Mbowe hawezi kukwepa lawama za kukosa adabu na kutukana matusi ya nguoni kunakofanywa na vijana wake wa CHADEMA

Zamani ulikuwaga unajenga hoja nzuri sana huku jukwaani.lakini siku hizi sijuwi umepatwa na nini? Mimi nahisi labda anayetumia jina na ID hii kwa sasa siyo yule wa awali .

..hali ngumu ya uchumi na uchumi ya wananchi haimhusu Samia na chama chake?
 
Mtei alimuachia chama Bob makani ambaye huyo Bob makani alikuwa ni shemeji yake Mtei kwa kuwa mdogo wake na Mtei alikuwa ameolewa na Bob makani....
Hivi huu Uongo Huwa mnautoa wapi?

Nani anawalisha hizi propaganda?

Mbona mnapotosha sana?

Mke wa Bob makani namfahamu vizuri Sana kwanza ni mtu anayefahamika Tanzania Kwa sababu ya kuvunja Record ya kusoma akiwa na umri mkubwa kaongeza Elimu akiwa na miaka 70s..

Namjua Makani Tangu Mwaka 1992 Na 94 Namjua hata aliposimamia Kesi ya Yule Mbunge wa Upinzani wa Kwanza Tanzania Kule kigoma! Mwaja 1992-1994..

Sijamsoma kwenye Vitabu kama wewe Najua uwezo wake Tangu akiwa kaimu Gavana mkuu wa Tanzania..
Najua pia alipokuwa anagombea Ubunge Shy akisimama na Mwanaderefa..miaka ya 95 mpaka 2000..

Mke wa ke Makani anaitwa Vickie Ambwene Joab Kakuyu Makani
Ni mnyakyusa wa Mbeya..
Sasa Tangu lini Mnyakyusa akawa na Undugu na wachaga?

Makani ni Msukuma wa Shy na Mke wa makani ni Mnyakyusa undugu na mtei unakujaje?

Play that Stupid Propaganda cards with yo fellow kids.. Sio kwangu Mimi..
 
..jibu swali.

..Samia na Ccm wanahusika na hali ngumu ya maisha na uchumi inayowakabili Watanzania?
Kazi ni kipimo cha utu.fanya kazi acha kupiga Makele yako humu jukwaani.wanzako wanaendelea kupiga hatua za kimaendeleo wewe unabaki unalalamika hapa.maendeleo yapo katika juhudi za mikono yako mwenyewe.
 
Wanaoshindwa kutumia lugha za staha na hekima kwa watu wanaotofautiana nao ndio wahame hapa nchini ,maana kama Taifa hatuwezi tukawa na mawazo sawa na kufikiri kwa namna moja kama ambavyo CHADEMA wanataka.acheni matusi.
Ila mkipora chaguzi za nchi hiyo ni heshima kuliko matusi.
 
Kama Mdude Nyagali ndio kabisa .akili yake ni kama haipo katika hali ya ubinadamu maana huwa hafikirii wala kuwaza Kabla ya kuandika au kusema jambo.yeye ni kuropoka ropoka tu chochote kinachomjia katika mdomo wake.
Kwa taarifa yako, Mdude ana point kuliko ww, ila hana muda na point za kujipendekeza kwa viongozi. Na kwako mtu asiyejipendekeza kwa Hawa viongozi majizi ya kura, huyo ana matusi.
 
Kwa taarifa yako, Mdude ana point kuliko ww, ila hana muda na point za kujipendekeza kwa viongozi. Na kwako mtu asiyejipendekeza kwa Hawa viongozi majizi ya kura, huyo ana matusi.
Ile mimatusi ndio unazoita hoja?
 
Kazi ni kipimo cha utu.fanya kazi acha kupiga Makele yako humu jukwaani.wanzako wanaendelea kupiga hatua za kimaendeleo wewe unabaki unalalamika hapa.maendeleo yapo katika juhudi za mikono yako mwenyewe.

..kama wananchi waliowengi wamekwama kwenye lindi la umasikini, na huduma za serikali ni za kiwango cha chini, maana yake ni kwamba serikali, na chama kilichoshika madaraka, wameshindwa ktk majukumu yao. Ndio maana tunasema Rais Samia, serikali, na chama chao, hawafai.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Wakati mwingine huwa ni aibu sana,fedheha kubwa sana pale unapoweza ukawa unasikiliza mkutano wa hadhara wa CHADEMA unaohutubiwa na vijana wake huku mitaani.kiukweli inasikitisha sana na inaleta maswali mengi sana kichwani juu ya maadili ya kiuongozi yanayotolewa na kufundishwa ndani ya CHADEMA kwa vijana wake ambao ndio viongozi wa kesho.

Kinachokuwa kinatawala na kutoka katika vinywa vya vijana hao huwa ni matusi matupu tena matusi ya nguoni,ni lugha za ukakasi na za aibu kubwa sana ambayo unakuwa unaona wewe unayesikiliza.huwa najiuliza mimi binafsi kuwa hivi hawa vijana hawawezi kuzungumza na kujenga hoja bila kutukana matusi kwa viongozi wetu na watu wengine? Kwamba Huwa haiwezekani kupeleka na kufikisha ujumbe kwa wananchi bila kutukana matusi? Kwamba hawawezi kujenga hoja za kuwashawishi watu bila matusi? Kwamba hawawezi kueleweka kwa watu wasipotukana matusi?

Ni vipi na namna gani mbowe anawalea vijana wake? Anawafundisha nini akiwa nao kwenye vikao vya ndani? Anafurahia matusi yanayotolewa na vijana wake kwenda kwa watu wengine wanaotofautiana nao mitizamo na itikadi? Amewahi kuwaonya? Je wamemshinda au anawaogopa? Shida nini kukosa huku adabu na hekima kwa vijana wa CHADEMA? Je malezi mabaya toka kwenye familia zao? Kama ni malezi mabaya kutoka kwenye familia zao, iweje wawe ni vijana wa CHADEMA pekee waliokosa adabu ,hekima ,busara na staha na kutukana matusi kama vichaa au wendawazimu?

Je, CHADEMA ni kimbilio la vijana waliozibuka akili na kuvuta mibangi bila kikomo? Je CHADEMA imejaa vijana ambao wameshindikana kutoka katika familia zao? Je CHADEMA ni mrundikano wa vijana walioathirika kisaikolojia,waliokosa malezi pamoja na kujikulia tu bila uangalizi wa aina yoyote ile? Inawezekana vipi kijana unayejitambua ,mwenye adabu ,hekima,busara,staha,aibu na hofu ya Mungu ukawa unatukana matusi na kuandika matusi makubwa kiasi kile katika mitandao ya kijamii kuwatukana watu waliokuzidi umri na ambao wanaweza kulingana na wazazi wako au kuwazidi kabisa? Kwani huwezi ukamkosoa mtu kwa staha pasipo kumporomoshea matusi ya nguoni na kumdhalilisha?

Unapata wapi ujasiri wa kumtukana mtu matusi ya nguoni utafikiri kuna kosa kubwa? Kutofautiana tu mitizamo ndio umdhalilishe mtu? Kukosolewa tu ndio iwe nongwa? Kwanini pia vijana wa CHADEMA wanaona ufahari sana na kumpongeza sana na kumuona shujaa na jasiri mtu anayetukana matusi makubwa makubwa viongozi wetu pamoja na wale wanaotofautiana mitizamo katika mambo fulani fulani? Kwamba watanzania wote tuwe na mawazo sawa na kuwaza sawa wakati wote kama mazuzu?

Mimi naona Mbowe alikuwa na nafasi kubwa sana na ya kipekee sana kuwakuza vijana wake kiuongozi wakawa na adabu,hekima,busara,staha na utulivu wajengapo hoja ama kuandika katika kurasa zao za mitandao.angewafunda na kuwakemea au kuwafundisha namna ya kujenga hoja badala ya kushambulia watu kwa matusi.sasa kinachoonyesha kwa sasa ni kama Mbowe anawaogopa vijana wake kuwaambia ukweli kwa hofu kuwa wataanza kumshambulia kwa matusi na kejeli na kumtaka ajiuzulu na kuwaachia chama chao.

Lakini pia nimefanya uchambuzi wangu binafsi na wa kina kwa kutumia akili yangu nikabaini kitu kingine kuwa kwa muda mrefu Mbowe amekuwa akiwatumia vijana hawa katika kuwashughulikia mahasimu wake na washindani wake walioonekana kukimendea na kukinyemelea kiti cha uenyekiti.ambapo amekuwa akiwatumia vijana wake kupeleka mashambulizi ya lugha za aina zote kuanzia matusi, udhalilishaji pamoja na tuhuma za kupikwa ,uzushi,uongo na kuwapaka matope wapinzani wake ndani ya chama kwa kutumia vinywa vya vijana hawa.

Hivyo kama amewatumia katika michezo haramu na mibaya ya kuumiza wapinzani wake na akafanikiwa kuendelea kusalia katika kiti hicho cha Uwenyekiti kwa miaka 20 ,maana yake ni kuwa hawezi kuwa na ujasiri wala uwezo wala nguvu wala kifua wala sauti ya aina yoyote ile kuwakemea au kuwaonya vijana hawa kuwa waache matusi. kwa sababu ni matusi hayo hayo ndiyo waliyoyatumia kumuokoa yeye kudondoshwa au kupata ushindani mkali katika kinyang'anyiro cha Uwenyekiti. ndio sababu anaamua kukaa kimya hata kama hapendi matusi hayo ya vijana wake.na kama akizungumza hawezi kuzungumza kwa ujasiri au nguvu au sauti ya mamlaka na akaeleweka na hao vijana,zaidi zaidi watamdharau tu moyoni mwao na kumpuuza. na ndio sababu ya kuendelea kwa hali hii ya matusi miongoni mwa vijana wa CHADEMA.

Hali hii ya matusi inayofanywa na vijana wa CHADEMA kwa sasa inawakwaza sana Watanzania,inawakera sana maana hakuna mtanzania anayependa kusikia habari za matusi ya nguoni.au hakuna kijana anayeweza kufurahia kuona mzazi wake au mama yake akitukanwa matusi ya nguoni na vijana wadogo mitandaoni bila sababu ya msingi.hii ndio sababu CHADEMA inakuwa inaonekana kama chama cha kihuni huni tu kilichojaa na kusheheni wahuni. Lakini ikumbukwe ya kuwa wahuni hawa na waliokosa adabu na kutukana matusi leo ndio watakaokuwa viongozi kesho ndani ya CHADEMA.hivyo chama kitaendelea kukosa mvuto na ushawishi kwa watu kwasababu kitakuwa hakina hoja ya msingi kuwashawishi watu kuwaunga mkono zaidi ya matusi tu ambayo hakuna jamii inayoweza kufurahia jambo hilo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania wote kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Lucas kakutukana nini🤔
 
Huwezi kupata uteuzi wa aina yo yote kwa sababu wameshagundua kwamba huna akili .Ulikuwa unaweka namba ya simu kwenye kila mada ili upigiwe,lakini kwa kuwa wewe ni chawa mpumbavu waliamua kukupuuza.
 
Kwa nini huwa unasikiliza na kufuatilia au kusona matusi yao?Ina maana unapenda wanavyotukana.
Acha unyumbu mjinga sana wewe, wananchi tuna haki ya kusikiliza hotuba za viongozi. Sasa kama mnakuja kutukana mseme mapema ili tusije kusikiliza hayo matusi .
 
Ninyi vijana wa CHADEMA badilikeni kitabia .acheni matusi na kudhalilisha watu.kuweni na adabu na hekima mnapojenga hoja badala ya kushambulia watu kwa matusi ya nguoni utafikiri mmeshikwa na ukichaa au uwendawazimu.
Mkuu, hebu nipe mfano wa matusi ya nguoni aliyotukanwa mtu kutoka kwa kijana wa chadema tafadhali
 
Acha unyumbu mjinga sana wewe, wananchi tuna haki ya kusikiliza hotuba za viongozi. Sasa kama mnakuja kutukana mseme mapema ili tusije kusikiliza hayo matusi .
Mkuu naomba nijifunze kutoka kwako ni aina yapi ya matusi hayo ya nguoni waliyotukana wanachama wa chadema tafadhali
 
Kamsikilize vizuri Kinana kwenye hotuba yake ya jana, ndio utajua ww kutukanwa ni lazima.
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itashinda na kupita kwa kura nyingi za kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.hii ni kutokana na ubora wa sera na ajenda zake zinazogusa maisha ya watanzania. tofauti na vyama kama CHADEMA havina uwezo hata wa kuandaa ilani yake ya uchaguzi
 
Mkuu, hebu nipe mfano wa matusi ya nguoni aliyotukanwa mtu kutoka kwa kijana wa chadema tafadhali
Siwezi kusema kuyarudia na kuyaandika matusi hayo hapa jukwaani maana nami nitakuwa nafanya ujinga ule ule wafanyao vijana wa CHADEMA wakishavuta mibangi yao.
 
Back
Top Bottom