Jamaa ameniwahi maana nilikuwa na mpango wa kuja na idea hii pia! Unajua Bariadi pako tricky sana kwa CDM maana kule kwa cheyo jamaa amewakamata wale wacheza mbina kwa njia rahisi sana! Cheo huongelea pamba tu na utani mwingi ndicho wanachotaka kusikia wanyatunzu! Vijisenti kwa upande wake anatumia rushwa tu na kawateka watu kwa kuwanunulia roli ambalo mtu ukiwa na harusi,shere au msiba wewe unaweka mafuta tu unaumia. Huduma hii imesambaa sana mpaka vijiji vya karibu na mjini!
Kimsingi Bariadi imekaa vibaya ila kama alivyosema masalapa, CDM wanahitaji kutengeneza wapiga kura wao hasa vijana ambao hupenda mabadiliko. Vijana wana nguvu sana jimbo la vijisenti, maana katika kata moja niliambiwa kwenye uchaguzi wa 2010 diwani wa udp alibebwa na vijana ambao walikuwa wameamua kumpigia kampeni kwa kutembea kijiji hadi kijiji kwa maandamano!
Kwa namna ambavyo chadema inapendwa na vijana, kama viongozi watafika bariadi na kufanya mikutano ya uamsho katika kata zote ni lazima wataacha msisimko mkubwa sana wa vijana na watu wa rika la kati.
CDM bado haijajulikana sana bariadi sijui ni kwanini!
Lakini kwa mtazamo wangu mimi kama CDM hawajachukua Bariadi basi watakuwa bado hawajakubalika kanda ya ziwa. Wanayantuzu ni wadau muhimu sana kule kanda ya ziwa!
CDM waende bariadi wakitambua kuwa kuna fedha nyingi sana za kifasidi zimewekwa kwenye miradi ya pamba. Fatilieni pia zile pesa zilizotolewa kwa wafanya biashara wa pamba mtazikuta huko pia!
Ushauri wangu kwa CDM sasa hivi ni muda wa kuwa na mikakati tofautitouti ambayo nitaonyesha tofauti ya Chadema na CCM. Mimi nadhani CDM lazima wawe na wanauchumi ambao watafanya analysis na kushauri namana ya sera za kiuchumi zinazotekelezeka amabazo CCM hawana na kuzitangaza kwa wananchi. Nadhani sasa kunahaja ya kutumia TV zaidi kuelezea sera za CDM badala ya kutegemea mikutano ya hadhara ambayo CCM wanatumia mbinu zote kuikwamisha. Nadhani watu wengi tuko tayari kuchangia airtime ya TV kwa ajiri ya kuanalyse sera za chadema kuelekea 2015 ili watu wajue tofauti ya chadema na ccm kuanzia sasa. Sera kama kupunguza bei ya vifaa vya ujenzi ina mvuto sana kwa wananchi kama analysis ikifanywa vizuri na wachumi wa chama na kuwekwa hewani kwenye TV itakuwa safi sana! Pia namna ya kuwainua wakulima kwa kuborsha kipato chao pengine kwa kutoa garantii ya bei za mazao yao!
Kwa kifupi CDM need to come up with a new strategy zaidi ya mikutano ya hadhara ambayo serikali inaipinga kwa nguvu zao zote!