Mbowe in informal meeting with JK

Mbowe in informal meeting with JK

shehe yahya jr alisema mwaka huu kikwete atangara kwa kuwahisisha wapinzani katika seriikali tusubiri,pili hiyo ni karata nzuri lwa cdm kwa hali ilivyo huwezi kuiondoa ccm madarakani yoooote overnight
 
Kwa wanaojua kanuni ya kutafuta Power hii ni bonge ya Opportunity uwezi kuiondoa CCM overnight yataka mchakato tena makini sana,kwa kuwa ndani ya CCM ya miaka 50 ukiuunganisha miaka ya TANU na CCM kuna watu wameshakuwa walevi [addictive] wa madaraka kwa tiketi ya CCM,kiasi kuwa hawaamini watu wengine wanotoka nje ya CCM,kumbe Tanzania ni yetu sote,Na kuwa hata mawaziri wangeweza kutoka Nje kabisa ya Wabunge.Kwa wasomi wanajua madaraka ni kilevi [Opium] hivyo muhusika kama hana busara ujisahau ukiongeza na uafrika ndio usiseme ni balaa kwa kwenda mbele.

Sioni tatizo kwa CDM kuteam up na jakaya kwenye level ya kugawiana baadhi ya wizara potential ambazo zitajenga sheria na kusimamia sheria,na pia zitawapa CDM nafasi ya kupima uwezo wao,wa kutawala.Kwa watu makini Tanzania wanajua kuwa CDM pia iliitaji kukua na kuaminika kwa watu wake kuwa na uwezo wa kujiorganize kama Government Team ya watu ambao wana collective responsibility.Hayaji hivi hivi yanaundwa jamani.

Siasa za Tanzania sio kama za Kenya, sometimes maisha ya binadamu hayafanyiwi majalibio japo kuwa baadhi ya watawala wetu ndani ya CCM wametufikisha sehemu tunaamini kuwa wanatufanyia majaribio kwenye maisha yetu.
 
Muafaka kwani ni kitu gani jamani... sielewi? mm nijuavyo ni kuwa lazima pawepo na vita au ugomvi phisically ndo maridhiano yanapotokea tunayaita muafaka, nahisi ss tuna-mapishano ya kauli za kisiasa na hata USA, UK na nchi nyngine zlzoendelea ipo hvyo ss mnaposema muafaka ni upi au unahusu nn, kwamba Mbowe aache mapambano ya kisiasa au......?

Unadhani maanadamano kila kukicha hakutaki muafaka?
 
Sikuona uharaka wa hawa Citizen kuandika hii habari wakati wameambiwa wasubiri msiba uishe wapate habari kamili..hizi habari nusunusu mi naziona hazina uzito...

Habari kwao ni kwamba kulikuwa na mkutano wa siri. Yalijiri yaje baadaye. Kama mtu aliweza kufanya mkutano wa siri wakati wa msiba ni kwa nini asiseme walichokiongea wakati huo huo ati hadi wasubiri msiba uishe! Naona muafaka uko njiani!
 
Nakubaliana na Mhadhiri Bashiru Ali, ktk siasa hakuna siri.
Mbowe asituchanganye, sisi wanachadema tuna hamu ya kusikia kutoka kwake na kwanini alienda kwa siri. Je, viongozi wenzake akina Dr Slaa wanajua hilo? Benefit of doubt.

Mbowe amesaha sema atazungumza baada ya mazishi, hivyo siyo siri tusubili. si unajua jamaa nchi imesha mshinda? l
 
Habari kwao ni kwamba kulikuwa na mkutano wa siri. Yalijiri yaje baadaye. Kama mtu aliweza kufanya mkutano wa siri wakati wa msiba ni kwa nini asiseme walichokiongea wakati huo huo ati hadi wasubiri msiba uishe! Naona muafaka uko njiani!

Hapo hakuna muafaka. Tofautisha ccm b na CHADEMA. cuf ni ya maalimu seif peke yake, yeye ndo ana maamuzi ya chama. lakini CHADEMA si ya mbowe peke yake
 
Habari hii imeandikwa kwa lengo ovu .......na ni mkakati wa baadhi ya watu ndani ya serikali na ndani ya vyama vya siasa yaani CCM na CDM kutaka kukwamisha ama kuchafua hali ya hewa kwenye vyama husika.

Kama Mbowe , alienda kumjulisha rais kuhusiana na taratibu za msiba wa Regia itakuwaje? kwani ni siku hiyo hiyo na baada ya muda JK kaenda nyumbani kwa familia ya marehemu kutoa pole? Badop naungana na wengine waliosema kuwa tuvute subira kwani Mbowe kaahidi kuwa atasema baada ya msiba ama walikutana na nini walichokuwa wanazungumzia .

Gazeti hili ndio hilo hilo limeandika uwongo mwingine kuwa marehemu Regia ndio alitoa hoja kwenye kamati kuu juu ya kukutana na JK , ila ukweli ulikuwa kuwa hilo lilikuwa pendekezo lililotolewa na Secretariat ya chama kati ya mapendekezo 3 yaliyopelekwa kwenye kamati kuu .

Kiranja,

Una maana naibu katibu mkuu Zitto hakusema kweli? Maana hata humu JF hakusema kwamba pendekezo la kumuona Kikwete kumshauri asisaini sheria lilitolewa na sekretariati. Sasa tusibishane kwa kuwa kamanda wetu bado hatujampumzisha lakini tukimaliza maombolezo itabidi tuelezwe ukweli.

serayamajimbo
 
Nitaendelea kuipiga vita ccm mpaka nihakikishe inatoka madarakani hata kama chadema wakinunuliwa na ccm
 
Mbowe mbona anajirahisisha kwa huyo jamaa.. Dr. Slaa awezi kufanya jambo kama hilo. Period

uongozi wa chama si kitu cha mchezo, kuna wakati wa kutumia nguvu nyingi, kuna wakati wa kutumia akili zaidi,,, alimradi mambo yaende. kama uongozi ingekuwa ni suala la msuli basi leo dr slaa angedai haki yake kwa nguvu wengi wangeishakufa...

cha msingi unapokuwa kiongozi unaweka maslahi binafsi pembeni na unakuwa kama dereva....kutumia uwezo, ummarufu na mahusiano yako kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wengi....si lazima kupitia vurugu tu....

naamini kabisa mbowe akitumia heshima aliyonayo kikwete kwake (hawakukutana barabarani hawa)....wanaweza kutupeleka pahala pazuri kiuchumi na kijamii kama taifa!
 
Nitaendelea kuipiga vita ccm mpaka nihakikishe inatoka madarakani hata kama chadema wakinunuliwa na ccm

You sound like umekata tamaa.
Hivi je kama ukipewa nafasi tuseme huwe waziri wa nishati na madini je utafanya nini au sheria ama waziri mkuu?

Je utachukua kazi na kutumikia nchi yako kufanya mabadiliko,au utataka ubaki pembeni na kuendelea kulalamika.Kama mimi napiga mzigo safi nikionda obstacle katika kupitisha mambo ya msingi milango wazi kuresign ...mbaya ni ku kuunda serikali ya kitaifa na kuendelea kutenda kama wao wanvyotenda..na ukiona hivyo basi huyo chama chake naye kingepewa dola yangekuwa yale yale
 
Hapo hakuna muafaka. Tofautisha ccm b na CHADEMA. cuf ni ya maalimu seif peke yake, yeye ndo ana maamuzi ya chama. lakini CHADEMA si ya mbowe peke yake

Mkuu CUF ni ya wanachama kama ilivyo CDM. Mazungumzo ya CCM na CUF yalianza kwa siri kati ya Maalm na Karume!!
 
Habari hii imeandikwa kwa lengo ovu .......na ni mkakati wa baadhi ya watu ndani ya serikali na ndani ya vyama vya siasa yaani CCM na CDM kutaka kukwamisha ama kuchafua hali ya hewa kwenye vyama husika.

Kama Mbowe , alienda kumjulisha rais kuhusiana na taratibu za msiba wa Regia itakuwaje? kwani ni siku hiyo hiyo na baada ya muda JK kaenda nyumbani kwa familia ya marehemu kutoa pole? Badop naungana na wengine waliosema kuwa tuvute subira kwani Mbowe kaahidi kuwa atasema baada ya msiba ama walikutana na nini walichokuwa wanazungumzia .

Gazeti hili ndio hilo hilo limeandika uwongo mwingine kuwa marehemu Regia ndio alitoa hoja kwenye kamati kuu juu ya kukutana na JK , ila ukweli ulikuwa kuwa hilo lilikuwa pendekezo lililotolewa na Secretariat ya chama kati ya mapendekezo 3 yaliyopelekwa kwenye kamati kuu .

Mkuu soma hapa ujue kama ni Gazeti ama ni Mjumbe mwenzake wa CC aliyesema hayo

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/212834-nakuagaje-regia-zitto.html
 
Mkuu soma hapa ujue kama ni Gazeti ama ni Mjumbe mwenzake wa CC aliyesema hayo

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/212834-nakuagaje-regia-zitto.html

Kimbunga,

Inaelekea huyo mjumbe wa CCM hajasema ya kweli, kabla ya CCM ya CHADEMA huwa kuna kikao cha sekretariati. Kama ni kweli hilo pendekezo lilikuwepo kwenye nyaraka iliyowasilishwa na sekretariati kama ilivyoelezwa hapa JF basi mjumbe wa CC hakusema kweli. Alipaswa kusema kwamba Marehemu amekuwa na mchango mkubwa wa kukubaliana na sekretariati kuhusu kukutana na Rais.

serayamajimbo
 
mkutano gani tena wa siri wakuu, wakati tuna msiba mzito? asije (jk) akapendekeza tuunganishe vyama ili kuongeza kasi ya maisha bora kwa kila m-tz kuelekea 2015-- :lol:

Itakuwa ndoa hiyo.
 
JK na Mbowe ni marafiki wa siku nyingi na ninadhani JK hawai kurudisha kadi ya CDM aliyoichukuwa 1995 na kuilipia hadi 2005! Hata hivyo hao wote wawili ni Watanzania huru wenye haki yao kikatiba kukutana na hata kunywa kahawa pamoja, jambo lolote linaloongelewa kati ya wawili hawa bila kutumwa na vikao vya vyama vyao ni mambo yao binafsi hata kama yanahusu vyama vyao.

Kama hawataki kutwambia ni sawa kabisa, lakini nasisitiza kuwa kama tunataka maendeleo ya kweli lazima tusiwe mashabiki wa watu, hasa wanasiasa bila kuweka vigezo na vipimo vya nani tunataka atutawale na kwa staili gani na mwendo kasi upi.
 
Ingekuwa aliekutana na Rais ni Zitto kabwe sijui comment za wadau ingekuaje?
 
Muda si mrefu ntarudisha kadi yangu ya CHADEMA maana mambo haya ya vikao vya siri ndiyo yaliyoifikisha CUF hapa ilipofikia. Ole wako Mbowe na vikao kao vyako vya siri vya kutaka kutusaliti kwa kuhongwa Vyeo.
 
Kuna uzi mmoja uliwahi andikwa humu jamvini uliokuwa ni tetesi juu ya mkuu wa wadanganywa kubadirisha BARAZA LA MAWAZIRI ifikapo mwezi wa tatu. Kutokana na kikao cha siri kilichofanyika kati ya mkuu wa wadanganywa na yule mkuu wa magwanda, nahisi walikuwa wanakubaliana kuhusu wabunge wa magwanda washirikishwe katika hilo baraza la mawa ziri. Msiniulize sosi maana sosi ni hisia zangu tu.
 
Back
Top Bottom