Mbowe: CCM inaogopa serikali tatu

Rationalizer

Member
Jul 12, 2013
46
19
na Thomas Murugwa, Tabora

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinapinga mfumo wa serikali tatu usiingizwe katika Katiba mpya kwa vile kinajua kwamba huo ndio utakuwa mwisho wa utawala wake.
Mbowe alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Chipukizi mjini Tabora na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Alisema kuwa CCM inakwepa kuzungumzia suala la serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuhofia kwamba vyama pinzani vitatwaa ushindi katika ujaguzi mkuu ujao.

“CCM inaogopa serikali tatu kwa sababu inajua Zanzibar ni mali ya Chama cha Wananchi (CUF) na Tanganyika itakuwa ya CHADEMA; yenyewe itakuwa wapi?” alihoji.

Mbowe alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili umekuwa manufaa kwa Wazanzibar kwani Watanganyika wengi wakienda kwao hawana uhuru wa kumiliki mali tofauti na ilivyo wao wakija bara wanamiliki kila kitu sawa na Watanzania wengine.

“Tanganyika tupewe uhuru wetu kama Wazanzibari, wana bendera yao, wimbo wa taifa, rais wao na Bunge lao,” alisema.

Mbowe pia aliwatahadharisha wananchi juu ya hujuma wanazofanyiwa na serikali iliyo madarakani ikiwemo kulipia kodi ya umiliki wa laini ya simu za mikononi.

Alisema kuwa serikali ya CCM ilifuta kodi mbalimbali kwa ajili ya kumhadaa mwananchi ili aweze kuipigia kura lakini hivi sasa zimerejeshwa kwa mlango wa nyuma ikiwemo hiyo ya simu na ile inayowataka wananchi kununua visimbuzi ndipo waweze kupata mawasiliano ya runinga zao.

Mbowe ambaye yuko kwenye ziara ya kawaida kwa ajili ya kuimarisha chama, alisema kuwa kuanzia Agosti 4 chama hicho kitafanya ziara ya kutembelea mikoa yote nchini na kukutana na wananchi ili kuzungumza na kujadili nao wanataka Katiba iwe na muundo gani.
Katiika hatua nyingine wananchi wamelaani vikali kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kwamba wanaotaka serikali tatu ni wazee ambao wanagojea kifo.

Source: Tanzania Daima la tarehe 29 -07-2013.

Maoni Yangu:
Tanzania ni ya watanzania wote na kamwe haiwezi kuwa mali ya chama chochote cha siasa. Nalazimika kusema hivyo kwasababu, chama cha siasa ni tofauti na uzalendo uliopo kwa watanzania kwa nchi yao ya Tanzania.

Inasikitisha kuona kwamba propaganda zote za Chadema zinazoendeshwa kwa gia ya peoples powe, Movement for Change ( M4C) kupitia kwa viongozi wake wa kitaifa mfano Mh. Freeman Mbowe kuwataka watanzania waing'oe CCM madarakani haina maana kwamba, kuwawezesha watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii bali ni dhahiri kwamba Chadema imejikita hasa kuimiliki Tanzania hasa Tanganyika kama Mh. Mbowe alivyonukuliwa katika gazeti la Chadema la Tanzania Daima la leo tarehe 29-07-2013 huku akiongeza kuwa, Zanzibar ni mali ya chama cha wananchi CUF.

Umiliki wa mali maana yake ni kwamba, kamwe mali hiyo haiwezi kuwa ya mtu, watu, kampuni au taasisi nyingine yoyote bila ridhaa ya anayemiliki mali husika. Kwa kauli ya Mh. Mbowe, Chadema itakapoimiliki Tanganyika kupitia katiba mpya maana yake ni kwamba sanduku la kura halitakuwa na mantiki yoyote kwa Mtanzania/Mtanganyika maana kila mtu atalazimika kujiunga Chadema ili apate huduma za kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Maswali ni mengi lakini je, kwa viongozi aina ya Mh. Mbowe ambaye uwezo wake wa kufikiri umenasa katika chama cha siasa kuimiliki nchi hajui kwamba si kila mtanzani ni mwanachama wa chama cha siasa?

Je Chadema ikishaimiliki nchi watanzania watakuwa wageni wa kuomba uraia katika nchi ya Chadema au watapataje hisa ya kuimiliki nchi?

Au Mbowe anataka kuiaminisha Dunia kwamba chama cha Chadema ndio mbadala wa watanzania?

Ni kwamba Mbowe kasema kwa majigambo ili tu awape kiwewe mahasimu wake wa kisiasa hasa vyama vya CCM, UDP, TLP, CCK na kadhalika au Mwenyezi Mungu kaamua kuwaumbua kabla hawajaitumbukiza Tanzania yetu katika shimo la giza? Siamini katika kuwapa mahasimu wake kiwewe kwasababu Mh. Mbowe yuko makini kwani anazungumzia hilo ikiwa ndio njia ya kutetea uhalali wa serikali tatu katika katiba mpya ijayo hivyo nisitegemee mtu yeyote akijitetea hapa!

Chonde chonde ya mtoto wa mkulima, Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda inafaa kuwa kidhibiti mwendo cha viongozi mbumbumbu kama Mh. Mbowe wasiojua tofauti kati ya watanzania na vyama vya siasa katika uhalali wa kumiliki nchi.

Hii itamchoma Mbowe, Chadema yake na wote wanaotaka kuhalalisha chama cha siasa kuimiliki nchi na ninaamini wataifuta hii thread ila mara tu ilipobandikwa hapa jamii forums, pia mwenyezi Mungu kaiandika katika kitabu cha uzima wa milele kwaajili ya watanzania na si kwaajili ya chama cha siasa na watanzania watakumbushwa na kufunuliwa yote yaliyojifisha nyuma ya pazia kabla ya hukumu ya 2015 katika ulingo wa siasa.

Mungu uibariki Tanzania na watu wake, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Dunia iwe mahala salama pa kuishi
 
Post ingekuwa ya kizalendo sana hii kama usingekubali kuwa a political slave!!!!
 
eti zanzibar ni mali ya CUF kaanza kubagua hata nchi hatujampaa je tukimpa si atabadilisha na mji mkuu uwe arusha
 
hayo ni mambo ya kawaida kwenye siasa mbowe piga kazi ya kuwaelimisha watanzania
 
Waache waogope tuu; chadema lazima tuchukue nchi hata kwa kutumia mchupa wa tindikali.

Nani asiyejua tabia yenu ya siasa za tindikali, maandamano, vurugu za kila namna na kilio cha kuomba huruma kwa watanzania kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa ambayi ndio mnaijaza tindikali kama ulivyosema? Nani hajawah kusikia kauli ya kukata tamaa ya Dr. Slaa, eti chadema itachukua nchi hata kwa kumwaga damu? Nani asiyejua aliyetoa kauli ya nchi haitatawalika? Nani asiyejua msemaji wa kauli za watu wafe ili ukombozi upatikane? Ewe Mwenyezi Mungu, tawala ndimi za wanasiasa uchwara kama hawa maana wataipeleka Tanzania pabaya
 
Toka lini CCM wakawa na uchungu wa kuongeza gharama za uendeshaji wa nchi? Mbona walipinga vikali kuondoa POSHO za wabunge ambazo CHADEMA na vyama vya upinzani walisema na wanazidi kusema ni mzigo kwa wapiga kura. Leo hii Watanganyika kwa wepesi wa kusahau mnawasikiliza CCM eti serikali tatu zitaongeza gharama. Watu wamepiga kelele kuhusu mashangingi kuwa ni mzigo kwa mlipa kodi lakini kila kukicha yananunuliwa mapya, kila mkuu wa wilaya, mkurugenzi, mkuu wa mkoa, maafisa kibao ni mashangingi, halafu mtu unadiriki kuwaamini CCM kuwa serikali tatu ni mzigo? toka lini wakawaza hivyo? Serikali tatu sio sera ya CCM lakini sasa ni sera ya Wananchi, tulieni mnyolewe maana serikali ya Tanganyika itafyeka vyeo mnavyopeana kama zawadi kwa mashostito na wapambe.
 
Back
Top Bottom