Mbowe atolewa nje ya bunge

Mbowe atolewa nje ya bunge

SOKON 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Posts
1,134
Reaction score
331
Naibu spika J. Ndugai ametoa amri Mbowe atolewe nje baada ya Mbowe kuomba muongozo ila Job Ndugai akamuamuru akae chini na asiongee chochote ndipo Mbowe akakataa kukaa mpaka asikilizwe anachotaka kusema.

Wabunge wa upinzani wamegoma Mbowe kutolewa nje na kinachoendelea ni kupigana kati ya askari na wabunge wa CHADEMA.

Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.

****

Vurugu kubwa zimetokea Bungeni hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.

Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.

Mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.
 
Muda huu wabunge wote wa CDM na baadhi toka vyama vingne vya upinzani wameweka ngumu MBOWE asitoke. Wote wamekusanyika mbele kupinga asitoke, ni mwendo wa kushikana muda huu hii ni baada ya kura kusomwa ktk kura ya kuamua kama MUSWAADA uondolewe au majadiliano yaendelee.
 
mkuu unaweza kutuambia sababu iliyopelekea hayo?
 
Nadhani ni ishara ya wazi ya tatizo la uongozi wa Naibu Spika Huyo kwa kushindwa kusimamia na kujibu hoja chokochoko za Upinzani ambazo zipo katika mabunge yote Duniani yenye vyama vingi!

Sidhani kama Mh huyu anajua kuwa ni kipimo kibaya kinachomshusha hadhi yake?
 
Duh kumbe Vita inaanzia humu humu ndani afu mnasingizia Rwanda ona Bunge lenu Full aibu
 
Naona spika anasema jambo juu ya hali hii, ila hali bado tete wabunge wa upinzani bado wako pale mbele kumkingia kifua kiongozi wao. Ndugai ametoa amri tena kwamba askari kama askari wahakikishe KAMANDA MBOWE anatolewa
 
...kimetokea nini mkuuu wengine tuko mbali ...
 
Atalipwa posho hapo kwa kufanya kazi hiyo ya kibedui
 
Ndugai hovyo sana,kwa nini asimsikilize anataka kusema nini Mbowe?
 
Kuna sauti za wabunge wa CCM zinasikika zikisema "KAMA ASKARI WAMESHINDWA WAWAACHIE WABUNGE WENYEWE". Hali ni tete kiukweli wabunge wanasukumana na askari
 
Haya matumizi ya nguvu ya Ndugai hayajengi badala yake yanabomoa. Kwa nini asimsikilize alichotaka kuongea Mbowe? huku kulazimisha wajumbe wa katiba kutasaidia kupata katiba iliyo bora kweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom