Mbowe anavyoshughulikia Wapinzani Wake Ndani ya Chama

Mbowe anavyoshughulikia Wapinzani Wake Ndani ya Chama

Km ni uongo mbowe ampleke mahakamu huyu kijana

Huyo na hao wanaomtumia tumesha wadharau, vinginevyo tuamini kuwa serikali na vyombo vyake vyote inamuogopa Mbowe. Ni taahira tu anaweza kuamini huu ujinga anaoandika huyu majununi. Na asichojua ni kuwa hao wanaomtumia wanaweza kumuua ili ionekane kuwa Mbowe ndiye kamuua. Kama kuna ndugu au jamaa yake amuonye aache huu ujinga hao jamaa siyo wa mchezo watamtoa roho ili wafikie malengo hao.
 
Huna hoja zakuwaeleza wanaume wenye akili timamu. Umeongea upupu uliojaa rangi ya kijani.
 
Wewe hujitambuwi kabisa,kama Mbowe anahusika na kilichompata Saanane kwanini hujaenda kuripoti polisi?Uongo huo kawaeleze mataahira,maana umeonyesha ni namna gani ulivyo na upeo mdogo.
Kwanni mbowe hakanushi
Hivi sasa magonjwa ni mengi kutokana na ugumu wa maisha,hivyo basi anayepaswa kujibiwa ni yule ambaye hana ugonjwa huo.Kinyume cha hapo wote mtaonekana ni wagonjwa.
 
Sasa kama una ushahidi dhidi ya hizi tuhuma dhidi ya Mbowe kwanini usimpeleke mahakamani kulikoni kuyaanika hapa,una lako jambo si bure. Mbowe ana matatizo yake lakini haya mengi yanaonekana unamchafua.
 
Write your reply...Kama anao ushahidi kwanini asiupeleke polisi sheria ichukue mkondo wake?Maana umesema hata chini ya kiapo utatoa ushahidi.Polisi walishasema wanafanyia kazi taarifa zozote bila kujali ,mbona hizi wako kimya?
 
Kwa andiko hili ni wazi kuwa TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA, hawa wazandiki wanatambua wazi kuwa bila kumchafua na kumtoa mbowe CHADEMA na upinzani kwa jumla hautakufa. Mbowe ni mti wenye matunda lazima wazandiki na wachumia tumbo watataka kumwangamiza
 
Mkuu Benson Mramba, maandiko yako ya kila siku yenye ladha ile ile kumhusu Mbowe yanalenga nini hasa?

Hata kama una hoja, tunakupuuza kwakuwa unaandika kama mwenye chuki Zaidi ya mwenye hoja. Jirekebishe Mkuu. Halafu, tunaaminishwa kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa kaskazini, iweje wewe 'wa kaskazini' uwe na bifu hivyo?

Kiukweli, sasa unaboa Mkuu. Kila siku Mbowe tu, WHY HIM ONLY?
Usiseme tutakupuuza, sema nitakupuuza! Huu ujinga wa kuwaongelea wengine huwa mnautoaga wapi?
 
Kwanini usiende kwenye mamlaka sahihi kama wewe ni jembe kweli na unauhakika na maneno yako
 
I don't doubt that Mbowe has his flaws but in the way he is attacked bybthise in power it makes him an "Angel" a brave one too
 
Katika maisha yangu ndani ya CHADEMA nimewahi kusikia hili neno la NITAKUSHUGHULIKIA toka kwa Mbowe Mara kadhaa na kwa watu kadhaa na kwa kweli wote walioambiwa neno hili hawakuwa na mwisho mzuri ndani ya Chama. Nitataja wachache:-

1. Kafulila
Huyu baada ya kuambiwa neno hili alipata tabu sana. Alishawahi mpaka kuanguka ghorofani kwa hila hizi hizi. Mwishowe alifukuzwa kazi na hata wakati wa ubunge wake kwa tiketi ya NCCR bado CHADEMA iliendelea kupambana nae ili asistawi kisiasa

2. Zitto
Huyu sina haja ya kueleza sana. Kila mtu anajua alivyopachikwa sifa ya USALITI ambayo ilikuwa na lengo la kummaliza kisiasa kabisa. Alitaka kuwekewa sumu, alishakatiwa break za gari mara kadhaa, alishawekewe vijana wamdhuru, na mwishowe alifukuzwa uanachama. Kwa sababu wanajua walimzushia leo wameshirikiana nae kule Buyungu.

3. Ben Saanane

Huyu tuliondolewa nae pale makao makuu kwa hoja kuwa hatuaminiki na sisi ni watu wa Zitto pia ni wajeuri tunaringia usomi wetu. Kubaki kwetu makao makuu ingekuwa ni sawa kutengeneza akina Zitto wengine kwa miaka ya mbeleni.
Mimi nilikubali matokeo. Mwenzangu akamfuata Mbowe na kwenda kumtisha kuwa akiondolewa atatoa siri zote za mambo ambayo ameyafanya na Mbowe hususan katika kumshughulikia Zitto. (Saanane alishatuhumiwa kutaka kumuwekea sumu Zitto)

Mbowe akamuuliza unanitisha? Akamwambia usinitishe wewe jenga hoja tu. Mbowe akampa nafasi ya msaidizi binafsi (Personal assistant na mshahara mkubwa) Nafasi hii haipo kwenye structure ya Chama na tayari Mbowe alikuwa na wasaidizi wengine wanne na personal assistant wake alikuwa Mndeme ambaye alikuwa akilipwa na Bunge sio Chama. Baada ya kuona mwenzangu karudishwa kazini nikauliza kwa watu wa karibu na Mwenyekiti nikaambiwa aa huyo tutamshughulikia tu. Miezi miwili baadae nikasikia Saanane kapotea tena akitokea South Africa kumwakilisha Mwenyekiti nikajua habari imeishia hapo. MTU ulikuwa hupendwi hata kidogo leo unatumwa South Africa lazima kuna hila. Ukweli ni kuwa katika watu waliokuwa hawapendwi pale Makao Makuu na Wakurugenzi wote ni Ben Saanane Mimi nilikuwa na afadhali mara 100.

Mbowe hapendi kuzungumzia swala la Saanane na wachache niliowasikia wakilizungumzia bungeni ndio walikuwa maadui zake wakubwa Lema na Selasini na wote hawa ni watoto wa Mbowe.

4. Msafiri Mtemelwa

Huyu alikuwa ndio Mwl wa Zitto Kabwe. Huyu aliambiwa wazi wazi kabisa na Mbowe kuwa ukiendelea nitakushughulikia nje ya siasa na nje ya Chama. Uhasama ulivyozidi aliamua kuacha kazi mwenyewe na kuondoka baadae akajiunga ACT. Mtemelwa alikuwa mwenyekiti wa vijana wa NCCR mageuzi iliyokuwa na nguvu wakati huo hivyo anajua matokeo ya uhasama.

5. Mtela Mwampamba, Adam Chagulani, Juliana Shonza, Habibu Mchange, Daniel Yona n.k

Hawa wote walipata msukosuko mkali ndani ya Chama. Wengine kama Yona walitekwa na kupigwa vibaya na hatimae kutupwa ununio kule. Wengine walifukuzwa, wengine walikimbia wenyewe .

6. Mimi Mwenyewe

Baada ya kuanza kuandika mambo ya Mbowe kwenye group la viongozi wakuu iliazimiwa Tume inishughulikie maana naongea sana. Majadiliano ninayo. Mwenyekiti Mbowe aliingilia kati na kusema mambo ya usalama yasijadiliwe pale ila wataona namna bora ya kudeal na Mimi. Baadae John Mrema aliwahi kunipigia simu na kunionya kuwa wameshanivumilia sana. Haikuishia hapo akamtuma mkewe kwa mama yangu anionye kuwa anaweza kunipoteza ila sijakoma. Nawasubiria.

Aidhaa wabunge kadhaa marafiki zangu wameshanionya sana maana wanamjua Mbowe na mambo yake. Ila nimekuwa nawajibu Demokrasia maana yake ndio hiyo sio tunamlalamikia Magufuli kumbe sisi wenyewe ndio waminyaji wakubwa wa demokrasia.

7. Lissu

Mimi nimekuwa katika vuguvugu la kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya Chama tangu 2009 ambapo nilikuwa namuunga mkono kafulila kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama dhidi ya John Heche aliyekuwa anaungwa mkono na Mbowe.

Katika Uchaguzi wa mwaka huu nilikuwa na niko timu yoyote inayompinga Mbowe. Kabla Lissu hajashambuliwa niliongea na kiongozi mmoja ya Kanda kumshawishi kuwa tumuunge mkono Lissu maana ndio anaweza kupambana na Magufuli. Yule Bwana ni Timu Mbowe akaniambia huyo Lissu tutamshughulikia hataamini. Heee haikuisha wiki au wiki mbili risasi.

Mimi nikajiuliza kwanini ashambuliwa wakati wa ripoti ya makinikia? Magufuli angetaka ripoti ndio iwe habari lakini ishu ya Lissu ikaja kama destructor nikaona oooo yale yaleeee!

8. Waitara

Nae juzi kwenye kipindi cha 360 cha Clouds FM kasema alionywa atashughulikiwa kwa sababu alikuwa anamuunga mkono Lissu. Waitara kama Mbunge ameamua kukimbia mapema maana anamjua Mbowe vizuri. Alinusurika kwenye ule waraka wa mkakati wa mabadiliko maana yeye na Mimi ndio tuliotuhumiwa kuwa ni M2 ila ushahidi ulikosekana. (Mpaka kesho naunga mkono waraka ule. Bado unaishi)

Hitimisho

Mbowe anaposema NITAKUSHUGHULIKIA basi jua ni kisiasa na Kimafia. Mbowe ameshatesa, amewatweza, kuwadhalilisha wengi. Haheshimu katiba ya nchi hata kidogo. Sasa ni zamu ya Kubenea, Komu, Lissu, Lwakatare na wabunge kadhaa wa majimbo kushughulikiwa. Ni ama waache siasa au watahama na wenyewe.

Wakati Fulani nilisema bila Magufuli kumdhibiti Mbowe Wanachadema hawatamuweza na wameshamshindwa. Serikali inapaswa kuingilia kati kama ilivyofanya TFF, Simba, Yanga na kwenye Vyama vya Ushirika. Vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria ni Mali ya Umma.

Haya ni ya kweli niko tayari kuyasema hata chini ya kiapo.
Rubbish
 
Kwakweli hata yule Mawazo nadhani alitofautiana na Mbowe.
Kwa maandiko kama haya ndugu soon utakula position. Mana haya kuna wanao fufahia masikioni.
 
anyway Mbowe must step down,wapinzani wengine waweze ku emerge....yaani kama 2020 atakuwepo CHADEMA itakuwa imekwisha kabisaa,sasa ni chaguo ni lake,kustep down chama kipate new politicians hivyo new directions,au ang'ang'anie chama kife kabisaa akose hata anachokipata sasa hivi...
Jemedari makini hawezi kuliacha jeshi lake kwenye mapambano makali km haya!!! Chadema wanamhitaji mno mbowe kipindi hiki kuliko wakati wowote ule
 
Kwa mujibu ya intelejensia yangu makini mleta mada yupo nakuru kenya amejificha!!
 
Back
Top Bottom