Nyie wakazi wa mtaa wa pili mlishaambiwa hata aondoke nani ukawa itabaki kwani ni ya wananchi. Mara Mbowe , Mnyika au nani haitawasaidia mwaka huu, mmeshakwama tutakuja kuwakwamua tarehe 28 Octoba.
Tunaitaka Tanzania isiyo na CCM wanyang'anyi, mmeifilisi mifuko ya hifadhi ya jamii, NHIF na hata Road fund na hata mumewaelekeza hata waajiri wachangie kampeni ya Chama chenu kwa kuwadhulumu haki za waajiriwa wao. Mwaka huu Mungu wetu aliyejuu amewakumbuka waja wake, mtaondoka tu. Dhuluma itakuwa basi, ufisadi basi, na jela zinawasubiri wote mliotuibia wananchi, na hukumu ya kumuua mwandishi kule Nyororo ni lazima. Kila nikiziona zile nyama za Mwangosi zimezagaa kwenye majani napata uchungu uliochanganyika na hasira. Hakika haitapita bila mtu kuwajibika vikali kwa mauaji yale yaliyodhaminiwa na serikali. Nasema kuwa yalidhaminiwa na serikali kwani hata aliyeamuru yale mauaji alipandishwa cheo na Mkuu wa Serikali. Kwa hili ni lazima mtu aje awajibike.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.