Helena Ongara sio wa wa Tawi la DMV.Helena ni wa columbas ,ohio.Mimi ni Ludigo Mhagama. ninawatoa hofu makamanda,tutaandika baadae ripoti nzuri kabisa.Mimi ni ndio katibu kwa DMV kwa muda kutokana na katibu wetu kwenda kugombea ubunge.Ninakupeni uhakika huo.Sisi chadema hatufichi kitu kama mnavyosikia mwenyekiti wetu Mbowe anavyoongea kila mara.umeandika uongo ,afadhali ungeandika propaganda.Kwanza nakuuliza hiyo hoteli ya ohio ipo mtaa upii???????.sijasikia kwa muda wangu au kuona hoteli inaitwa ohio.Labda.Najua hawa watu waliosomea propanda ulaya mashariki wanapata shinda sana siku hizi.Nafikiri mnawajua ni akina nani hao.Nakushauri rudi katengeneze tena hii propaganda ili hata ulete challange kidogo ndugu yangu.sasa hapo umepoteza muda na air time yako kwa kuandika kitu chepesi mno.alafu ccm wamekupa pesa bure,nawaomba ccm wawalete watu hapa watu makini.Inasikitisha ccm wanapoteza pesa kuwapa watu wakae kwenye computer ,na ni watu sio makini,kwanini hizo pesa msipeleke kwa kwenye nyumba za watoto yatima?
Baada ya mwenendo wa Kampeni kuonekana kuwa mgumu huku kila alichoahidi Lowassa kutotimia mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe aamua kukutana na aliyekuwa katibu wake Dkt. Wilbroad Slaa nchini Marekani.
Taarifa za uhakika ni kuwa Mbowe aliondoka nchini toka juzi na kupokelewa na wanachama wa Chadema tawi la DMV aliposhuka Uwanja wa Kimataifa wa Dulles huko Marekani ambapo Dkt. Slaa alimtangulia muda kidogo.
Taarifa zilizopatikana toka kwa moja ya viongozi wa tawi hilo aliyejulikana kama Kalley Pandukizi amesema ni kweli Mbowe na Slaa tumewapokea na wapo hoteli moja hapa Ohio kwa ajili ya mazungumzo binafsi. Amekiri baada ya kumpokea Mwenyekiti wao Mh. Mbowe walimpeleka moja kwa moja hotelini ambapo ndipo walipomkuta Dkt. Slaa.
Tetesi zaidi zinasema Mbowe amemuomba msamaha sana Dkt. Slaa na kumueleza walipotoka kwani mgombea waliomchukua anadhoofika kiafya kila kukicha kiasi kwamba mikutano mingine wananchi hawamsikii anapohutubia vile vile hakuna hata moja alilotimiza katika makubaliano kabla hatujampokea zikiwemo fedha za kampeni hivyo chama kinapata wakati mgumu wa kufanya kampeni kikamilifu.
Inasemekana Mbowe amemueleza Slaa kuwa ujio wa Lowassa umeigharimu Chadema kwani mpaka sasa John Mnyika hajakubali kupanda majukwaani kumnadi Lowassa kitu ambacho ni tabu zaidi kwao. Pamoja na vijana wa Lowassa kuuteka mchakato mzima wa kampeni hali inayokiuka makubaliano tuliyompa.
Kikubwa ni kuwa taarifa za ujumbe mfupi toka kwa Bi. Helen Ongara ambaye ni katibu wa BAWACHA tawi hilo la DMV ni kuwa Mwenyekiti huyo amepoteza tumaini hasa alipowapa video ya Mgombea akiomba kura kwa kigezo cha ulutheri kimewagharimu zaidi hivyo amedai watapigana ili wapate viti vya ubunge ila urais watapoteza.
Hata hivyo aliwadokeza kuwa kampeni zinaratibiwa na Lissu lakini wanafikiria kuchukua maamuzi magumu ya kuwatosa UKAWA ili wabaki wao kama wao kuliko sasa ambapo wanavibeba vyama vya NCCR MAGEUZI, NLD na CUF. Ambapo hata hivyo hali ya mpasuko imeanza kuonekana kupitia vyama vya CUF na NCCR MAGEUZI.
Walisahau Majuto ni mjukuu huja baadae!!
Mbowe yupo Marekani?
Lowasa-Tumaini letu
Helena Ongara sio wa wa Tawi la DMV.Helena ni wa columbas ,ohio.Mimi ni Ludigo Mhagama. ninawatoa hofu makamanda,tutaandika baadae ripoti nzuri kabisa.Mimi ni ndio katibu kwa DMV kwa muda kutokana na katibu wetu kwenda kugombea ubunge.Ninakupeni uhakika huo.Sisi chadema hatufichi kitu kama mnavyosikia mwenyekiti wetu Mbowe anavyoongea kila mara.umeandika uongo ,afadhali ungeandika propaganda.Kwanza nakuuliza hiyo hoteli ya ohio ipo mtaa upii???????.sijasikia kwa muda wangu au kuona hoteli inaitwa ohio.Labda.Najua hawa watu waliosomea propanda ulaya mashariki wanapata shinda sana siku hizi.Nafikiri mnawajua ni akina nani hao.Nakushauri rudi katengeneze tena hii propaganda ili hata ulete challange kidogo ndugu yangu.sasa hapo umepoteza muda na air time yako kwa kuandika kitu chepesi mno.alafu ccm wamekupa pesa bure,nawaomba ccm wawalete watu hapa watu makini.Inasikitisha ccm wanapoteza pesa kuwapa watu wakae kwenye computer ,na ni watu sio makini,kwanini hizo pesa msipeleke kwa kwenye nyumba za watoto yatima?
Wakuombwa msamaha awe Dr.Slaa kweli!?, na mwombaji wa msamaha awe mbowe!!!!?.Hii itakuwa moja ya maajabu ya DUNIA.