Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Yuko huyu FaizaFoxy, tarehe 7/6/2011 ametuma posts 75 kuanzia saa sita usiku Jumanne hadi saa sita usiku Jumatano. Huu ni wastani wa post zaidi ya tatu kwa saa, assuming halali kabisa na hana muda wa kusoma posti za wengine, je hii yawezekana ? Kwa mtindo huo atakuwa amefikisha posti 75 x 365 = 27,375 na kumpita Mwanakijiji aliyejiunga na JF mwaka 2006 ! Mfano kidogo ni posti zake hizi;
  1. 6.16 pm
  2. 6.19 pm
  3. 6.21 pm
  4. 6.24 pm
  5. 6.25 pm
  6. 6.26 pm
  7. 6.29 pm
  8. 6.29 pm
  9. 6.31 pm
  10. 6.32 pm
Hizi ni posti kumi kwa robo saa ! Kwa ufupi ni kuwa katika masaa 24 aliweza tu kupumzika kwa masaa chini ya manne (kati ya saa kumi usiku na saa mbili asubuhi), je ni binadamu au mashine ! Hapumziki, halali, hali, haogi, haendi chooni - anayo kazi moja tu kuitetea serikali ya KiweteKikwete. Je hii ni ajira au utumwa ? Duh, yaani Chadema inawakosesha watu usingizi namna hii !
ukweli pamoja na mapungufu yake lakini huyu dada/kaka ni kichwa akiamua kujibu kwa point anakuwa vizuri. Ila wakati mwingine unashindwa kuelewa though response yake hufanana na wahusika.
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.

Waambie ccm nao waende NSSF kukopa - ruksa. Huyo unayemuita brazamen naona kawakamata nyonga. Your people have ruined this country FaizaFoxy and now we are fighting back. Hizo ngenjera zako hapo juu hazitakusaidia chochote, na kama mngekuwa na akili mmesoma kwa umakini wa hali ya juu hi press release ya leo ili mjue ni machine ya gani mtapulimia - kila kitu kina mwisho. Semina za ukimwi ndio hivyo zinakufa.
 
Chadema ina viongozi makini sana,wanatetea maslahi ya taifa,matumizi yasiyo ya lazima ni muhimu tuyaepuke!! futa posho,nauli,zipelekwe kwenye sector ya afya(zahanati zijengwe,waboreshe makazi ya wamama wajawazito muhi2),wapeleke sector ya elimu(watoto wa masikini wapate mikopo full).SAFI sana Mbowe,Safi CHADEMA VIVA 4EVER.
 
Hongera Mbowe!! Hukulalamika, umesema ukweli. Ukatenda kama kielelezo kwa kulirudisha "shangingi" walilokupa ulitumie KUB. Ni aibu kwa viongozi wa juu wa Taifa wanaolalamika lakini bila matendo ya mfano wakati wanamamlaka ya kufanya lolote lililondani ya sheria.
 
Tungekuwa na viongozi kama wa CDM tangu enzi zile za Nyerere,nafikiri Tanzania ingekuwa kama Marekani.Mungu ametuletea viongozi wenye kutetea haki za wananchi kama SOKOINE.Lakini enzi zile ukitete haki za wananchi! Eee unaiga dunia.Wako wapi? Akina Sokoine,akina Kolimba.
 
Hoja ya msingi Ndugu Mbowe, nasi tutambue mustakabali wa taifa letu umewekwa mikononi mwa wanasiasa kwa muda mrefu na hawahawa wanasiasa ndio wenye ridhaa yakufanya uamuzi ulio sahihi wakubadili mfumo wa uendeshaji wa serikali na nchi.
Hivyo basi wanapaswa kutazama umma wawa tanzania unahitaji nini kwani hakuna maana baba mwenye nyumba kuja na roast kuku kutoka mjini akala peke yake akiwaacha wanae kula ugali kwa mchicha kisa yeye ndio mtafutaji mkuu katika familia.
WAR FRONT CHADEMA LETS GO!
 
Du...!Bravo!
Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!
Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!
****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!

Siasa safi ni ule ubunifu bora wenye kuwahakikishia wapiga kura maisha na ndoto walizo nazo. Pamoja na Chadema kuteka kundi la kizazi kipya kwa kasi ya ajabu, sasa hivi itikadi mpya ya security life for senior citizen (mafao ya uzeeni ya Sh. 20,000) ni kichocheo tosha cha kuteka kundi la wazee ambalo wengi wao walikuwa bado njia panda.

Nadiriki kusema Chadema kuna vichwa vya uhakika, na ubunifu uliotukuka, hapa tutegemee nini kwa nchi maskini kama ideology hii ya Chadema kuwakumbuka wazee?
 
- Well, my Respect kwa Mheshimiwa sana Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, huu wako ni mfano wa kuigwa sana na wengine wote sio tu walioko bungeni, bali hata sekta zingine za taifa! I mean huu ndio hasa uongozi wa kimapinduzi ninaouongelea kila siku, kama una magari mengi tu kwa nini kubeba magari mengine kwa jasho la wananchi wasio hata na baisikeli!

- SALUTE! na ni matumaini yangu sana kwamba Viongozi wengine nao watafuata mfano wako!

Willie @ NYC, USA.
 
Wewe Mwenye lolote,umefanya nini la maana? vua gamba!!! Alichokifanya mbowe ni cha kishujaa na ni mfano wa kuigwa na wanamagamba kama nyinyi

Mtu atoe hoja bila kuwa mfano maneno mengi mbona hajafanya, sasa kafanya kuonyesha mfano hao wanageuza habara anatafuta polarity, huu ni utumwa wa kiitikadi bila ridhaa.
 
- Well, my Respect kwa Mheshimiwa sana Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, huu wako ni mfano wa kuigwa sana na wengine wote sio tu walioko bungeni, bali hata sekta zingine za taifa! I mean huu ndio hasa uongozi wa kimapinduzi ninaouongelea kila siku, kama una magari mengi tu kwa nini kubeba magari mengine kwa jasho la wananchi wasio hata na baisikeli!

- SALUTE! na ni matumaini yangu sana kwamba Viongozi wengine nao watafuata mfano wako!

Willie @ NYC, USA.

Inapendeza kuona kwamba unaweza kuwafagilia Viongozi wa CHADEMA pale wanapofanya maamuzi mema kwa ajili ya nchi yetu. Hongera zako na wala usiogope Mkuu hutageuka jiwe :)
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.
Mbowe ni kiongozi wa Chadema ambayo ni mwiba kwa CCM na jeshi la polisi.Kama hiyo Vogue ingekuwa ni ya wizi ni kitu gani kinawashinda CCM na Said Mwema( alikuwa Interpol) kunyanyua simu na kumaliza Mbowe kisiasa?
 
An intelligent and conscientious opposition is a part of loyalty to our poor exploited by fisadis country.
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.

Ukistaajabu ya Malaria Sugu.....
 
Big up, Freeman!
Lakini next time muyakatae hayo magari kabla hamjapewa ama kupewa hiyo mikopo yake.
 
Back
Top Bottom