Mbowe kutikisa Shinyanga kesho Jumamosi

Mbowe kutikisa Shinyanga kesho Jumamosi

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kesho ataongoza maelfu ya wananchi katika uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki.

Uzinduzi huo utafanyika mjini Shinyanga ambayo ni ngome kuu ya Chadema kwa ukanda huo.

Kanda ya Ziwa Mashariki inajumuisha mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu.

Uzinduzi huo utatanguliwa na maandamano makubwa yakifuatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara.

Leo Mbowe aliongoza viongozi zaidi ya mia mbili wanaounda Kanda hiyo kutoka majimbo yote katika kikao cha kupanga mikakati.

Mwenyekiti Mbowe kwa wiki zaidi ya tatu sasa amejichimbia mikoani katika kanda mbalimbali za Chadema akiwajengea uwezo viongozi wa ngazi za chini,akifungua mashina na ofisi za chama,akipokea maelfu ya wanachama wapya vijijini na akihutubia mikutano ya hadhara kutangaza sera za Chadema.
 
Kazi nzuri Mh. Freeman Mbowe nadhani maandalizi ya kuelekea 2015 yanaendelea vizuri. CCM bado wanaumana wao kwa wao. Sijui ni lini Hamis Mgeja aliitisha maandamano ua kuhutubia hao wananchi wa Shinyanga.
 
Wao wakizidi kupika propaganda Chadema inaendelea kuchanja mbuga
 
Kuelekea 2015,cdm muwe na solution ya matatizo haya vijijini:- 1)migogoro kati ya wakulima na wafugaji ipo kila kijiji.2)kuna njaa kila kijiji huku kukiwa na maeneo mazuri ya kilimo kipindi cha masika tuu.3)kuwepo na shule za msingi na zahanati bila ya kuwepo waalimu na madaktari.4)vijana wote kukimbilia mijini kuendesha bodaboda zinazowaua kila kukicha ajali.5)soko la uhakika kwa bei nzuri ya mazao ya wanavijiji eg wakulima pamba,korosho wamekata tamaa.6)cdm iwe na mchanganuo wa kila kijiji nini kifanyike ktk kukuza uchumi wa sehemu husika kutokana na resources zilizopo.7)kutoa suluhu ya huduma za maji,barabara kwa kila kijiji
 
karibu sana tunataraji utakua n MKUTANO wa khstoria na mapnduz kwel
 
Kuelekea 2015,cdm muwe na solution ya matatizo haya vijijini:- 1)migogoro kati ya wakulima na wafugaji ipo kila kijiji.2)kuna njaa kila kijiji huku kukiwa na maeneo mazuri ya kilimo kipindi cha masika tuu.3)kuwepo na shule za msingi na zahanati bila ya kuwepo waalimu na madaktari.4)vijana wote kukimbilia mijini kuendesha bodaboda zinazowaua kila kukicha ajali.5)soko la uhakika kwa bei nzuri ya mazao ya wanavijiji eg wakulima pamba,korosho wamekata tamaa.6)cdm iwe na mchanganuo wa kila kijiji nini kifanyike ktk kukuza uchumi wa sehemu husika kutokana na resources zilizopo.7)kutoa suluhu ya huduma za maji,barabara kwa kila kijiji

Umeongea vema sana.Point Noted.
 
ama kweli Chadema wako vyema sisi ngoja tuendelee kukomaa na akina
hugo humu jf.

Endeleeni huko na makamanda waendelee kuwa Field.
 
Last edited by a moderator:
kama kawa,
wakati wao wanaendelea kutengeneza clip sisi tunavuna wanachama
 
ama kweli Chadema wako vyema sisi ngoja tuendelee kukomaa na akina
hugo humu jf.

Mkuu habari za kuaminika ni kwamba Hugochaves ni Mwigulu na Bukoba boy ni nape; Pamoja na hao, kuna group kubwa la vijana wa Kawa-mbwa waliokubali akili zao kuwa-controlled na remote za Lumumba baada ya kutaga mayai kwenye mtihani wao wa kidato cha nne, wamevamia humu JF the same day na hao mabwana zao wa Lumumba walipo badili ID zao, kwa kazi maalumu ya kuipigia upatu clip yao ya kichina, nimeamini kweli elimu ya bongo ni matatizo, kwani wanacho kiandika hawa misukule ni dhahili hata wao wenyewe hawakielewi, sijui ndo matatizo ya kutokuwa na mitaala inayoeleweka?
 
Huwa ninaamini sikuzote Mungu hawezi kuruhusu Baali ajitwalie utukufu.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kesho ataongoza maelfu ya wananchi katika uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki.

Uzinduzi huo utafanyika mjini Shinyanga ambayo ni ngome kuu ya Chadema kwa ukanda huo.

Kanda ya Ziwa Mashariki inajumuisha mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu.

Uzinduzi huo utatanguliwa na maandamano makubwa yakifuatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara.

Leo Mbowe aliongoza viongozi zaidi ya mia mbili wanaounda Kanda hiyo kutoka majimbo yote katika kikao cha kupanga mikakati.

Mwenyekiti Mbowe kwa wiki zaidi ya tatu sasa amejichimbia mikoani katika kanda mbalimbali za Chadema akiwajengea uwezo viongozi wa ngazi za chini,akifungua mashina na ofisi za chama,akipokea maelfu ya wanachama wapya vijijini na akihutubia mikutano ya hadhara kutangaza sera za Chadema.

Safi sana Bw. Mbowe, umeomba kibali, umepewa na sasa una uhuru ya kufanya maandamano halali, mpaka kieleweke!
 
Absalom Kibanda Jicho lake moja limetolewa baada ya jitihada za KULIOKOA KUSHINDIKANA.
 
Makamanda tunawaombea kila raheri kwa maandalizi ya kuchukua hatamu za uongozi wa Taifa letu linaloibiwa kila kukicha.
 
Back
Top Bottom