Mbowe kaanza vizuri kwa kuhubiri uzalendo

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,118
7,701
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tangu ameachiwa huru mazungumzo na mahubiri yake yamekuwa ni kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja na kuipenda nchi yao kwanza, amekuwa akisisitiza kuwa "siasa ni chombo tu cha kutufikisha kwenye matamanio yetu" hivyo itikadi zetu za kisiasa kamwe zisitigawe.

kwa mwendo huu ameanza vizuri, asije kupotoka mbele ya safari aende hivyo hivyo kwa msilahi ya watanzania.

Uzalendo, Amani na Haki.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tangu ameachiwa huru mazungumzo na mahubiri yake yamekuwa ni kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja na kuipenda nchi yao kwanza, amekuwa akisisitiza kuwa "siasa ni chombo tu cha kutufikisha kwenye matamanio yetu" hivyo itikadi zetu za kisiasa kamwe zisitigawe.

kwa mwendo huu ameanza vizuri, asije kupotoka mbele ya safari aende hivyo hivyo kwa msilahi ya watanzania.
Uzalendo, Amani na Haki.

Hatimaye mmefika bei. Si mmejaribu huku:

IMG_20220309_074636_371.jpg


Mkajaribu na huku pia?

IMG_20220309_201907_744.jpg


Kama mfa maji vile.

Hiiiiii bagosha!
 
Wanasiasa wote matamanio yao yanafanana, kitendo cha Mbowe kutinga Ikulu baada kutoka jela Mama lazima amemwaidi vitu vizuri...

Na Mama hapendi kelele hivyo Mbowe atakuwa ameaidiwa kuanzia kwenye biashara zake hadi kwenye siasa kuwa utapewa kila kitu ila watulize hawa watu wako.
 
sula la msingi hapa ni kuitanguliza nchi yetu Tanzania mbele sio Chama cha siasa au mtu yeyote.

sisi sote ni watanzania kamwe tusibaguane au kuchukiana eti kisa siasa.....ni ujinga!!

Tulumbane kwa hoja sio matusi na kejeli, wanasiasa wetu watoe hoja za kuijenga nchi yetu, kutatua Kero za wananchi na kuleta maendeleo.

wanasiasa wahimize umoja na ushirikiano ktk kuijenga nchi na sio kutugawa.
Rais wetu Samia katuonyesha njia na nia thabiti.....sasa yatupasa sote tuifuate.

Wananchi tunataka maendeleo na kero zinazo tukabili zitatuliwe au kutoa mawazo na njia bora za kuzitatua.

Utulivu wa kisiasa ni njia pekee ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Heko sana kwa Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kuliona hilo.
 
Mbowe ameanza kuonyesha ukomavu wa kisiasa.
naamini ameamua kubadili gia,
ndio maana amewashangaa wanao mbeza eti asinge kutana na Mhe. Rais....kwa madai eti ameonewa!!.......Mbowe kawajibu kua
"wengi walitegemea eti baada ya kuachiwa niwe na hasira na nianze kulaumu...hasira....hasara..." tuijenge nchi yetu.
Hongera kwa Mbowe., kazi iendelee Taifa lisonge mbele.
 
maadui wenye kuiombea nchi yetu mabaya watabaki wanapiga miayo.
Umoja ni nguvu........................mshokamano wetu ndio nguvu kwa Taifa letu.
tushikamane kuijenga nchi yetu bila kujali wewe ni chadema, cuf, ccm n.k, sisi sote ni watanzania,, Baba yetu mmoja na Mama yetu ni mmoja tu.
 
wapo watakao nuna upande wa Chadema na hata vyama vingine kwa kuwa Mbowe kakutana na Mhe. Rais Ikulu, lkn wale wote wanao itakia mema nchi kamwe hawawezi kununa wala kuvimba kwani Rais wa Watwnzania wote kaonyesha njia ya Umoja na Ushirikiano wa kuendelea kuijenga nchi yetu pamoja.
 
Back
Top Bottom