Mbowe anapaswa awaombe radhi Watanzania

Mbowe anapaswa awaombe radhi Watanzania

bahati mbaya kesi imeondolewa na mahakama.
haijatamkwa kama mbowe hana hatia ya Ugaidi, hivyo Mbowe bado anazo tuhuma za ugaidi kwa kuwa mhakama haija thibitisha vinginevyo.
Kama gaidi anaitwa Muheshimiwa na ikulu anaitwa huu utakuwa ujuha wa kiwango cha lami
 
Sijakuelewa mkuu aombe radhi kwa kutuhumiwa tuhuma za uongo? Yaani wewe utuhumiwe kuwa ni shoga huko kitaani kwenu halafu uombe radhi?
nani kasema zilikuwa tuhuma za uongo au za kweli?....... .
 
Naamini Mbowe na wenzake ni waumini wazuri hivyo njia pekee aliyo nayo baada ya sakata hili ni kutubia mbele za Mungu na kuwaomba radhi watanzania.
UNachanganya Sana mkuu, Umesema Suala hili analijua yeye na Mungu wake; Sasa inakuwaje tena unasema aombe msamaha? wewe unajuaje kwamba ametenda kweli ama hajatenda ????
 
nani kasema zilikuwa tuhuma za uongo au za kweli?....... .
Aliyempa tuhuma ndie kamwachia, kaitwa ikulu halafu Mh raisi akamwita Muheshimiwa mbowe, toka lini gaidi akaitwa muheshimiwa tena raisi ndio katamka hivyo. Ulitaka mbowe afie jela kama yule nyapara wa malaika alivyodedi
 
Waliombambika kesi ya ugaidi ndo yapaswa wawaombe radhi watz
 
Waswahili husema; " uungwana ni vitendo",

pamoja na mashitaka yaliyo kuwa yanamkabili kuondolewa na DPP iwe kwa sababu yoyote ile lkn kwa kuwa tuhuma zilizo kuwa zinamkabili zililenga kuhatarisha amani na usalama wa watanzania basi naona ni vyema Mbowe akaomba radhi watanzania na ninaamini watanzania wote watamsamehe na kumpokea.

Hatua hii inahitaji uadilifu wa kiroho zaidi sio wa kisheria, hapa sasa sio mahakamani bali ni kati ya roho yake na Mungu wake, inawezekana wafuasi wake wakawa wanamtetea kwa nguvu sana na kuweza kuuaminisha umma kuwa tuhuma zilizo kuwa zinamkabili ni za uongo lkn Mbowe mwenyewe ndiye anaye jua zaidi kuliko mwengine.

Naamini Mbowe na wenzake ni waumini wazuri hivyo njia pekee aliyo nayo baada ya sakata hili ni kutubia mbele za Mungu na kuwaomba radhi watanzania.
hakika Mungu atamsamehe na watzania wote tutamsamehe na tutampokea.

Njia pekee ya kuwaunganisha watanzania wote baada ya sakata hili ni kuwaomba radhi watanzania kwa yote yaliyo tokea na sio kuleta utetezi na lawama, maana katika jambo hili kuna watanzania wanao amini kuwa Mbowe alikuwa na mipango ya kuharibu amani ya nchi lkn pia wapo amabo hawaamini tuhuma hizo, hivyo njia pekee kwa mbowe ni kuwaomba radhi wale walio kwazika na tuhuma hizo na kwa pamoja tutasonga mbele.
nami kwa niaba ya watanzania wenzangu tupo tayari kumsamehe na kumpokea.

Mbona nyie hamjaomba msamaha kwa kumlima risasi Lissu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom