Mbowe atoa ruhusa kwa TAKUKURU kuwachunguza Lowassa, Sumaye na Nyalandu juu ya Ufisadi

Mumesharuhusiwa sasa na komredi Mbowe anzeni sasa kuchunguza hamna cha kuchunguza nilimusikiliza kwa makini kigwangala akimtuhumu nyalandu kuwa ni fisadi lakini mwisho wa mchango wake akasema hakusaini mkataba sasa nikajiuliza mtu msomi kama kigwangala anatuletea ujinga kama huu nakutufanya sisi ni wajinga hatujui kupambanua mambo,

kingine huyu Kigwanga aliwahi kusema pr. Muhongo ni muongo hujawahi kuona alipo teuliwa na baba yao kurudi kwenye wizara ya nishati na madini akampongeza sasa tuwaeleweje.
 
Tukisema chadema ni chama cha ajabu, watu wanakuja juu.
Yaani ili takukuru ifanye kazi yake kwa wanachama wenu, mpaka mwenyekiti atoe ruksa! what a non-sense!
 
Unapo kuwa waziri lazima ufisadi utokee kwenye wizara yako na ni lazima wakiamua kuufuatilia wakukute na kosa, haiwezeka kwenye wizara watu wote wawe waminifu
 
Hivi Mbowe ndiye anayeruhusu wanachama wa CHADEMA kuhojiwa na TAKUKURU au Polisi? Kwa hiyo bila ruhusa yake hawawezi kuhojiwa? Au ni kwa mamlaka hayo aliyojipa ndio maana hajamruhusu yule dereva kuhojiwa?
 
Kigwangallah anasiasa za maji taka.. Hiyo wizara kuna waliotoka huko wakiwa na kashfa nzito ikiwemo ya Twiga aliyepandishwa ndege bado hawaguswi mpaka leo hii

Toka Nyalandu atoke ccm Kigwangallah amekuwa msemaji Juu yake, hiyo wizara haikuwa na mawaziri wengine mpaka unahangaika na mmoja tu aliyeondoka?

Anasema kuna docs zinahitaji tu kusainiwa alizikuta kwenye meza ya Nyalandu, je baada ya Nyalandu wizara haikuwa na wa waziri kushughulika na issue hiyo?

Je, Maghembe ameondolewa kwa sababu gani? we mwenyewe unasema kuna mtu anataka kukuhonga je kwanini hukuweka mtego ili TAKUKURU wafanye kazi yao? Naongea na Kigwangallah
 
Hivi Mbowe ndiye anayeruhusu wanachama wa CHADEMA kuhojiwa na TAKUKURU au Polisi? Kwa hiyo bila ruhusa yake hawawezi kuhojiwa? Au ni kwa mamlaka hayo aliyojipa ndio maana hajamruhusu yule dereva kuhojiwa?
Kama wanaosimamia hivyo vyombo hawaelewi we unafikiri Mbowe angefanyaje?
 
Mimi si mfuasi wa chama chochote, ila kwa speech ya KUB Mbowe Jana, ilikuwa nzuri , si ya kubeza kisa kasema mpinzani..hata ivyo jamaa yuko smart ktk kudadavua issues... Kuna watu huwa wanambeza sana, sioni ubutu wake kimaarifa.

haaa hiii ndo unavo jidanganya kua huna chama kua na chama kaka c lazma uwe na card ya wana chamaa wala ushabikie kua na chama ni kuunga mkono mapambano kwa unavo aminia kua ni ya haki na yakweli ,kila chama kina sera yake na hakuna chama kilicho na sera mbaya ila utekelezaji tuu,uchama una ingia hapa,kuona jitihada za ukombozi kwa kile unacho kiamini na kuamini zina faa
 
Maneno ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mbeya kuendelea na ziara ya kuwanadi Wagombea wa Udiwani katika uchaguzi mdogo.

Mbowe akiwa jukwaani amesema “Nimemsikia Waziri mmoja, Waziri Kigwangalla……. anatoa maelekezo kwa TAKUKURU wamshughulikie Lazaro Nyalandu aliekua Waziri wao ambae sasa hivi fresh ndani ya CHADEMA“

“Wakasema CHADEMA mlisema Lowassa alikua fisadi tukawaambia sawa tulisema kwa wakati wake, kwenye siasa hauna Rafiki wa kudumu wala Adui wa kudumu lakini tumeshtuka kwamba huo ufisadi wake hamjaweza kuudhihirisha, mpelekeni Mahakamani…….. hawana cha kupeleka Mahakamani”

“TAKUKURU wanasema wameshapewa malalamiko kwahiyo wanayafanyia kazi tunawaambia CHADEMA hatuogopi Mahakama na kiongozi yeyote ndani ya CHADEMA mnaetaka kumchunguza akiwemo Mbowe anzeni leo hatuogopi”

“Awe ni Lowassa mchunguzeni, awe ni Sumaye mchunguzeni… awe ni Nyalandu mchunguzeni, awe ni Sugu mchunguzeni”

My take
:
Haya sasa sijui watakuja na kisingizio gani wakati wao ndio wenye dola.
Masamaki aachiwa huru na mahakama baada ya DPP kutokuwa na nia ya kumshitaki .
 
Kwenye siasa hauna Rafiki wa kudumu wala Adui wa kudumu.....
Kama ndo hivyo Mbowe analalamika nini?
Halafu hili swala sio la urafiki ama uadui, ni swala la kuwa kigeugeu na kuuhadaa umma kwa makusudi ili upate mtaji wa kisiasa.
Ni mojawapo ya aina mbaya sana ya utapeli.
 
Back
Top Bottom