHAMBI kadhaa, na kwa bahati mbaya wanaelekea kuzoea na hawaonyeshi dalili za kuacha au hata kupunguza kasi ya kuboronga. DHAMBI hizo zipo nyingi, lakini nitaainisha nne (4) tu ambazo kwa maoni yangu ni DHAMBI KUBWA.

1. KUBWETEKA kunakotokana na kupendwa kwa ghafla na kukubaliwa na umma wa watanzania.

2. KUCHOKA na kuacha mapema kazi ya msingi ya kujenga chama kwa uenezi wa sera, kujibu na kujenga hoja, pamoja na elimu kwa wananchi wakavamia Propaganda nyepesi na siasa za kibabe.

3. Wanatembelea nyota ya KUCHOKWA kwa chama tawala, wakiacha kujipambanua kiushindani na ki-ubora, kama chama cha siasa cha upinzani, chenye malengo ya kushika dola.

4. Kwa kubweteka kunakotokana na kupendwa, viongozi, wafuasi, wanachama na mashabiki wa Chadema wamejenga DHARAU dhidi ya watanzania, kwa upande mmoja huku wakichukia, kudhihaki na kuwatusi wale wanaoonekana kutoa changamoto kwa kuwa na mtazamo tofauti.

Kwanza mmebaki na imani hewa, kwamba wananchi mnawapenda upeo, na kwahiyo mnaweza kulala, kuamka, kula na kutembea kifua mbele. Ninyi ndio chaguo la watu kwahiyo hata mkifanya makosa kiasi gani, hamtaathirika. Kwani tayari mmeshawaroga watanzania kwa helkopta, magwanda na makasheshe ya M4C.

Pili mmeacha kabisa kufanya kazi ya uenezi na kufanya maandalizi ya kisera kuelekea kushika dola. Mmehamia kwenye kudandia hoja nyepesi na propaganda za ‘vyama tawala”. Siku hizi mnasubiri CCM ikosee ndipo mpate hoja. Mnasubiri wanafunzi wapate Ziro, Mnasubiri Magazeti yafungiwe, mnasubiri, watu watekwe, waandishi wapigwe, mabomu yalipuke, wakulima na wafugaji wapigane, ndipo mpate mada za majukwaani. Hakuna tena mwendelezo wa kufuata dira ya kimkakati, kutekeleza mipango iliyokwishawekwa (kama ipo) na kusimika nguvu zaidi katika kuwaamsha watu wajue haki zao, wafahamu nguvu iliyoko kwenye karatasi ya kura, umuhimu wa kutunza kadi ya kupigia kura na ulazima wa kuchagua mabadiliko. Huko mmeshahama!

Tatu, kama nilivyoeleza hapo juu, kuna kelele nyingi sana nchi nzima, zinazoelekezwa kwa CCM, kwa mapungufu kadhaa ya kiutawala. Kitu ambacho ni cha kawaida kwa chama chochote kilichopo madarakani kulalamikiwa. Nguvu yenu Chadema mmeilekeza katika kuendelea kuwahamasisha wananchi waendelee kuichoka CCM, huku mkiwa hamna mpango wowote wa kuwaonyesha watanzania kuwa Chadema ni chama mbadala. Kwa ufupi ni kwamba mnatembelea nyota ya kile kinachodhaniwa kuwa ni ‘uchovu’ wa chama tawala. Sina hakika kama mlifanya utafiti kufahamu kwa hakika chama hicho kimechoka kiasi gani au kama ni kweli kimechoka, ama ni simba aliyenyeshewa mvua tu!

Nne, kwa kutokana na kubweteka huko, Chadema mmejikuta mkijenga kiburi, dharau kwa wananchi. Pia mmejenga chuki na jazba za kizembe kwa kila anayeonekana kuwa na mtazamo tofauti. Ukitaka kufahamu hili, tembelea kwenye mitandao ya kijamii. Kila hoja pinzani inajibiwa kwa matusi ya nguoni badala ya ufafanuzi wa kisomi. Chadema ile ya mwanzo ya kina Bob Makani, Dr. Kabour, Zitto Kabwe na Dr. Slaa; CHADEMA ya akina Dr.Kitila Mkumbo, Prof. Baregu, Tundu Lisu, Prof. Safari, John Mnyika na wengine; Chadema tuliyoizoea na kuikubali kwa uwezo wa kujenga hoja na kujibu hoja kwa hoja za kisomi na kistaarabu imepotea ghafla. Sasa kuna makundi sijui yameanzishwa na nani maskini, wao ukiuliza tu taarifa ya fedha, utaambulia kutukaniwa viungo vyako vya uzazi au hata vya wazazi wako.

Ukiuliza tu mbona hili halijakaa sawa, utajuta kuzaliwa! Ni kama kakundi ka vijana waliotumwa na wazee wakorofi, na wote wakiwa ni watumiaji wazuri wa vitu fulani vinavyoharibu akili. Mwenye akili kwao ni yule tu anayesifia chama chao. Yeyote anayewakosoa ni adui, hana akili, katumwa na CCM, msaliti, kirusi n.k.

Kwa sasa imeibuka laana kubwa zaidi, ya kuvuana nguo wao kwa wao kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ukiona tuhuma nzito zinazoelekezwa kwa Zitto Kabwe utashangaa. Zitto ni Makamu Katibu Mkuu wa Chadema mwenye dhamana ya masuala yote ya utendaji wa chama kwa upande wa Tanzania bara. Watu wanamtuhumu mtandaoni, viongozi wa juu wa chama wamekaa kimya. Hawaungi mkono wala kukanusha tuhuma…Siku zinaenda!

Kwa bahati mbaya sana mnadhani kuna makundi mawili tu ndani ya Chadema, yaani lile la Mbowe na lile la Zitto Kabwe. Na mnajidanganya eti haya ndiyo makundi makubwa ndani ya Chadema. Hakika hamuijui hii nchi na wala hamna upeo mzuri katika kuchambua masuala mtambuka. Idadi kubwa ya watanzania ni ya wale wasio na chama (un decided). Ukitaka kujua hili angalia idadi ya wanachama katika vyama vyenu. Wakati watanzania tuko zaidi ua milioni 45 huku wapiga kura wakikaribia milioni 30, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa hawazidi milioni 10. Kwahiyo, wakati wanachama na wafuasi wa Chadema wakijigawa katika makundi mawili madogo, kuna kundi la tatu ambalo ni kubwa zaidi ya hayo mawili kwa pamoja. Hili ni kundi la hao’ undecided’..watu ambao husubiria mwelekeo wa chama ili kuamua kama wakiunge mkono ama la. Kwa kugawanyika, Chadema mna‘frustrate’ image ya chama na kuwakimbiza watu waliotarajia kuwaunga mkono. CHADEMA-Mbowe pekee haina ubavu wa kushindana na CCM na kutwaa dola. Na CHADEMA-Zitto Pekee wala isiote. Kama mnabisha waulizeni NCCR. Waliparaganyika wao, CCM ikapendeza!

Mwenye akili ndogo atasema, mbona CCM nako kuna makundi? Ni kweli, lakini CCM ni chama dola, kipo madarakani kwa umri wa Taifa la Tanzania, wameshazoea kushinda katikati ya migogoro. Lakini pia CCM wamethibitisha kuwa wanaweza kuwa wamoja linapokuja suala la kubaki madarakani. Hakuna wakati kulikuwa na mgogoro ndani ya CCM kama kipindi ambacho Kikwete (Rais) alipitishwa kwa mara ya kwanza kugombea, na akashinda kwa 80%+. Lakini pia haya ni mawazo ya kijinga tu, kuacha nyumba yako iungue kwakuwa hata ya jirani nayo inaungua? …Mvivu mwingine wa kufikiri alatela hoja ya ‘ukomavu wa demokrasia’. Huu nao ni utoto. Ukomavu wa demokrasisa ni mapambano ya hoja, sio shutuma za kilevi na mitusi kama vichaa. Kwa tabia hizi, mnapoteza uhalali wa kuaminiwa kupewa nchi!

Wakati ninyi mnaendeleza matusi kwenye mitandao, mnararuana mchana kweupe, mnaendeleza makundi na mipasuko ya kichawi, CCM wanaendela kutulia na kupanga mashambulizi kisayansi. Mwigulu Nchemba mliyezoea kumsikia akitoa shutuma za ‘kujilipua’ sasa anatumia muda mwingi kufungua matawi ya chama na kuimarisha yale ya zamani, vijijini. Katika mikutano yao wanazungumzia changamoto za ajira, umuhimu wa vijana kujituma na kuzifuata fursa na kuwaomba watanzania waendelee kukiamini chama hiki kilicholeta uhuru wa Tanganyika. Wakati vijana wa chadema mkivuana nguo mitandaoni, kina Januari Makamba wako ‘busy’ kwenye mashamba ya chai, pamoja na wakulima wao, wakijitahidi kwa pamoja, kutatua kero za wapiga kura wao.

Wakati wawakilishi wa Chadema wakitungiana nyimbo za mipasho kila kukicha, lile jukumu la kusimamia serikali na hata kuhakikisha bunge linaendeshwa kwa kanuni sasa limehamia kwa vijana wasomi wa CCM. Dr.Kigwangwala leo ndiye anakusanya saini za kumwajibisha Spika. Wakati mawaziri vivuli wa Chadema wakiwa ‘busy’ na kutafuta risiti feki za kupakaziana posho hewa, mawaziri wa CCM wako bize kujenga barabara, kuchimba visima vya maji, kujenga madaraja, kujenga shule kila kata, kuboresha mazingira ya watu kujitegemea na kujitafutia kipato. Na wakati wote, wakiwatahadharisha watanzania, kwamba CCM tu ndicho chama chenye nidhamu, wala hawahitaji kuonyesha ushahidi, kwani ushahidi tunauona Facebook na Jamii forum.

CCM wanahitaji utulivu tu, wala wasiingie kwenye mkumbo wa kujibizana kihuni na hawa waliojipambanua tayari kuwa wahuni. Waendelee kutekeleza ilani yao ya uchaguzi. Katika muda uliobaki, Mwenyekiti na sekretarieti yake wafanye maamuzi magumu. Waendelee kuwatumikia watanzania kwa unyenyekevu mkuu. Waendelee kusimamia vyema utajiri wa gesi, mafuta, urani, madini na utalii. Waandaeni wagombea wachapakazi. Nasisitiza WACHAPAKAZI kwani kwa umaskini wa nchi yetu kwa sasa hatuhitaji malaika kutuongoza.Hakuna mwanasiasa msafi Tanzania, tunahitaji kiongozi mwenye uthubutu, mwenye umakini na mwenye kufuatilia mambo. Kiongozi mwenye upeo wa kubuni na kusimamia mipango. Mwenye kusimamia vema timu yake ya ushindi. Kiongozi mwenye kuwaheshimu watu na kuwatumikia mchana usiku. Kisha mshikamane, punguzeni makundi, muwe kitu kimoja. CCM mkifuata ushauri wangu na Chadema mkiendelea na dharau zenu, uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani utasimika maana ya ujumbe wa msingi unaoletwa na makala hii.

HITIMISHO

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, “Ukipewa kazi ya nchi lazima ujiheshimu”
Vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuheshimu wananchi. Viongozi wanaochaguliwa na watu wanapaswa kuwa na adabu kwa waliowachagua. Kama chama tawala kilivyojidanganya kwa kudhani watanzania ni wajinga na wakidhani wangetawala milele, ghafla wakashtukia watu wamemka na kuweka rehani utawala wao wa milele. Vyama vya upinzani navyo visilewe ulevi ule ule. Na ni hatari sana kwa watu kulewa madaraka ya chama tu, siku tukiwakabidhi nchi itakuaje?

Watanzania wa leo si wale wa miaka ile. Watanzania wa leo wanaaangalia TV, wanatumia computer, I-Pad, smart phones, wako facebook, twiter na kwingineko. Wanasafiri wanaona. Wanajifunza wanaelewa. Wengi wetu hatuko katika makundi ya ‘wafia chama’. Tunachambua kila habari, tunatafakari kila neno. Wanafalsafa wa mlengo wa ‘Sophist’ wanatuelekeza kuhoji kila kitu. Hakuna NDIYO ya milele wala HAPANA ya milele.

Sisi sio misukule kwamba tutahudhuria kila midundiko yenu bila kujua ina faida gani kwetu. Tukiwauliza swali tunategemea majibu, sio matusi. Tukileta hoja tunategemea ‘data’ sio umbea! Tumewaweka mioyoni ninyi mkatutupa jalalani. Tumewaamini na kuwapenda upeo, mkalewa na kutudhihaki! Mlikuja kutuomba kura mikono ikiwa nyuma leo tukihoji utendaji wenu mnatutukana?!. You have disappointed us! Tumevunjka mioyo, tumechanganyikiwa mno, Tumekasirika Sana! NA MKIENDELEZA DHARAU........... TUTAWAADHIBU VIKALI SANA!





Mwandishi wa Makal hii ni Mtafiti, Mwanasosholojia na Mtaalamu wa uandishi, uandaaji na usimamizi wa Miradi. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Mwaka wa tatu Shahada ya Sheria, Pia ni Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro.(MUSO-SECRETARY GENERAL).Anapatikana kwa Email: rlengeju@yahoo.com au Simu # 0715901001/0762341522
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Vijana werevu wameshatambua hilo na wanajitoa mmoja baada ya mwingine.

Mazezeta ndio yanabaki yakitumika kama miili ya maandamano tu...
 
Wakati wawakilishi wa Chadema wakitungiana nyimbo za mipasho kila kukicha, lile jukumu la kusimamia serikali na hata kuhakikisha bunge linaendeshwa kwa kanuni sasa limehamia kwa vijana wasomi wa CCM. Dr.Kigwangwala leo ndiye anakusanya saini za kumwajibisha Spika. Wakati mawaziri vivuli wa Chadema wakiwa ‘busy’ na kutafuta risiti feki za kupakaziana posho hewa, mawaziri wa CCM wako bize kujenga barabara, kuchimba visima vya maji, kujenga madaraja, kujenga shule kila kata, kuboresha mazingira ya watu kujitegemea na kujitafutia kipato. Na wakati wote, wakiwatahadharisha watanzania, kwamba CCM tu ndicho chama chenye nidhamu, wala hawahitaji kuonyesha ushahidi, kwani ushahidi tunauona Facebook na Jamii forum.

Vijana werevu wameshatambua kuwa kujishughulisha na harakati za Chadema ni kupoteza muda kwa manufaa ya wachache.

Posho yote ya mabilioni ya shilingi inaishia makao makuu. Wilaya hazipati hata shilingi!

Wanaojitolea kujenga chama mawilayani wakitoa maoni juu ya mwenendo wa chama, hakuna anayewasikiliza!

Watu wa makao makuu wanalipana posho kwa kila wanachofanya, wamekuwa kama wabunge.

Pesa za ruzuku tu wamelewa kiasi hiki!!! Dola hawaiwezi hawa...
 
Tupeni dola tuwanyoshe mafisadi mnao waogopa maccm.
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Vijana werevu wameshatambua hilo na wanajitoa mmoja baada ya mwingine.

Mazezeta ndio yanabaki yakitumika kama miili ya maandamano tu...

Mje na propaganda mpya hii imechuja na hawasaidii.
 
chadema ipo imara kuliko watu wanavyofikiri.

Mungi mbona unatoa kauli ya kukata tamaa mno.

Chama sio jeshi. Uimara wa chama sio siri unaonekana mitaani. Njoo vijiweni usikie watu wanaongea nini.

Watu hawajafurahishwa kwa jinsi watu fulani kuwa above the law na kufanya chochote wanachotake huku wengine wakipewa adhabu bila hata kupewa nafasi ya kujieleza. Jambo hili ndio lililoiua Chadema.
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Vijana werevu wameshatambua hilo na wanajitoa mmoja baada ya mwingine.

Mazezeta ndio yanabaki yakitumika kama miili ya maandamano tu...
Ni kweli kama viongozi wa juu Mhe Mbowe na Dr Slaa hawatachukua hatua mara moja wanachama tumechoshwa na hizi aibu za wanachama kufukuzwa kama kuku tena wengine wanapigwa bila hatua kuchukuliwa,wanachama wenye busara wengi wamebaki wakiangalia anguko la chama.
 
Mleta mada umetoa mawazo na ushauri wa ujenzi lakini tegemea matusi na kejeli kutoka pro-Chadema.
 
makala yako ni nzuri sana,nimeipenda sana,wale wakombozi hakika si wakombozi tena
 
Nadhani hili ni somo zuri kwa akina slaa, mbowe na zitto..kwa mwenye kiburi huja majuto kwa mnyenyekevu huja neema. Chadema kina nafasi ya kurudi kwenye mstari kwa sasa hata mimi nakubali chama hakiko katika mstari sahihi kwa bahati mbaya uwingi wa wabunge wa chadema bungeni haujawa na faida sana kwa sababu ni wachache wenye kujenga hoja na kupambana kama ilivyokuwa kabla ya 2010, ubabe nao umeathiri haiba ya chama, imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya chadema wengi wameanza kujiuliza maswali, naamini kama hatutabadilika chama hakina mwendo mrefu.
 
Kinachoendelea ndani ya CHADEMA sasa hivi sio tu kinakishushia hadhi chama hicho bali pia kinawafanya Watanzania walioanza kukiamini chama hicho wajione kama ‘wameingizwa mkenge'
 
Ritz; Mbona mimi nampongeza kwa makala yenye lengo la kuimarisha chama, usikariri Mkuu! Wahenga walisema mficha maradhi, kifo humuumbua!
 
Last edited by a moderator:
Ritz; Mbona mimi nampongeza kwa makala yenye lengo la kuimarisha chama, usikariri Mkuu! Wahenga walisema mficha maradhi, kifo humuumbua!
 
Last edited by a moderator:
Ritz; Mbona mimi nampongeza kwa makala yenye lengo la kuimarisha chama, usikariri Mkuu! Wahenga walisema mficha maradhi, kifo humuumbua!
 
Last edited by a moderator:
chadema ipo imara kuliko watu wanavyofikiri.

af mijitu mingine bana sijui inatazama kwa makalio? chama kipo imara mnavuana nguo mitandaoni? katibu mkuu wa chama ana like jumbe zinazomponda naibu wake? eti chama kipo imara? we utachukuliwa mkeo ukidhani uko nae b.w.e.g.e. we!
 
Kuna tofauti moja ya msingi kati ya vyama vilivyowahi kuwa juu miaka hiyo yaani NCCR, TLP na CUF na hiki kilichosimama miaka ya hivi karibuni, yaani CHADEMA. Tofauti hiyo ni kwamba, wakati vile vingine vikitegemea zaidi nguvu ya waasisi wake ama watu Fulani maarufu katika kuimarisha ukubalikaji wake mbele ya jamii, CHADEMA kimejijenga haraka kimfumo, kikiwa na umaafuru wa ki-CHAMA, sio jina la mtu, japo kuna majina makubwa makubwa yanayoongezea umaarufu wake.


hapa naomba ntofautiane na wewe,haijawahi na haijatokea cdm wakajijenga kimfumo hata siku moja,haya ya mtandaoni na unayoyapigia kelele kwenye makala yako yasingetokea,tuhuma za mwenyekiti kuteua viti maalum uchagani sio mfumo imara,kuuza magari chakavu kwa chama sio mfumo,mwenyekiti kuwa mtia saini kutoa pesa za chama benki huo sio mfumo wa kujenga,maamuzi mengi ya kibabe ya mbowe disko joka hayatokani na mfumo,bali ulevi wa viroba pale club bilicanas
 
af mijitu mingine bana sijui inatazama kwa makalio? chama kipo imara mnavuana nguo mitandaoni? katibu mkuu wa chama ana like jumbe zinazomponda naibu wake? eti chama kipo imara? we utachukuliwa mkeo ukidhani uko nae b.w.e.g.e. we!

Ha ha ha ha ha!!Unanivunja mbavu mkuu!!!Wasamehe bana wenzio wanakaririshwa kila kitu vichwani mwao na wenyewe hawanaga muda wa kuchambua wanakuja wanayamwaga kama yalivyo tu hapa mtandaoni.
 
Back
Top Bottom