Mbowe atembelea Gereza la Uyui

Mbowe atembelea Gereza la Uyui

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Ziara ya Mbowe Gereza Kuu Uyuwi, waibua gumzo kubwa, wafungwa na askari, wasimulia.

Kumekuwa na gumzo kubwa miongoni mwa wafungwa na askari katika Gereza Kuu la Uyuwi, kutokana na kupata ugeni mzito wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na KUB, Freeman Mbowe alipofika gerezani hapo kwa kushtukiza, akiwa na viongozi na makamanda kibao wa chama hicho Kanda ya Magharibi, mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma.

Makamanda hao walifika kuwaona makamanda wenzao walioko mahabusu gerezani hapo! Itakumbukwa kuwa makamanda watano wa CHADEMA, Henry Kilewo na wengine wamebambikiwa kesi ya ugaidi huko Tabora! Wafungwa na askari walionekana kuonesha nyuso za matumaini na tabasam bashasha kila walipopishana na kusalimiana na makamanda wa M4C! Wafungwa wengine kwa furaha, hawakusita kunyoosha alama ya 'V' hewani kuonesha kuwa wanatambua na kukubali M4C, huku askari kwa kubanwa na sheria, wakinong'ona maneno ya matumaini!
 
Thanks MM kwa taarifa hizi maana Mbowe angalisema basi wangaliweza wazuia kuwaona wenzao .Good trick naona intelijensia haikunasa hili .
 
wao wana pesa sisi tuna MUNGU tulianza na MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU
 
safi sana kamanda Mbowe.. Fanyeni kazi m4c iwafikie mpaka sisimizi...!
 
"Makamanda hao walofika kuwaona makamanda wenzao walioko mahabusu"....mnapokuwa mnareport muwe mnaangalia lugha zenu unapokuwa kiongozi katika ngazi ya taifa dosari kama hizi hazitakiwi kuwepo

"kiongozi huyo alifika kuwajulia hali mahabusu katika gereza hilo"ingetosha sana

Au na kura ya urais ataomba kwa makamanda tu???
 
Nimeamini kwa kweli ccm sasa wamebakiwa na dola tu,ila wananchi ,wanyonge wanai support cdm

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Na tena ukichagiza na ujinga wa mwezi wa saba bila ya shaka walikuwa wanatabasamu kuomba siku ziende haraka watoe hukumu 2015.
 
si mbali, naliona tumaini hai la ukombozi, OOH Asante Mungu.
 
Ziara ya Mbowe Gereza Kuu Uyuwi, waibua gumzo kubwa, wafungwa na askari, wasimulia.

Kumekuwa na gumzo kubwa miongoni mwa wafungwa na askari katika Gereza Kuu la Uyuwi, kutokana na kupata ugeni mzito wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na KUB, Freeman Mbowe alipofika gerezani hapo kwa kushtukiza, akiwa na viongozi na makamanda kibao wa chama hicho Kanda ya Magharibi, mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma.

Makamanda hao walifika kuwaona makamanda wenzao walioko mahabusu gerezani hapo! Itakumbukwa kuwa makamanda watano wa CHADEMA, Henry Kilewo na wengine wamebambikiwa kesi ya ugaidi huko Tabora! Wafungwa na askari walionekana kuonesha nyuso za matumaini na tabasam bashasha kila walipopishana na kusalimiana na makamanda wa M4C! Wafungwa wengine kwa furaha, hawakusita kunyoosha alama ya 'V' hewani kuonesha kuwa wanatambua na kukubali M4C, huku askari kwa kubanwa na sheria, wakinong'ona maneno ya matumaini!
Ha ha haa yaani we jamaa ni mbeeya hao askari wakinong'ona maneno ya matumaini uliwasikia

haya bwana kawekewe kabaaaang yako paleeeeeeeee makao makuu Kinondoni au uko Tabora
 
Hii ni taarifa nzuri sana na inaleta faraja kwa wapenda mabadiliko ambao wengine hufungwa kwa hila za watawala!
 
"Makamanda hao walofika kuwaona makamanda wenzao walioko mahabusu"....mnapokuwa mnareport muwe mnaangalia lugha zenu unapokuwa kiongozi katika ngazi ya taifa dosari kama hizi hazitakiwi kuwepo

"kiongozi huyo alifika kuwajulia hali mahabusu katika gereza hilo"ingetosha sana

Au na kura ya urais ataomba kwa makamanda tu???

Kama vipi na wewe jiunge na Chadema ili uitwe kamanda! Vinginevyo piga kimyaaaaaaaaa!
 
Back
Top Bottom