Mbowe anavyoshughulikia Wapinzani Wake Ndani ya Chama

Mbowe anavyoshughulikia Wapinzani Wake Ndani ya Chama

Mkuu Benson Mramba, maandiko yako ya kila siku yenye ladha ile ile kumhusu Mbowe yanalenga nini hasa?

Hata kama una hoja, tunakupuuza kwakuwa unaandika kama mwenye chuki Zaidi ya mwenye hoja. Jirekebishe Mkuu. Halafu, tunaaminishwa kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa kaskazini, iweje wewe 'wa kaskazini' uwe na bifu hivyo?

Kiukweli, sasa unaboa Mkuu. Kila siku Mbowe tu, WHY HIM ONLY?
Uteuzi tu hakuna jingine.
 
Akishughulikiwa pia utasema anaonewa. Jinai haifi.

Kw hiyo hatu hazichukuliw kwa kuwa jinai haifi? Inasubiriwa kama ile ya kumkamata Lowasa? Haya tusubiri. Ingekuwa vizuri na zile za mikutano ya siasa pia tungesubiri ila hatusubiri kwa kuwa ndio makosa makubwa zaidi kuliko kuua.
 
Aibu yako, hatakama watanzania ni wazito kuelewa. KAMA UNASEMA UKWELI, KWANINI UNAUSEMA BAADA YA KUONDOKA CHADEMA. Waambie waliokutuma, ni rahisi kuua kabisa vyama vya upinzani lakini hawawezi kuondoa mawazo mbadala (hoja kinzani) ndani ya mioyo ya watu.
 
Katika maisha yangu ndani ya CHADEMA nimewahi kusikia hili neno la NITAKUSHUGHULIKIA toka kwa Mbowe Mara kadhaa na kwa watu kadhaa na kwa kweli wote walioambiwa neno hili hawakuwa na mwisho mzuri ndani ya Chama. Nitataja wachache:-

1. Kafulila
Huyu baada ya kuambiwa neno hili alipata tabu sana. Alishawahi mpaka kuanguka ghorofani kwa hila hizi hizi. Mwishowe alifukuzwa kazi na hata wakati wa ubunge wake kwa tiketi ya NCCR bado CHADEMA iliendelea kupambana nae ili asistawi kisiasa

2. Zitto
Huyu sina haja ya kueleza sana. Kila mtu anajua alivyopachikwa sifa ya USALITI ambayo ilikuwa na lengo la kummaliza kisiasa kabisa. Alitaka kuwekewa sumu, alishakatiwa break za gari mara kadhaa, alishawekewe vijana wamdhuru, na mwishowe alifukuzwa uanachama. Kwa sababu wanajua walimzushia leo wameshirikiana nae kule Buyungu.

3. Ben Saanane

Huyu tuliondolewa nae pale makao makuu kwa hoja kuwa hatuaminiki na sisi ni watu wa Zitto pia ni wajeuri tunaringia usomi wetu. Kubaki kwetu makao makuu ingekuwa ni sawa kutengeneza akina Zitto wengine kwa miaka ya mbeleni.
Mimi nilikubali matokeo. Mwenzangu akamfuata Mbowe na kwenda kumtisha kuwa akiondolewa atatoa siri zote za mambo ambayo ameyafanya na Mbowe hususan katika kumshughulikia Zitto. (Saanane alishatuhumiwa kutaka kumuwekea sumu Zitto)

Mbowe akamuuliza unanitisha? Akamwambia usinitishe wewe jenga hoja tu. Mbowe akampa nafasi ya msaidizi binafsi (Personal assistant na mshahara mkubwa) Nafasi hii haipo kwenye structure ya Chama na tayari Mbowe alikuwa na wasaidizi wengine wanne na personal assistant wake alikuwa Mndeme ambaye alikuwa akilipwa na Bunge sio Chama. Baada ya kuona mwenzangu karudishwa kazini nikauliza kwa watu wa karibu na Mwenyekiti nikaambiwa aa huyo tutamshughulikia tu. Miezi miwili baadae nikasikia Saanane kapotea tena akitokea South Africa kumwakilisha Mwenyekiti nikajua habari imeishia hapo. MTU ulikuwa hupendwi hata kidogo leo unatumwa South Africa lazima kuna hila. Ukweli ni kuwa katika watu waliokuwa hawapendwi pale Makao Makuu na Wakurugenzi wote ni Ben Saanane Mimi nilikuwa na afadhali mara 100.

Mbowe hapendi kuzungumzia swala la Saanane na wachache niliowasikia wakilizungumzia bungeni ndio walikuwa maadui zake wakubwa Lema na Selasini na wote hawa ni watoto wa Mbowe.

4. Msafiri Mtemelwa

Huyu alikuwa ndio Mwl wa Zitto Kabwe. Huyu aliambiwa wazi wazi kabisa na Mbowe kuwa ukiendelea nitakushughulikia nje ya siasa na nje ya Chama. Uhasama ulivyozidi aliamua kuacha kazi mwenyewe na kuondoka baadae akajiunga ACT. Mtemelwa alikuwa mwenyekiti wa vijana wa NCCR mageuzi iliyokuwa na nguvu wakati huo hivyo anajua matokeo ya uhasama.

5. Mtela Mwampamba, Adam Chagulani, Juliana Shonza, Habibu Mchange, Daniel Yona n.k

Hawa wote walipata msukosuko mkali ndani ya Chama. Wengine kama Yona walitekwa na kupigwa vibaya na hatimae kutupwa ununio kule. Wengine walifukuzwa, wengine walikimbia wenyewe .

6. Mimi Mwenyewe

Baada ya kuanza kuandika mambo ya Mbowe kwenye group la viongozi wakuu iliazimiwa Tume inishughulikie maana naongea sana. Majadiliano ninayo. Mwenyekiti Mbowe aliingilia kati na kusema mambo ya usalama yasijadiliwe pale ila wataona namna bora ya kudeal na Mimi. Baadae John Mrema aliwahi kunipigia simu na kunionya kuwa wameshanivumilia sana. Haikuishia hapo akamtuma mkewe kwa mama yangu anionye kuwa anaweza kunipoteza ila sijakoma. Nawasubiria.

Aidhaa wabunge kadhaa marafiki zangu wameshanionya sana maana wanamjua Mbowe na mambo yake. Ila nimekuwa nawajibu Demokrasia maana yake ndio hiyo sio tunamlalamikia Magufuli kumbe sisi wenyewe ndio waminyaji wakubwa wa demokrasia.

7. Lissu

Mimi nimekuwa katika vuguvugu la kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya Chama tangu 2009 ambapo nilikuwa namuunga mkono kafulila kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama dhidi ya John Heche aliyekuwa anaungwa mkono na Mbowe.

Katika Uchaguzi wa mwaka huu nilikuwa na niko timu yoyote inayompinga Mbowe. Kabla Lissu hajashambuliwa niliongea na kiongozi mmoja ya Kanda kumshawishi kuwa tumuunge mkono Lissu maana ndio anaweza kupambana na Magufuli. Yule Bwana ni Timu Mbowe akaniambia huyo Lissu tutamshughulikia hataamini. Heee haikuisha wiki au wiki mbili risasi.

Mimi nikajiuliza kwanini ashambuliwa wakati wa ripoti ya makinikia? Magufuli angetaka ripoti ndio iwe habari lakini ishu ya Lissu ikaja kama destructor nikaona oooo yale yaleeee!

8. Waitara

Nae juzi kwenye kipindi cha 360 cha Clouds FM kasema alionywa atashughulikiwa kwa sababu alikuwa anamuunga mkono Lissu. Waitara kama Mbunge ameamua kukimbia mapema maana anamjua Mbowe vizuri. Alinusurika kwenye ule waraka wa mkakati wa mabadiliko maana yeye na Mimi ndio tuliotuhumiwa kuwa ni M2 ila ushahidi ulikosekana. (Mpaka kesho naunga mkono waraka ule. Bado unaishi)

Hitimisho

Mbowe anaposema NITAKUSHUGHULIKIA basi jua ni kisiasa na Kimafia. Mbowe ameshatesa, amewatweza, kuwadhalilisha wengi. Haheshimu katiba ya nchi hata kidogo. Sasa ni zamu ya Kubenea, Komu, Lissu, Lwakatare na wabunge kadhaa wa majimbo kushughulikiwa. Ni ama waache siasa au watahama na wenyewe.

Wakati Fulani nilisema bila Magufuli kumdhibiti Mbowe Wanachadema hawatamuweza na wameshamshindwa. Serikali inapaswa kuingilia kati kama ilivyofanya TFF, Simba, Yanga na kwenye Vyama vya Ushirika. Vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria ni Mali ya Umma.

Haya ni ya kweli niko tayari kuyasema hata chini ya kiapo.
Nilitaka kukuamini kidogo ila Kwa namna ulivyozungumzia namba 7, nimeamini yote uliyoandika itakuwa uongo.
 
Mkuu Benson Mramba, maandiko yako ya kila siku yenye ladha ile ile kumhusu Mbowe yanalenga nini hasa?

Hata kama una hoja, tunakupuuza kwakuwa unaandika kama mwenye chuki Zaidi ya mwenye hoja. Jirekebishe Mkuu. Halafu, tunaaminishwa kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa kaskazini, iweje wewe 'wa kaskazini' uwe na bifu hivyo?

Kiukweli, sasa unaboa Mkuu. Kila siku Mbowe tu, WHY HIM ONLY?
Ukiona hvyo kuna kitu, why akisemwa mbowe mnaruka sana? Mnaficha nn?
 
bismillahi, na yaanze ya kweli na ysio kweli.

sisi watazamaji wa haya yanayoendelea tushajinunulia popcorn na kuwahi seat za mbele. hapa nnaangalia kushoto na kulia nione sehemu ya kununua cola nijikite kuangalia nn kitafuata?
'Kwa kweli.
 
Huyo mshughulikiaji watu aliyeongelewa na mkuu Benson ameshadhibitiwa vya kutosha mpaka tarehe ya leo hii. Ngosha ni mtu anayeuweza sana ugomvi ingawa hupenda kuwaomba watu wamuombee.

Huyo mshughulikiaji watu enzi zile za JK alipenda sana kuandika makala za kutisha watu kwamba nchi hii kuna siku itawaka moto kwa sababu ya mfumo wenye uonevu.

Akawa ndio kiongozi wa mawazo ya kuwajaza watu moyo wa uasi. Elimu yake sio kubwa, ndio maana anashindwa kuisoma jamii ya sasa inahitaji nini. Anashindwa kuwa mpya ingawa uongozi wa kisiasa siku zote unahitaji upya wa kimawazo na kimkakati.

Atawatisha hao hao ambao anao uwezo wa kuwadhibiti. Na wa sasa sio JK aliyekuwa rafiki wa kila mtu mwenye uwezo wa kuvimilia ujinga ili mradi tu mambo yake yaende kadri ya alivyotaka yawe.
 
Chadema sasa iko imara kuliko wakati wowote ule.Mtoto akiwa tumboni mwa mama yake alitukosea miezi minane huanza kutengenezwa upya akiandaliwa kuzaliwa.
 
Nitashangaa sana kama huyopewa nafasi yeyote kwa kijipendekeza/kufanya kazi hii,am ashamed that we share the same region,


Shame on you and your stomach
 
Mzee wa mipasho kma shangingi wa manzese kwa mfuga mbwa,mbowe sio size yko humuwezi kwa vyote kuanzia akili,uwezo etc,mwenyekiti wko pamoja n phd feki yke kamshindwa mbowe sembuse wewe mrombo njaa kali.
Siasa huwezi pambana kma warombo wenzako ufungue genge la vyakula
Duh! hiyo ni trailer, movie bado
 
We Benson Mramba , unatafuta uteuzi kisenge mno! Ili uonekane ulikuwa kwenye uongozi!Who the **** are you? Nobody knows your stupid ass! You've fucking lost your mind!Very very stupid.

Katafute kazi nyingine ya kufanya kilaza mkubwa wewe! Tatizo ni liserikali la ccm, ajira ya uhakika ni kwenye siasa, na qualifications ni ujinga na low IQ kama inavyoonyesha kwako mleta mada na wengi tu humu.
Haya ndo tunayojiuliza huyo mbowe kawapa nini wafuasi wake kias ukihoji tu ni matusi?
 
Back
Top Bottom