Mkuu
TataMadiba usiseme kwa nguvu,maana utakuwa unamsema pia na yule mwingine.Maana alivyopewa Pound Milion 2.7 na Balozi wa Uingereza kusaidia Wahanga wa Tetemeko,alisema Uingereza wametupa hela hizo baada ya kuona tumewatumbua wale akina RAS na DED wa Bukoba.Hivyo wameona pesa wanayotupa inafanya kazi.
Mkuu akasema ataendelea "kutumbua" ili watusaidie kwenye maeneo mengine ya maendeleo maana wanajua hela zao wakitupa zinatumika ipasavyo.
Wewe ni mkongwe,unajua nini maana ya "International Relation and Dipolomacy"...Kila chama na nchi ktk Afrika huwa na "marafiki" nje ya mipaka ya nchi zao.
Mfano CCM rafiki yao mkubwa ni Chama cha Kikomunisti cha China,matatizo yao huyapeleka China,iwe ya kifedha au ya kisera.Hao wachina ndio CCM imewapelekea ombi hicho chama cha Kikomunisti kiwajengee chuo cha chama mbadala wa Kivukoni,chuo kitajengwa Ihemi-Iringa kwa msaada wa Wachina.
Ndio hao hao Makonda kaenda kuwaomba na sasa watajenga uwanja wa nyasi bandia pale chuo cha Utalii(bandari Tandika) kwenye uwanja wa "Ndondo Cup".Wakorea juzi wamesema watajenga daraja la kutoka Coco mpaka Agha Khan na mkuu wa nchi akasema ni msaada wa kujivunia.
Hawa Chadema kama chama,nao wana marafiki huko nje,urafiki haimaanishi "Ukooloni" bali "Uswahiba" tu,au kilicho halali Lumumba basi Ufipa ni haramu?